Jumapili, 30 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Bila Mfumo wa Elimu ya Kiislamu, Haramu inakuwa ni Sharti la Kusoma

Mnamo tarehe 16 Novemba, gazeti la Times la India liliripoti kwamba Chuo Kikuu cha Uttarakhand Sanskrit huko Haridwar kimeanzisha hatua za kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Upeo juu ya mavazi ya wanafunzi ndani ya chuo kikuu na madarasani, Makamu wa Chansela wa Chuo Kikuu Dinesh Chandra Shastri aliiambia TOI mnamo Alhamisi. Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko kuwa “wanafunzi kadhaa wa Kiislamu wa kike wanaendelea kuvaa burka au hijabu wakiwa chuo hicho kikuu.”

Baada ya Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki (na Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu), Watawala wa Ruwaibidha Wakusanyika Tena Kuendeleza Kejeli na Usaliti wao

Ni mwaka mmoja kamili baada ya watawala wa Waarabu na Waislamu kukusanyika kujadili kadhia ya Palestina kufuatia mkasa wa Oktoba 7, wanakutana tena mahali pale pale, pamoja na mtu yule yule, wakishughulikia tatizo lile lile, na hatimaye kutoa maazimio yale yale! Zaidi ya viongozi 50 wa dola za Waislamu walihudhuria Mkutano wa Waarabu na Waislamu mnamo tarehe 11/11/2024, akiwemo Waziri Mkuu wa Malaysia. Kwa kutabiriwa, mapendekezo yaliyochakaa yaliwasilishwa, na Mkutano huo ulihitimishwa kwa maazimio yaliyochakaa vilevile. Kikubwa kinachotolewa na watawala hao ni kulaani mauaji ya halaiki ya Gaza na ‘Israel’ na kuomba Umoja wa Mataifa (UN) - shirika lile lile lililohusika na kuzaliwa kwa umbile halifu la Kiyahudi.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi “Gaza Inamwachia Mwenyezi Mungu Kiwango cha Usaliti jijini Riyadh na inataka Msaada kwa Umma na Majeshi yake!”

Matembezi ya hamsini na nane ya kunusuru Palestina na mateka Al-Aqsa, ambayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, chini ya kichwa “Gaza Inamwachia Mwenyezi Mungu Kiwango cha Usaliti jijini Riyadh na inataka Msaada kwa Umma na Majeshi yake!”

Watawala wa Iran ni Uhalisia tu wa Sauti na Maonyesho ya Fataki Hawana Uhusiano Wowote na Ushindi au Ukombozi

Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Meja Jenerali Hossein Salami, alithibitisha katika ufunguzi wa mazoezi ya mapambano ya usalama ya “Nasrallah” kwamba “umbile la Kizayuni linakosea ikiwa linadhani kuwa Hizbullah itatoka nje ya uwanja kwa kuwauwa viongozi wake,” na kubainisha kuwa “chama hicho ni vuguvugu kubwa ambalo haliwezi kuzimwa wala kumalizwa.” Akalitisha umbile la Kiyahudi kwa kusema: “Leo tuna nyinyi machoni mwetu, na tutapigana mpaka mwisho, na hatutakuruhusuni kudhibiti hatma ya Waislamu, na tutalipiza kisasi, nanyi mtapata pigo chungu, na lazima musubiri.”

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu