Jumanne, 27 Shawwal 1447 | 2026/04/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Taarifa ya Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan katika Mkutano na Waandishi wa Habari Wenye Kichwa: “Usimamizi wa Amerika wa Mgogoro wa Sudan Unazidisha Majeraha na Kugawanya Nchi”

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Katibu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Muawiya Othman, kufuatia ziara ya Mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Utawala na Kamanda wa Jeshi, Luteni Jenerali Burhan, nchini Saudi Arabia, Muawiya alisema mnamo Jumatatu jioni, 15/12/2025: “Rais alielezea shukrani zake kamili kwa azimio la Rais wa Marekani Donald Trump la kushiriki katika juhudi za kufikia amani na kukomesha vita nchini humo, kwa ushiriki wa Ufalme wa Saudi Arabia. Mheshimiwa alithibitisha nia ya Sudan kufanya kazi na Rais Trump, Waziri wake wa Mambo ya Nje, na Mjumbe wake Maalum wa Amani nchini Sudan, ili kufikia lengo hili zuri bila shaka.”

Mwaliko wa Kuhudhuria Mkutano na Waandishi wa Habari

Tunafurahi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, kuwaalika wataalamu wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wanaopenda masuala ya umma kuhudhuria mkutano na waandishi wa habari ambapo Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan atazungumza chini ya kichwa: “Usimamizi wa Amerika wa Mgogoro wa Sudan: Kuongeza Majeraha na Kugawanya Nchi”

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Kiongozi wa Al-Ikhwan Al-Muslimina Hassan Abdel Hamid

Jana, Ijumaa 19/12/2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh AbduAllah, Mratibu wa Kamati hiyo, ulikutana na Ustadh Hassan Abd Al-Hameed kiongozi katika Al-Ikhwan Al-Muslimina nchini Sudan.

Vyombo vya Usalama Vyawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kutoa Wito wa Kutibua Mpango wa Amerika wa Kutenganisha Darfur

Kikosi kutoka kwa vyombo vya usalama kiliwakamata Mashababu watano (wanachama) wa Hizb ut Tahrir katika mji wa Al-Shawak, ambao ni: Othman Al-Amin Kanda, Hassan Al-Amin Kanda, Muhammad Thamin Adam, Ahmad Babikr, na Al-Amin Abdullah. Hili lilikuja kufuatia Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan kufanya kisimamo mbele ya Msikiti wa Kale huko Al-Shawak, ambapo Sheikh Othman Al-Amin Kanda, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, alihutubia hudhuri ya watu mashuhuri wa eneo hilo na umma kwa jumla. Katika hotuba yake, alielezea hatari ya mpango wa Marekani unaotaka kuigawanya Sudan kwa kuikata Darfur, akiwapa wale waliohudhuria jukumu la Kisharia linalofanya umoja wa Ummah na umoja wa dola kuwa suala nyeti. Baadhi ya watu mashuhuri walishiriki kwa kutoa kauli zinazothibitisha msimamo wao na pamoja na hizb ili kuzuia mpango wa kujitenga.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu