Alhamisi, 21 Rabi' al-awwal 1443 | 2021/10/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mashirika ya Kimataifa Hayaepuki Mapendeleo

(Imetafsiriwa)

Habari:

Aljazeera iliripoti kuwa, "Fikra kwamba janga la virusi vya korona ilichipuza kwa bahati mbaya kupitia wafanyikazi wa maabara ya China imeibuka tena", kufuatia makala ya Runinga ya Denmark mnamo tarehe 12 Agosti, 2021 ambayo kwayo Peter Ben Embarek, mkuu wa timu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) iliyopewa jukumu la kuchunguza vyanzo vya ugonjwa wa virusi vya korona, ilipendekeza nadharia kwamba "Mfanyakazi mmoja wa maabara aambukizwe wakati anafanya kazi  ndani ya pango la popo kukusanya sampuli. Hali kama hiyo, huku ikiwa ni mvujo wa maabara, pia huenda ingefaa nadharia yetu ya kwanza ya maambukizi ya moja kwa moja ya virusi hivi kutoka kwa popo hadi kwa binadamu. Hii ni nadharia ambayo tunaona kuwa inawezekana zaidi.

Maoni:

Maoni ya Peter Ben Embarek yamezua utata kwa sababu timu hiyo ya WHO iliripoti matokeo yake mnamo Februari ikisema kwamba chanzo cha maabara "hakiwezekani pakubwa". Tangu wakati huo, mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema kuwa uamuzi kuwa sio mvunjo wa maabara "ungali mchanga". Embarek alielezea kuwa uondoaji wa timu hiyo wa nadharia ya mvujo wa maabara ulitokana na shinikizo kutoka kwa wanasayansi wa China kwenye timu ya WHO ambao mwanzoni walikataa kuruhusu majadiliano juu ya uvujaji wa maabara, lakini mwishowe wakakubali maridhiano ambapo nadharia hiyo ingetajwa katika ripoti kama "uwezekano mchache mno" badala ya kuwa haiwezekani, lakini "kwa sharti kuwa hatungependekeza utafiri wowote maalum ili kuendeleza nadharia hiyo."

Wale ambao wanafurahi kugundua njama ya WHO, na vile vile wale walioshtushwa kwamba WHO inaweza kushawishiwa na nchi moja kuchakachua matokeo yake, wote wameshindwa kufahamu WHO ni nini na inafanya kazi vipi. Ndio, ni shirika la kimataifa, lakini hiyo haimaanishi kuwa linaweza kutotegemea nchi ambazo zimejiunga nayo. Kila nchi ina maslahi yanayogongana na yale ya nchi zengine na migongano hii kimaumbile hujitokeza katika timu na kamati ambazo zinafanya kazi ya shirika la kimataifa au shirika linalodhaniwa kuwa na ushawishi wa kimataifa.

Licha ya Amerika kuwa uchumi nambari moja ulimwenguni na licha ya vitisho vya rais wa zamani Trump, wanasayansi wa China kwenye timu hiyo walianzisha ulainishaji wa maneno ya ripoti ya Februari ili kuzuia kumpa risasi Trump kuifyatulia China wakati alipokuwa akiilaumu China kwa kuanzisha janga hili la maambukizi. WHO inafanya kazi kupitia makubaliano ya pamoja, ambayo inamaanisha kuwa maridhiano juu ya msingi na ukweli-nusu hayawezi kuepukika kwa sababu ya utulivu. Fauka ya hayo, ujenzi wa makubaliano ya pamoja ni wa polepole na kamati nyingi mara nyingi hulisha maneno ya mwisho ya shirika hilo, ambayo huandikiwa kwa uangalifu na kwa hamu ya kutomshambulia yeyote.

Hivyo basi, huku nchi nyingi zikiwa zimesaidiwa na msaada wa shirika la kimataifa lenye utaalam na rasilimali ambazo nchi masikini hazina, serikali binafsi hazipaswi kamwe kutelekeza jukumu lao kwa ripoti au kamati ya WHO na kila moja inapaswa kuamua ni lipi lenye manufaa kwa raia wake. Mbali na kuwa nuksani kama wanadamu wenyewe wanaolifanyia kazi yake, limejengwa chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, juu ya maadili na fahamu za Kimagharibi ambazo zinatangazwa kuwa za kiulimwengu. Lakini, kama maadili hayawezi kuthibitishwa kutoka kwa makisio yoyote ya kiulimwengu, hakuwezi kuwa na maadili yoyote ya kikweli ya kiulimwengu, na kwa hivyo heshima kwa shirika ambalo limejengwa juu ya maadili kama hayo ina hatari ya kutawaliwa. Kwa kuwa afya na ustawi wa binadamu unazingatiwa kama jambo la jumla katika Uislamu na kama vile WHO pia ina mtazamo mpana afya zaidi ya fiziolojia na viungo vya mwili, Waislamu wanapaswa kuwa waangalifu juu ya mizozo ya kimaadili katika baadhi ya nyanja za afya.

Ama kuhusu asili ya SARS Coronavirus-2, bado lingali ni swali lililo wazi la ima ni ajali ya maabara au kuambukizwa kwa wanasayansi wanaokusanya sampuli za virusi kutoka kwa popo kwenye misitu ya China na kuvipeleka virusi kwa idadi ya watu wa Wuhan na kisha ulimwengu, au ima maambukizi ya awali yalikuwa huru na uchunguzi wa kisayansi wa Kichina. Huu sio mfano wa kwanza wa virusi kuenea kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu, na kusababisha janga la maambukizi la kiulimwengu, na labda hautakuwa wa mwisho.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu