Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Nchi za G20, kama inavyo tarajiwa, Zimejikwaa juu ya Hali ya Hewa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kuna simu nyingi, lakini ahadi chache thabiti. Hivi ndivyo mazungumzo ya nchi za G20 kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa yalivyomalizika.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliita tangazo la G20  "maendeleo ya wastani" tu. Alitoa wito wa kuchukua hatua madhubuti zaidi kwa washiriki katika Kongamano la Umoja la Mataifa wa Hali ya Hewa jijini Glasgow:

"Ikiwa Glasgow itafeli, basi kila mtu atafeli. Makubaliano ya Paris yatasambaratika kwa hesabu za mwanzo mwanzo kabisa, njia pekee inayofaa ulimwenguni ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa itazama ..."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisema kuwa matokeo ya kongamano hilo hayajafikia matarajio yake. Chanzo: https://ru.euronews.com/2021/10/31/g20-climate-final-ppp-blow

Maoni:

Kwa kweli, kufeli kwa mkutano huu hakushangazi.

Kabla ya hili, G-20, G-7, UN, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine sawa hayakuwa na nguvu katika mapambano dhidi ya matatizo muhimu zaidi na ya kimataifa yanayowakabili wanadamu.

Ikiitwa kukabiliana na kuibuka kwa mizozo na vita vipya vya kimataifa, Umoja wa Mataifa (na kabla ya hapo Ushirika wa Mataifa) ilikuwa ni chombo tu mikononi mwa dola kuu cha kuendeleza maslahi yao ya kibinafsi, ambayo hatimaye ilipelekea kuibuka kwa mizozo mibaya ya umwagaji damu zaidi duniani, vita, mauaji ya halaiki, mauaji ya kikabila na njaa ...

Umaskini, njaa, kiwango cha chini cha huduma ya matibabu duniani, kutopatikana kwa elimu, miji mikubwa na nchi zote zimechoka kutokana na matatizo ya mazingira, yote haya ni karata ya ziara ya ulimwengu wa kisasa, ambayo ilitolewa na mfumo wa kirasilimali, ambayo inasifiwa na wanachama wa G20, G7, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mashirika mengine.

Viongozi wanaoelezea wasiwasi wao kwamba matokeo ya mkutano wa Glasgow hayakufikia matarajio ni viongozi wale wale wa mashirika anuwai na nchi kubwa ambao hapo awali walishindwa kutatua changamoto zaidi za kiulimwengu, ni viongozi hawa ndio wanaohusika na hasara kubwa ya maisha katika maeneo mbalimbali ya dunia kutokana na vita, njaa na mauaji ya halaiki.

Je, inawezekana kulinda mazingira kwa kile kinachoitwa jumuiya ya kimataifa ikiwa kabla haikuweza kulinda mamia ya maelfu na hata mamilioni ya wanawake, watoto na wazee kutokana na kifo?

Kwa hivyo, kushindwa kwa mkutano huu wa G20 kunatarajiwa na hakupasi kusababisha mshangao wowote. Bila shaka, ulinzi wa mazingira, wanyama walio katika hatari ya kutoweka, nk. unawezekana tu ndani ya kivuli cha Khilafah Rashida, mfumo wa Mwenyezi Mungu na nidhamu ya kisiasa ya kimungu, ambayo kimsingi itashughulikia maisha ya mwanadamu, ubora, ustawi na kisha kuchunga malengo ambayo yametajwa katika kile kinachoitwa "Mkataba wa Paris".

#أزمة_البيئة     #EnvironmentalCrisis

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazyl Amzayev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu