Ijumaa, 04 Rabi' al-awwal 1444 | 2022/09/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gaza Yaungua, Huku Majeshi Yakitazama!

(Imetafsiriwa)

Habari:

hashtag غزة_تحت_القصف#  “#Gaza_under_seige” imevuma kwenye Twitter.

Maoni:

Majeshi ya Misri, Jordan, Hijaz na Uturuki yanawatazama Mayahudi wakiupiga mabomu Ukanda wa Gaza, lakini hawahamasiki, kana kwamba jambo hilo haliwahusu!

Enyi Majeshi ya Waislamu: Kwa nini hamuitikii amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, anayesema:

(وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ)

 “Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni” [Surah Al-Baqarah 2:190].

Hivi, kwa nini hamjikusanyi katika kuwanusuru Waislamu na kuwakomboa kutoka katika uvamizi na ukafiri?!

Watawala hawa hawatakunufaisheni Siku ya Kiyama, kwani watakurukeni, na majuto hayatakufaeni. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُواْ مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ وَرَأَوُاْ الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُواْ لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّؤُواْ مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُم بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ)

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. (166) Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni. (167) [Surah Al-Baqarah 2:166-167].

Kukuteni vumbi la udhalilifu kutoka kwenu. Musiwatii vibaraka wa Magharibi kafiri. Wang'oeni na muwaweke watu wanyofu watakaokuongozeni kuelekea kwenye ukombozi wa ardhi yenu na kuregesha izza kwa Ummah wenu.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Surah Al-Anfaal 8:24].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdul Aziz Al-Munais – Idara ya Habari katika Wilayah Kuwait

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu