Alhamisi, 15 Jumada al-awwal 1444 | 2022/12/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 

Shambulizi la Kitambulisho kwa Vijana wa Kashmir

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 24 Septemba 2022 Muttahida Majlis-e-Ulema (MMU), muungano wa makundi ya kidini na kijamii katika Bonde la Kashmir, mnamo Jumamosi walisema majaribio yalikuwa yanaendelea "kuhujumu kitambulisho cha Waislamu wa Kashmir". MMU ilipanga mkutano katika Msikiti wa Jama wa Srinagar ili kujadili hatua za hivi majuzi za kuanza kuimba nyimbo za Kibaniani na Surya Namaskar katika taasisi za elimu za Bonde hilo.

Maoni:

Mapambano ya miaka 75 ya Waislamu wanaoishi chini ya ugaidi wa ukandamizaji wa serikali ya India yameongezeka hadi kuwa ufunzaji itikadi kali zaidi kwa vijana katika jaribio tasa la kudhoofisha hamasa za Kiislamu na kitambulisho cha Waislamu katika eneo hilo.

Hatua za sasa zinafuata njia sawa na ya China na Ufaransa kufuta mawazo na fikra zinazowafanya Waislamu kuwa imara na nguvu dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na hofu vinavyotumika kuudhibiti Umma duniani.

Msemaji wa MMU alisema kuwa azimio la pamoja lilipitishwa "kuelezea wasiwasi mkubwa na wa kina juu ya majaribio yanayofanywa ya kudhoofisha kitambulisho cha Waislamu wa 'Bonde hili la Watakatifu .... MMU inajutia sana shughuli zinazotekelezwa kupitia shule na taasisi za elimu zinazolenga kuendeleza ajenda ya Hindutva huko Kashmir. Kwa jina la yoga na maombi ya asubuhi, wanafunzi wa Kiislamu wanafanywa kuimba bhajans na wakati mwingine kuulizwa kufanya Surya Namaskar. Hili ni kinyume na misingi ya desturi zetu za kidini.”

Katika ombi la MMU kwa serikali kuondoa mara moja maagizo yake na kuacha tabia hizi ilisema; “Wazazi, ikiwa watoto wenu watalazimishwa kushiriki katika amali zisizo za Kiislamu katika shule za serikali, mnapaswa kuwaondoa watoto wenu. Tunawahimiza walimu wa Kiislamu kuepuka kuendeleza amali hizo zisizo za Kiislamu na waipe upendeleo imani yao.”

Haja ya wakati huu sio tu kukataliwa kwa desturi mpya za kithaqafa zinazo lazimishwa kwa watoto wetu, lakini mfumo mpana utakaoruhusu utekelezaji kamili wa mifumo yote ya Uislamu, sio tu mifumo ya elimu. "Shule za Kiislamu" nchini Uingereza zinakabiliwa na tatizo la maafisa wa serikali kuangalia kwamba viwango fulani vinadumishwa katika usomeshaji jambo ambalo linaweza kusababisha mgongano na kitambulisho cha Kiislamu kwa vijana, haswa katika masuala ya kitambulisho cha kijinsia na mahusiano ya kijamii. Hatuwezi kusahau madhumuni ya vijana kubeba Dini ya Haki hadi kote ulimwenguni, jambo ambalo maadui wa Uislamu wanalijua vyema. Sisi kama wazazi lazima tutekeleze njia iliyonyooka kwenda Peponi katika vijana wetu na tunahitaji Khilafah ili kulinda usafi wa elimu.

(وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ)

“Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu” [At-Tawbah: 71]

 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu