Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Afya ya Watoto wa Umma iko Hatarini bila ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 20 Oktoba 2022, BBC iliripoti kwamba Indonesia imepiga marufuku uuzaji wa dawa zote za kikohozi za watoto baada ya watoto 99 kufariki kutokana na kufeli kwa figo. Iligunduliwa kuwa viwango vya juu vya sumu haramu vilikuwepo ndani ya dawa zilizochafuliwa. Maafisa wanahofia kwamba idadi kamili ya vifo haijajulikana kwani dawa hizo zilikuwa na mzunguko mkubwa.

Kisa hiki cha kuhuzunisha kinakuja wiki chache tu baada ya dawa ya kikohozi nchini Gambia kuhusishwa na vifo vya karibu watoto 70.

Shirika la Afya Duniani (WHO) liligundua dawa zinazotumiwa huko - zilizotengenezwa na kampuni moja ya dawa ya India zilikuwa na "kiasi kisichokubalika" cha kemikali ya diethylene glycol na ethylene glycol. Dawa hizo "zimehusishwa pakubwa na majeraha makali ya figo" (AKI).

Waziri wa Afya wa Indonesia alisema misombo mithili ya hiyo ya kemikali pia ilipatikana katika baadhi ya dawa zinazotumiwa nchini humo. Maafisa wa afya wa Indonesia walisema wameripoti takriban visa 200 vya AKI kwa watoto, wengi wao wakiwa na umri wa chini ya miaka mitano. (BBC)

Maoni:

Haja ya udhibiti wa kimataifa katika mbio za usambazi katika maduka ya dawa ina maanish kuwa shughuli za utengenezaji zisizo adilifu zipo kote ulimwenguni aghlabu ufisadi wa serikali ukichochea hili.

Hivi sasa katika mgogoro wa UVIKO nyaraka nyingi zilizovuja zimeonyesha jinsi chanjo zilivyosambazwa sana bila hatua za kawaida za majaribio zichuma mabilioni ya dolari kwa washikadau waliohusika. Hadi sasa hakuna hata mmoja kati ya pande hizi aliyefikishwa mahakamani kwa jinai hizi dhidi ya watu walio hatarini zaidi na wasio na hatia wa Ummah wetu.

Kashfa ya makampuni yenye ulafi kutumia idadi ya watu duniani kama maabara ya upimaji wa binadamu haijadhibitiwa na tunaweza tu kutarajia vifo vingi zaidi na majeraha kutokea.

Katika muundo sahihi wa Kiislamu, maisha na hadhi yake takatifu inalindwa tukiwa na utulivu wa kutokiuka.

Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika hotuba yake ya kuaga:

«أَلَا أَيُّ شَهْرٍ تَعْلَمُونَهُ أَعْظَمُ حُرْمَةً» “Ni mwezi upi mnaoujua kuwa utukufu zaidi?” Wakasema, “Ni mwezi huu wetu, Dhul Hijjah.” Mtume akasema:

«أَلَا أَيُّ بَلَدٍ تَعْلَمُونَهُ أَعْظَمُ حُرْمَةً» ““Ni mji upi mnaoujua kuwa mtukufu zaidi?” Wakasema, “Ni mji huu wetu, Makka.” Mtume akasema:

«أَلَا أَيُّ يَوْمٍ تَعْلَمُونَهُ أَعْظَمُ حُرْمَةً» “Ni siku ipi mnayoijua kuwa na utukufu zaidi?” Wakasema, “Ni siku hii yetu, Arafat.” Mtume akasema:

«فَإِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى قَدْ حَرَّمَ عَلَيْكُمْ دِمَاءَكُمْ وَأَمْوَالَكُمْ وَأَعْرَاضَكُمْ إِلَّا بِحَقِّهَا كَحُرْمَةِ يَوْمِكُمْ هَذَا فِي بَلَدِكُمْ هَذَا فِي شَهْرِكُمْ هَذَا أَلَا هَلْ بَلَّغْتُ؟»

“Basi hakika, Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha juu yenu, damu zenu, mali zenu, na heshima zenu, isipokuwa kwa haki yake, mithili ya (uharamu kutokana na) utukufu wa siku yenu hii, na mji wenu huu, ndani ya mwezi wenu huu. Je, nimefikisha ujumbe?” Kisha Mtume akasema:

«وَيْحَكُمْ أَوْ وَيْلَكُمْ لَا تَرْجِعُنَّ بَعْدِي كُفَّارًا يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ»

“Ole wenu! Msiregee baada yangu mkawa makafiri, mukikatana shingo nyinyi kwa nyinyi.” (Sahih Bukhari)

Kurudi kwa muundo wa muongofu wa Khilafah kutahakikisha kanuni sahihi zimewekwa ili kulinda maisha ya watoto wapendwa wenye thamani katika Uislamu. Kina mama wa Ummah huu wanaomboleza kwa kufiwa na watoto wao ovyo ovyo kutokana na kukosekana Amir wa waumini wa kutekeleza kivitendo Quran na Sunnah duniani na kutoibakisha tu katika kurasa za Quran.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu