Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kizazi Kichanga - Mshawishi katika Kusimamisha Uislamu

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uteuzi wa Dato Seri Anwar Ibrahim kuwa Waziri Mkuu wa 10 wa Malaysia hatimaye umemaliza kipindi cha siku 5 cha ‘wadhifa wazi wa serikali’ baada ya Uchaguzi Mkuu wa 15 (GE15). Mfalme wa Malaysia, Yang di-Pertuan Agong Sultan Abdullah Ri’ayatuddin Al-Mustafa Billh Shah, ameridhia uteuzi huu na kuanzishwa kwa serikali ya umoja ya Malaysia. Ingawa hakuna chama au muungano wa vyama wa kipeke yake ulioweza kuunda idadi ya wengi bungeni, kuna shaka kidogo kwamba matokeo ya uchaguzi yalitegemea kwa kiasi kikubwa kuhusika kwa wapiga kura vijana katika GE15. Katika GE15, usajili wa kiotomatiki wa wapigakura kwa Mmalaysia yeyote ambaye amefikisha umri wa miaka 18 uliidhinishwa, hivyo basi kubadilisha idadi ya wapigakura kwa kiasi kikubwa. Hili bila shaka limebadilisha hali ya kisiasa ya nchi huku vyama vya kisiasa vikibadilisha mbinu zao katika kuvutia wapiga kura na tunaweza kuwa na uhakika kwamba serikali ijayo ya umoja itakuwa inazingatia mahitaji ya vijana kudumisha uungwaji mkono kutoka kwa kizazi hiki muhimu.

Maoni:

Kuhusiana na idadi ya wapiga kura vijana wa GE15, jumla ya wapiga kura vijana milioni 10.6 walirekodiwa (umri wa miaka 18-40), ambayo ni 58.5% ya wapiga kura milioni 21.1 waliojiandikisha. Idadi kubwa ya maeneo bunge yanakaliwa na wapiga kura vijana na ukweli huu ulikuwa na ushawishi mkubwa katika mbinu za vyama vya kisiasa vinavyogombania. Vinaweza kuonekana vikiangazia wagombezi wachanga na kuwaondoa wagombezi wakongwe ingawa ushawishi wa wakongwe hawa bado unaweza kuhisiwa. Zaidi ya hayo, masuala ambayo yanachezeshwa kabla ya GE15 yanahusu wasiwasi wa vijana kama vile kuongezeka kwa gharama ya maisha, ukosefu wa ajira, elimu, utulivu wa kisiasa, ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka.

Kiuhalisia, vijana sio tu kwamba wanawakilisha mustakbali wa nchi yoyote, wao ndio mawakala wakuu wa jamii wa kuleta mabadiliko na maendeleo. Huku hali ya kisiasa ya sasa ikitawaliwa na kanuni chukivu za kidemokrasia za kisekula, sio vigumu kuona kizazi kichanga, kwa nguvu zao, kikielekezwa kwenye njia ambazo zinaweza kuwa na uharibifu katika siku zijazo. Hivyo basi ni muhimu sana kwamba kizazi hiki kielekezwe kwenye kuukumbatia Uislamu kwa ukamilifu wake ili kuvunja minyororo ya usekula ambayo imewafunga dhidi ya kuelekeza uwezo wao kwenye mwamko wa Kiislamu. Nishati inayomilikiwa na kizazi hiki ina uwezo wa kubadilisha jamii kwa ukali ikilinganishwa na kizazi kikongwe. Hili linaweza kuonekana si tu kwa upande wa nishati ya kimwili, lakini pia katika upande wa kiroho na kiakili. Ni wakati wa ujana wetu ndipo tunaanza kutafuta kitambulisho chetu na kukuza michakato ya kifikra ambayo itadumu maisha yetu yote. Ni katika kipindi hiki ambapo ikiwa kijana ataongozwa kuelekea mwelekeo sahihi na mchakato sahihi wa kifikra na kitambulisho sahihi, atashuhudia mlipuko wa uwezo ndani yao. Kwa hiyo, ili kuwaamsha Waislamu na kufikia nahdhah, mambo ya vijana yanapaswa kutiliwa mkazo sana. Hili ni suala muhimu sana ambalo tunapaswa kuzingatia - kuhakikisha maendeleo sahihi ya vijana wetu ili uwezo wao uweze kupatikana kikamilifu.

Ili kuzalisha vijana ambao wanaweza kukabiliana na msukosuko wa mwamko wa Kiislamu, tunahitaji kuzingatia jinsi Mtume (saw) alivyotangamana na kundi hili mwanzoni mwa da’wah yake. Alichoonyesha Rasulullah (saw) ni wahyi kwetu kuufuata na inatosha kuangalia jinsi kizazi cha vijana kilivyobadilishwa kutokana na da’wah yake. Waislamu wengi wa mwanzo walikuwa kizazi cha vijana - Sayyidina Abu Bakar alisilimu akiwa na umri wa miaka 37, Sayyidina Umar al Khattab akiwa na umri wa miaka 26, Talhah Ubaidillah akiwa na miaka 11, Mus'ab Umair akiwa na miaka 24 na Al-Arqam Abi Arqam akiwa na umri wa miaka 12. Kila mmoja wao alikuwa na nguzo madhubuti ya aqidah na fikra za Kiislamu na walidumisha Iman na kujitolea kwao hadi mwisho wa maisha yao.

Vile vile Mtume (saw) alipokuwa Madina, vijana ndio waliomhami katika da’wah yake. Wakati wa Vita vya Uhud, kijana, Anas Ibnu Nadhar, alikuwa tayari kujitolea muhanga nafsi yake kama ngao na akapata majeraha 80 ya kudungwa ili kumlinda Mtume (saw). Vijana hawa ni watu muhimu katika kueneza Uislamu na katika kuiamsha jamii ya Waarabu kutokana na ujinga. Kizazi chetu kichanga lazima kiwe na ufahamu mpana wa Uislamu na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa mikono yao, tutabarikiwa kwa kusimamisha dola ya kweli ya Kiislamu, Khilafah kwa njia ya Utume.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu