Jumanne, 29 Sha'aban 1444 | 2023/03/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Badala ya Kuwaita Mabalozi, Viota vya Ugaidi, hadi Wizarani, Wanapaswa Kufukuzwa Mara Moja

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uturuki: Mabalozi wa nchi 9, zikiwemo nchi zilizosimamisha kazi za ubalozi wao nchini Uturuki kwa kisingizio cha tishio la vitendo vya kigaidi, waliitwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje. Mabalozi hao waliambiwa kwamba "Vitendo kama hivyo vya wakati mmoja havijumuishi njia ya usawa na ya busara." (TRT Haber, 03.02.2023)

Maoni:

Mabalozi na wawakilishi wa Uholanzi, Uswisi, Uswidi, Uingereza, Ujerumani, Ubelgiji, Ufaransa na Italia, ambao walitoa tahadhari ya usalama kwa Uturuki na kisha kufunga kwa muda baadhi ya uwakilishi wao wa kidiplomasia na kibalozi, waliitwa kwa Wizara ya Mambo ya Nje. Maonyo haya yalitolewa ili kutia shinikizo kwenye uchaguzi na kujenga mazingira ya hofu katika rai jumla. Badala ya kutoa jibu la kweli na linalofaa, Uturuki, kama kawaida, ilitoa majibu dhaifu na ya kiuoga kwa nchi hizo za Ulaya, haswa Uingereza.

Kama inavyojulikana, balozi za nchi ndogo na kubwa za kigeni katika nchi za Kiislamu, ikiwemo Uturuki, ni viota vya ugaidi na ndio wanaobuni na wafuasi muhimu zaidi wa ugaidi. Nchi za kigeni zinafanya vitendo vya kigaidi dhidi ya raia katika nchi za Kiislamu na mawasiliano yao na makundi ya kigaidi kupitia balozi na mabalozi. Ukweli kwamba walitahadharisha juu ya ugaidi dhidi ya Uturuki ni uthibitisho tosha kwamba wanawasiliana na makundi ya kigaidi, kwamba wanayaelekeza na kwamba wanapata habari kupitia vibaraka wao. Haiwezekani kwa nchi kama Uturuki isijue hili. Waziri Çavuşoğlu alisema, "Tunafikiri kwamba kufungwa huku kuna kusudio." Kauli hii ni ishara kuwa Uturuki inalijua hili.

Wakati huo huo, badala ya kujibu kwa uzembe na bila huruma na badala ya kuwafukuza mabalozi wao nchini na kufunga balozi zao ambazo ni maeneo ya ugaidi, inastahiki kwa nchi zenye hofu, uoga na utegemezi kama Uturuki kuzijibu nchi za Ulaya kwa uoga, na hasa Marekani, inayozalisha, kulisha na kuchochea ugaidi, na kuandaa vitendo vya kigaidi nchini Uturuki kwa miaka mingi. Ingawa usalama na ustawi wa watu wake unapaswa kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake, si kingine bali ni kuvujisha wito kwa balozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na kuutumia kama nyenzo ya sera ya ndani. Iwapo usalama wa watu wake ungekuwa miongoni mwa vipaumbele vyake, angewatangaza mara moja kuwa ni watu wasiofaa kuwepo na kuwataka waondoke nchini, badala ya kuwaita mabalozi wa nchi za kigaidi kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na kuwakinaisha kuwa hakuna tishio kama hilo au kuwauliza taarifa na nyaraka kuhusiana na tishio la kigaidi walilotahadharisha. Ukweli kwamba haikulipiza kisasi unathibitisha kwamba majibu ya Uturuki yalikuwa ya kioga.

Leo hii, sababu pekee inayozifanya nchi za kikafiri za kikoloni zifanye operesheni dhidi ya nchi yetu, kulisha na kuchochea mashirika ya kigaidi, na kutoheshimu utukufu na adhama ya ummah, ni majibu dhaifu ya watawala wasaliti na vibaraka waoga katika nchi za Kiislamu. Lau wangejibu kwa ujasiri na ushujaa, mabalozi kwa hofu hawangeweza kuchukua hatua kiholela na kuingilia mambo ya ndani ya nchi. Kwa ufupi, ujasiri wa nchi za kioga za kikoloni za kafiri unatokana na uoga wa watawala vibaraka katika nchi za Kiislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu