- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Ulemavu wa Marekani huku Ikijila Yenyewe ikiwa Hai Sehemu Nyingi Zaidi
(Imetafsiriwa)
Habari:
Kichwa cha habari cha Fox News mnamo tarehe 22 Mei kilisema kwamba "Utawala wa Trump wasitisha mpango wa visa ya wanafunzi wa Harvard" na makala hayo yalimnukuu Waziri wa Elimu, Kristi Noem, akisema: "Utawala huu unaihisabu Harvard kwa kuendeleza vurugu, chuki dhidi ya Mayahudi, na kuratibiana na Chama cha Kikomunisti cha China kwenye chuo chake ... Ni fursa, sio haki, kwa vyuo vikuu kuchukua wanafunzi wa kigeni na kufaidika na malipo yao ya juu ya masomo ili kusaidia kulipa ruzuku zao za mabilioni ya dolari. Harvard ilikuwa na fursa nyingi za kufanya mambo kwa usahihi. Ilikataa. Wamepoteza cheti chao cha Mpango wa Wanafunzi na Ubadilishanaji wa Wageni (Student and Exchange Visitor Programme) kutokana na kushindwa kwao kuzingatia sheria. Hebu hili na liwe ni onyo kwa vyuo vikuu na taasisi zote za kielimu kote nchini."
Maoni:
Ni onyo la hatari kwani lina maanisha kwamba chuo kikuu chenye hadhi kilichoorodheshwa na Ivy League huenda kisichukue wanafunzi wa kigeni mwaka ujao wa masomo, na hata wale wanafunzi ambao wamechukuliwa hivi sasa watapoteza haki yao ya kubaki Marekani isipokuwa wahamishiwe chuo kikuu chengine kabla ya mwaka mpya wa masomo kuanza! Waziri wa Elimu alisema hoja yake katika barua aliyoiandikia chuo kikuu hicho: “Kutokana na kukataa kwenu kwa ushupavu kutii maombi mengi ya kutoa taarifa muhimu kwa Idara ya Usalama wa Taifa huku mukiendeleza mazingira yasiyo salama ya chuo kikuu ambayo ni chuki kwa wanafunzi wa Kiyahudi, munakuza matamshi ya kuunga mkono Hamas, na kutumia ‘sera za ubaguzi wa rangi za, anuwai, usawa, na ushirikishwaji', mumepoteza fursa hii.”
Harvard aliwasilisha kesi mahakamani ikidai kwamba hatua ya Trump ni kinyume cha katiba na jaji wa shirikisho alizuia marufuku ya visa hadi kesi hiyo iamuliwe, lakini Idara ya Usalama wa Taifa ilijibu: "Uamuzi wa leo unachelewesha haki na unatafuta kuzuia mamlaka ya Rais aliyopewa kikatiba" na kuongeza kuwa utawala wa Trump umejitolea "kuregesha busara kwa mfumo wetu wa visa, na tunatarajia sheria yetu ya juu ya visa, na tunatarajia mahakama ya juu zaidi kutuidhinisha kwa hili. Tunayo sheria, ukweli, na busara kwa upande wetu." Fauka ya hayo, Trump anatafuta kuondoa hadhi ya chuo kikuu ya 'kutolipa ushuru' ambayo ingeongeza shinikizo la kifedha kufuatia kufungia kwake mwezi uliopita wa ufadhili wa serikali wa $2.2 bilioni kwa Harvard.
Akikashifu shambulizi la hivi punde la utawala wa Trump dhidi ya elimu ya juu kwa madhumuni ya kisiasa, Barbara R. Snyder, rais wa Chama cha Vyuo Vikuu vya Marekani, alisema, "Uamuzi huu ambao haujawahi kushuhudiwa ni usumbufu wa kikatili na usio na msingi kwa maisha na elimu ya wanafunzi wenye vipaji ambao nishati na ubunifu wao hunufaisha nchi yetu kwa kiasi kikubwa ... Hatimaye ni mustakabali wa nchi yetu – uongozi wake katika sayansi na uvumbuzi na ufanisi wake – ambao unahatishiwa kwa kosa lisilolazimishwa."
Mashambulizi haya ya utawala wa Trump dhidi ya Harvard ni sehemu ya kampeni pana dhidi ya vyuo vikuu ili kuwanyang'anya uhuru wao wa muda mrefu kutoka kwa udhibiti wa kisiasa. Mashambulizi ya Trump juu yao hayajawahi kutokea tangu McCarthyite kuwaondoa washukiwa wa kikomunisti katika miaka ya 1950. Hata hivyo, tishio la wakati huo lilikuwa dola kuu yenye nguvu, Muungano wa Kisovieti, ambayo ilikuwa ni mshindani rika wa kweli wa Marekani na ambayo mfumo wake ulikuwa ukikabiliana na mfumo wa ubepari duniani kote! Kwa hivyo, ni tishio gani kubwa jipya linalosababisha Trump kuwa mkali sana? Ni kama alivyosema Waziri wake wa Elimu: "Utawala huu unaihisabu Harvard kwa kuendeleza vurugu, chuki dhidi ya Mayahudi, na kuratibiana na Chama cha Kikomunisti cha China kwenye chuo chake." Je, kuna uhalali wowote wa madai haya?
Kwa hakika lobi za Mazayuni (Mayahudi pamoja na Wakristo muhimu zaidi wa kiinjilisti) na msaada mkubwa wa kifedha wa Miriam Adelson kwa Trump umemtia motisha kukabiliana moja kwa moja na maandamano ya kupinga mauaji ya halaiki huko Gaza ambayo yanafanyika kwenye vyuo vikuu vya Marekani, lakini vipi kuhusu China? Ufadhili wa kigeni kwa vyuo vikuu vya Marekani kwa muda mrefu umeibua shaka, na juhudi za China kupata ushawishi wa kisiasa kupitia mafungamano yake ya kifedha na taasisi za Marekani zimeripotiwa mara kwa mara katika muongo mmoja uliopita. Profesa wa zamani wa Harvard Charles Lieber alipatikana na hatia mnamo 2021 kwa kusema uongo juu ya mafungamano yake kwa China. Mnamo 2023, Taasisi ya Hudson ilichapisha ripoti iliyopewa kichwa: "Kampeni ya Chama cha Kikomunisti cha China kwenye Mabewa ya Vyuo Vikuu."
Bila kujali nukta hizi za mzozo, kampeni dhidi ya Harvard na pia vyuo vikuu vyengine vingi kwa kweli ni sehemu tu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoila Amerika wakati huu Trump anapotafuta kuangamizi ushawishi wa dola ya kina (deep state) wa upinzani wa kisiasa kwa mpango wake wa 'kuifanya Amerika kuwa tukufu tena' popote unapotokea. Kwa hivyo mashambulizi yake dhidi ya mashirika ya serikali ya shirikisho na ufadhili wao yakiongozwa na Idara ya Ufanisi wa Serikali aliyoianzisha mnamo Januari huku Elon Musk akiwa mkuu wake. Mgogoro huu wa madaraka ndani ya idara za serikali, mabaraza ndani Bunge la Congress na mahakama katika ngazi ya serikali na majimbo sasa unazidi kupanuka na kujumuisha elimu ya juu na nani anaweza kusema mgogoro huo utaishia wapi na matokeo yake ni nini.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin