Jumanne, 18 Safar 1447 | 2025/08/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uzbekistan Yaanzisha Mashtaka ya Jinai kwa Kufundisha Uislamu kwa Watoto

(Imetafsiriwa)

Habari:

Bunge la Seneti la Uzbekistan limeidhinisha sheria inayotoa adhabu ya uhalifu kwa kufundisha watoto dini bila kibali na elimu ifaayo. Vitendo kama hivyo sasa vinaweza kuadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka mitatu gerezani.

Bunge la Seneti la Oliy Majlis la Uzbekistan, katika kikao cha Juni 25, liliidhinisha sheria inayoimarisha mashtaka ya elimu haramu ya kidini kwa watoto. Hati hiyo imetumwa kwa Rais kwa ajili ya uhakiki.

Mwenyekiti wa Kamati ya Seneti ya Sayansi, Elimu na Afya, Bahrom Abdullayev, alisema kuwa nchi hiyo inafanya kazi ya kimpangilio ili kuhakikisha ulinzi wa kuaminika wa haki na maslahi halali ya watoto, na kuunda mazingira ya maendeleo yao kamili. “Umuhimu maalum unatolewa kwa malezi ya watoto wa ufahamu wa kisheria na tamaduni, pamoja na kuunda hali zote za kupata elimu bora, ambayo inachangia ukuaji wao wa kimwili, kiakili, kiroho na kimaadili”, alisisitiza.

Kulingana na Abdullayev, wakati huo huo, katika miaka ya hivi karibuni jamhuri imeona ongezeko la kesi za elimu haramu ya kidini ya watoto wadogo, na katika suala hili, marekebisho yanafanywa kwa Kifungu cha 229-2 cha Kanuni ya Jinai (ukiukaji wa utaratibu wa kufundisha itikadi za kidini).

Maoni:

Ni vyema kutambua kwamba, tofauti na kifungu cha awali ambapo kitendo kama hicho kiliadhibiwa kwa faini ya kiidara au kukamatwa kwa hadi siku 15, hivi sasa mara moja ni suala la mashtaka ya jinai ikiwa mada ya elimu ni mtoto mdogo.

Kupitishwa kwa sheria hii kunaendeleza mwenendo wa Mirziyoyev wa kuimarisha udhibiti juu ya mwamko wa Kiislamu, na, kimsingi, kuiregesha nchi kwenye matendo ya zama za rais aliyejulikana sana Islam Karimov.

Kama inavyojulikana, SGB (zamani SNB) tayari hufanya uvamizi mara kwa mara kwenye kile kinachoitwa "hujras" - madrasa za kibinafsi, za siri ambazo zilionekana nchini Uzbekistan zama za Usovieti.

Ikumbukwe kwamba sheria kama hiyo ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1998. Sheria “Kuhusu Uhuru wa Dhamiri na Mashirika ya Kidini” iliweka vizuizi vikali juu ya shughuli za kidini. Hasa, kufundisha dini kuliruhusiwa tu katika taasisi za elimu za kidini zilizosajiliwa rasmi na tu baada ya kupokea elimu maalum. Kifungu cha 229-2 cha Kanuni ya Jinai ya Uzbekistan kilianzishwa mwaka huo huo; kilianzisha mashtaka ya jinai kwa “kufundisha dini kinyume na utaratibu uliowekwa na sheria”.

Marufuku hii na kifungu cha jinai mara nyingi ilitumika katika miaka ya 2000 na mwanzoni mwa 2010, ambayo ilisababisha ukosoaji kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu, kwani ilipunguza usambazaji wa maarifa ya kidini hata ndani ya familia – yaani, watu walifunguliwa mashtaka hata kwa kufundisha Uislamu kwa watoto wao wenyewe.

Mirziyoyev alipoingia madarakani, matendo hayo yalisimamishwa kwa muda, lakini sasa yameregeshwa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu