Alhamisi, 05 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kuhuisha Uislamu: Njia Pekee ya Kuepuka Majanga

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo Jumatano, Karachi ilifurika kufuatia mvua kubwa iliyonyesha, ikilemaza jiji hilo la bandari lililo eneo la kusini lenye watu 20 milioni chini ya wiki moja baada ya mafuriko mabaya kusomba vijiji katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa. (Al Jazeera.com)

Maoni:

Mafuriko ya hivi majuzi nchini Pakistan yameharibu Khyber Pakhtunkhwa na Sindh, huku maeneo mengine yakipambana na barabara zilizojaa maji ambayo yamegeuza maisha ya kila siku kuwa hatari. Masaibu ya kupoteza maisha na riziki katika KPK yamewaacha watu na hofu. Kinachosumbua zaidi ni kukosekana kwa vifaa sahihi vya uokoaji – na kufanya wengi kuhoji uwezo wa serikali kujibu. Wafanyikazi wa uokoaji wanaachwa wakifanya kila kitu kwa mikono, na kwa mara nyingine tena, ni watu wa eneo hilo ambao, waliopata ukakamavu kwa miaka ya kupuuzwa, wanajua lazima wajitegemee wenyewe kwa sababu ima utakuja msaada mdogo hautakuja kabisa.

Mara nyingi maafa haya yanatambulishwa na Serikali kuwa ya kimaumbile na yasiyoweza kuepukika, ingawa uharibifu mwingi unatokana na ulafi wa binadamu wa madaraka na unyonyaji wa maliasili. Tariq Ali Shah, mtaalam wa misitu ambaye anafanya kazi kwa karibu na serikali ya KP, alisema mkoa huo umekuwa ukipoteza misitu kwa kiwango cha takriban pc 1.5 kila mwaka, ambayo ni sawa na hekta 8000 kwa mwaka, karibu na ukubwa wa eneo la jiji la Islamabad, kati ya 2000 na 2023. Suala jengine ni ujenzi wa hoteli na mikahawa kwenye kingo za mto. Katika mafuriko ya 2022 katika eneo la Swat, karibu hoteli 700, moteli, nyumba za kulala wageni na mikahawa zilifurika kabisa. Katika mafuriko ya hivi majuzi tuliona athari mbaya hata jijini Islamabad, uvamizi wa ardhi na kujenga kwenye vikwazo vilivyoundwa na nullah, ambapo ililazimisha maji ya mafuriko kuingia katika nyumba za chini. Mafuriko ya Karachi ni ushahidi wa kufeli kwa mfumo wa maji taka na mitaro ya maji, kwani mitaro ya maji ya mvua ya asili ya jiji (nullahs) imesaki kwa taka ngumu, na mfumo jumla hauwezi kushughulikia ujazo wa maji, haswa kwa mitindo ya mvua isiyo tabirika. Hii inachangiwa na utawala duni, kusambaratika kwa utawala, na ukosefu wa jumla wa miundombinu ya maji ya kudhibiti maji machafu ya jiji na maji ya mvua.

Mipango pofu ya maendeleo nchini Pakistan inaweza kufuatiliwa hadi kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza. Waingereza, waliolenga kudhibiti nafasi na kuongeza faida, walianzisha mkusanyiko wa mamlaka ovyo za mipango miji na sera zisizo na usawa za makaazi. Walitanguliza ukuzaji wa utepe, mtawanyiko wa miji, na utengano wa matabaka ya watu. Baada ya uhuru, falsafa yetu ya upangaji haikubadilika - jenga nje, jenga kubwa, na jenga kwa ajili ya matajiri. Mipango mikuu ilirasimiwa na kupuuzwa. Ardhi ya kilimo ililiwa na jumuiya za nyumba zinazoendelea kupanuka.

Huku ulimwengu wa kibepari ukistawi kwa majanga, Uislamu una mtazamo tofauti kabisa. Katika Uislamu Serikali ina wajibu wa kutunga sera za kulinda misitu ya asili, kudhibiti shughuli za uchimbaji madini na ukataji miti pamoja na shughuli nyengine zinazohitajika ili kuepuka uharibifu wa misitu ya miti. Mwenyezi Mungu (swt) aliumba dunia na vilivyomo ndani yake kwa ajili ya mwanadamu na inaweza tu kulindwa kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu (swt). Chini ya enzi ya dhahabu ya Uislamu, wahandisi na wapangaji wa miji walitengeneza teknolojia za hali ya juu za maji ili kulinda maeneo ya mijini kutokana na mafuriko na kuhakikisha usambazaji wa maji thabiti. Udhibiti wa mafuriko ulihusisha kujenga mabwawa na njia kuu, kujenga mifumo ya mitaro na kutengeneza mashini za kuinua maji kwa ajili ya usambazaji na kuhifadhi maji kwa ufanisi. Jitihada hizi, pamoja na mbinu za utengenezaji mifereji na ulinzi wa matuta kwa kutumia mierebi, zilianzisha mifumo mipana ya usimamizi wa maji ambayo ilisaidia kilimo, usambazaji wa maji mijini, na ustawi wa umma, yote hayo yakiwa uthibitisho wa ufahamu wao wa hali ya juu wa uhandisi wa maji.

Hili liliwezekana kwa sababu ya muunganisho wa maeneo hayo kuwa chini ya utawala mmoja licha ya kuwa mbali sana. Mafuriko, ukame, magonjwa au vita, changamoto yoyote ilihisiwa na kutunzwa na kiini cha Ummah, yaani, nguvu kuu ya Khilafah. Sisi tunahitaji sana Khilafah kuokoa, na kuhuisha utukufu wa zamani ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameandika kwa ajili ya watu wake. Khilafah, itakaposimamishwa kwa njia ya Utume, haitaruhusu ulafi wa wenye njaa ya madaraka kuharibu mali ya Ummah. Maji yanayosababisha kifo na uharibifu sasa, yatakuwa chanzo cha uzima na ukuaji. Mabwawa na mifereji itajengwa na maji yatasambazwa kwa maeneo yanayohitaji. Tunayo mifano kama ‘Mfereji wa Zubaida’, mfereji ambao ulijengwa kwa ajili ya watu wa Makka na mke wa aliyekuwa kaimu Khalifa Haroon ur Rasheed kwa ajili ya kuwafariji mahujaji. Mfereji huo bado upo, unatukumbusha zama za dhahabu za Uislamu na unatuita tufuate njia ya wafuasi wa Mtume Mtukufu Muhammad (saw).

[وَلِلَّهِ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ]

“Na Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.” [Surah Aali-Imran (3:189)]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu