Jumamosi, 19 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Swala Zimesimamishwa jijini Dushanbe kwa sababu ya Ziara ya Putin

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kuanzia Oktoba 7 hadi 12, misikiti kadhaa jijini Dushanbe itasimamisha kwa muda swala za jamaa. Kulingana na Idara ya Mambo ya Ndani ya jiji hilo, vikwazo hivyo vinatekelezwa “kuhusiana na matukio muhimu yanayotokea katika jiji hilo,” akimaanisha ziara rasmi ya Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Swala za jamaa hazitafanyika kwa muda katika misikiti ya Mavlono Yaqub Charkhi, Sari Osiyo, Abu Hanifa, na Khoji Ismatullo. Aidha, kuanzia tarehe 8 hadi 12 Oktoba, swala pia hazitafanyika katika msikiti wa Imam al-Bukhari.

Hasa, mnamo Oktoba 7, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Andrei Belousov aliwasili Dushanbe kutembelea vituo vya kijeshi vya Wizara ya Ulinzi ya Urusi vilivyoko Tajikistan. Katika Uwanja wa Ndege wa Dushanbe, Belousov alilakiwa na Waziri wa Ulinzi wa Tajikistan Emomali Sobirzoda na Mkuu wa Majeshi Bobojon Saidzoda, kwa mujibu wa taarifa hiyo.

Maoni:

Ni muhimu kukumbuka kuwa, kwa mujibu wa data rasmi, kambi ya jeshi ya 201 iliyoko Tajikistan ni kituo kikubwa zaidi cha kijeshi cha Urusi nje ya mipaka yake. Iko katika miji miwili - Dushanbe na Bokhtar. Kambi hiyo iko na magari yenye bunduki, vifaru, silaha, upelelezi, ulinzi wa anga, kemikali, kibayolojia, ulinzi wa radiolojia na vitengo vya mawasiliano. Kwa jumla, kikosi cha jeshi la Urusi nchini Tajikistan kina takriban wanajeshi 10,000, ambapo jeshi lote la taifa la Tajikistan linajumuisha wanajeshi 9,000 pekee.

Kwa kuzingatia haya yote, ziara ya Putin inaonekana kidogo kama ziara ya kidiplomasia ya kiongozi wa kigeni na zaidi kama ukaguzi wa bwana wa Kirusi wa koloni yake ya Asia ya Kati. Rahmon hajaribu hata kuficha utumwa wake kwa Warusi - haishangazi, kwani Moscow ndiyo inayodhamini usalama wa serikali yake.

Ni muhimu kutaja pia kwamba kusimamishwa kwa swala za jamaa misikitini wakati wa matukio kama hayo tayari imekuwa kawaida chini ya utawala wa Rahmon. Kwa mfano, mnamo Julai 2024, swala za Ijumaa jijini Dushanbe ilifutiliwa mbali kwa sababu ya ziara ya serikali ya kiongozi wa China Xi Jinping. Ni dhahiri, Rahmon anatafuta kuiwasilisha Tajikistan kwa mabwana wake wa kigeni kama iliyosafishwa na Uislamu - kwa maana nyengine, kama jinsi tu wanavyotaka kuiona.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu