- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mafunzo Kutokana Na Jinsi Nchi Kubwa Zaidi ya Kidemokrasia Duniani Inavyowafelisha Wanawake wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)
Habari:
Gazeti la ‘The Indian Express’ limechapisha makala yenye kichwa “Pindi kutokuwepo kukizungumza kwa sauti ya juu zaidi kuliko uwepo: Wanawake wa Kiislamu na Bunge la India”. Yanazungumzia ukosefu mkubwa wa uwakilishi wa wanawake wa Kiislamu katika afisi yake. Tangu Lok Sabha ya kwanza (Bunge la Kidemokrasia la India) mnamo 1952, ni wanawake kumi na nane pekee Waislamu ambao wamekuwa wachangamfu ndani bunge. Uwakilishi mdogo umerekodiwa katika kitabu kipya kilichoandikwa na waandishi wa habari Rasheed Kidwai na mwanasayansi wa siasa Ambar Kumar Ghosh chenye kichwa “Kukosekana Bungeni: Wanawake wa Kiislamu katika Lok Sabha”, kilichochapishwa na Juggernaut (2025). Waandishi hawajali katika utambuzi wao wa jinsi uwakilishi kama huo ulivyokuwa mara nyingi. Kwa vyama vingi vya kisiasa, ugombezi wa mwanamke wa Kiislamu ulifanya kazi kama ishara tu badala ya athari na ushawishi halisi.
Mojawapo ya hadithi muhimu zaidi ambazo kitabu kinadhihaki ni uhusiano usio na utulivu kati ya mwonekano na nguvu. Mbunge mmmoja mwanamke wa Kiislamu anaweza kuvutia angazo la vyombo vya habari. Lakini linapokuja suala la kufanya maamuzi halisi, uteuzi wa wagombea, vipaumbele vya sera, na nyadhifa za baraza la mawaziri, wanawake wa Kiislamu mara nyingi wanawekwa kando. Waandishi hao wanaweka wazi kwamba “uwakilishi wa Kidemokrasia” hautafsiri moja kwa moja uwezeshaji.
Maoni:
Hatupaswi kushangaa kama wanawake wa Kiislamu kushuhudia mwisho wa enzi ambapo majaribio ya nadharia ya kisiasa ya Kiliberali yanahitaji uthibitisho wa sumu yake. Tiba iliyopotea kwa muda mrefu ya uwezeshaji haiwezi kupatikana tena katika pengo jeusi la Demokrasia. Tumeuona udanganyifu wa “Ujumuishi” kwa namna yake yote, mawimbi ya ahadi za uongo na maneno potofu ya Kiislamu. Kuingia “mamlakani” daima kunamaanisha kuwatumikia mabwana zenu wa kisekula na kulegeza msimamo uhusiano wenu na Mwenyezi Mungu (swt).
Watetezi wa haki za wanawake wako kimya katika mashambulizi ya kimataifa na ya kitaifa na mauaji ya wanawake wa Kiislamu ambao wanaishi kwa hofu ya kudhihirisha kitambulisho chao na utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt).
Sisi kama wanawake wa Kiislamu hatupaswi kamwe kusahau kwamba tuna tamkini halisi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee na kwamba sauti zetu, usalama na utu wetu vililindwa daima chini ya Khilafah. Kamwe hatukuwahi kuhitaji harakati za haki za wanawake, na tulikuwa tukiwalinda wanawake wasio Waislamu kwa maadili yetu matukufu. Haki za kiuchumi pamoja na za kijamii ni takatifu na ziko wazi katika Quran 4:12;
[وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلاَلَةً أَو امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ فَإِن كَانُوَاْ أَكْثَرَ مِن ذَلِكَ فَهُمْ شُرَكَاء فِي الثُّلُثِ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَى بِهَآ أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَآرٍّ وَصِيَّةً مِّنَ اللّهِ وَاللّهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ]
“Na fungu lenu ni nusu walicho acha wake zenu ikiwa hawana mtoto. Wakiwa na mtoto basi fungu lenu ni robo ya walicho acha, baada ya wasia waliyo usia au kulipa deni. Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anaye rithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye ndugu mume au ndugu mke, basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi. Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi, baada ya wasia ulio usiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole.”
Iwapo tutazingatia pekee katika kurudisha mamlaka sahihi ya Uislamu kwenye maisha ya kisiasa, hatutachanganyikiwa tena katika vikengeushi vya ajenda ya kisekula ambayo inalenga tu kuwafanya wanawake wa kweli wa Kiislamu wasionekane na wasio na uwezo.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir