- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Utawala wa Uovu na Ghasia Utadumu kwa Muda Apendao Mwenyezi Mungu Uwepo!
(Imetafsiriwa)
Habari:
Uchaguzi wa mapema wa bunge ulifanyika Kyrgyzstan. Mnamo 13 Disemba, IA 24.kg iliripoti: “Tume Kuu ya Uchaguzi na Kura za Maoni imefupisha matokeo ya uchaguzi wa ajabu wa wabunge wa Zhogorku Kenesh wa Jamhuri ya Kyrgyz, ambao ulifanyika mnamo 30 Novemba 2025.
Uchaguzi wa mapema wa bunge ulipangwa kwa amri ya rais mnamo 30 Septemba 2025. Kulingana na Tume Kuu ya Uchaguzi, kampeni ya uchaguzi na mchakato wa kupiga kura wenyewe ulifanywa kwa mujibu wa mahitaji ya sheria”.
Maoni:
Muhula wa bunge ulitarajiwa kuisha Novemba 2026, lakini rais alivunja bunge baada ya wabunge wanaounga mkono rais kuanzisha uchaguzi wa mapema wa bunge mnamo 25 Septemba. Uchaguzi ulifanyika dhidi ya mazingira ya kuzuiliwa kwa watu mashuhuri wa upinzani. Mnamo 24 Novemba wanachama wa chama cha upinzani cha Social Democratic Party Temirlan Sultanbekov na Ermek Ermatov, mwana wa rais wa zamani Kadyrbek Atambayev, na wengine walikamatwa. Zhaparov alifanya ujanja kama huo ili kuwaondoa wabunge wasiohitajika bungeni mnamo 2021.
Kulingana na matokeo ya uchaguzi, jamaa wa Rais S. Zhaparov na Mkuu wa Huduma Maalum K. Tashiev walipata kura nyingi zaidi. Mapema, mnamo Oktoba, mtoto wa mwisho wa rais, Nurdoolut Nurgozhoev, akawa mwanzilishi wa benki mpya. Katika mahojiano na waandishi wa habari, alipoulizwa kuhusu ushiriki wa mwanawe katika ufunguzi wa benki mpya, Rais Zhaparov alijibu: “Hatuna cha kuwaficha watu. Kwanza kabisa, nimekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka mitano. Wakati huu, sijawahusisha wanafamilia wangu wowote, hata kaka zangu, katika masuala ya serikali. Ninaamini kwamba mwanasiasa mmoja kwa kila familia anatosha...”
S. Zhaparov anajiandaa kwa uchaguzi ujao wa 2027, na kwa lengo hili, kwa upande mmoja, anasafisha uwanja wa kisiasa wa watu wote wa upinzani wasiohitajika. Kwa upande mwengine, kwa kumpandisha cheo mwanawe katika miundo ya kifedha, anajipatia uungwaji mkono wa kudhibiti nchi kutoka kwa mtazamo wa kiuchumi. Vikosi vya usalama vinadhibitiwa na rafiki na mshirika wa Zhaparov, Kamchybek Tashiev, mkuu wa Kamati ya Serikali ya Usalama wa Kitaifa.
Mwanzoni mwa Novemba, S. Zhaparov alisema kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii: “Hakutakuwa na mapinduzi. Kwanza, hatutatoa sababu yoyote ya mapinduzi. Pili, dola dhaifu ya zamani haipo tena. Dola hivi sasa ina nguvu. Tatu, watu tayari wanajua vizuri ni nani wa kumuunga mkono na ni nani anapaswa kuwa madarakani. Kuanzia sasa, mutaona mapinduzi tu katika ndoto zenu. Uporaji, wizi, ulafi wa kutafuta faida na majaribio, kama hapo awali, ya kunyakua nyadhifa na kupata utajiri baada ya mapinduzi - acheni haya yote yabaki katika ndoto zenu tu.” Matendo na kauli hizi za rais zinamaanisha kwamba S. Zhaparov anakusudia kubaki madarakani kwa muda mrefu.
Kila mtu anayeingia madarakani katika jamhuri za Asia ya Kati anajitahidi kuweka mizizi mirefu na kushikilia madaraka hadi kifo chake, na kisha kuwaachia watoto wake mamlaka haya kama urithi. Rais wa Turkmenistan amehamisha madaraka kwa mwanawe. Rais wa Tajikistan ameweka mizizi mirefu kiasi kwamba jamaa zake wanashikilia nyadhifa katika karibu miundo yote ya madaraka, na amemtayarisha mwanawe kuchukua nafasi yake. Hali ni sawia na Rais wa zamani wa Kazakhstan Nazarbayev. Nyanja zote za kifedha nchini Kazakhstan zinadhibitiwa na watoto na jamaa wa Nazarbayev.
Rais wa Uzbekistan, Shavkat Mirziyoyev, alimteua binti yake kuwa mkuu wa utawala wa rais, na Saida Mirziyoyeva kivitendo ni mtu wa pili mwenye nguvu zaidi katika nchi hiyo.
Nchi zinazoitwa huru zenye taasisi za kisheria zimekuwa utaratibu tu rasmi katika ulimwengu wa kisasa. Matamko haya yote makubwa kuhusu jamii za kisheria, utawala wa sheria na haki za binadamu ni kama sarabi tu ambayo haipo katika uhalisia.
Kiuhalisia, tunashuhudia utawala wa uovu na vurugu, kama Mtume wetu mpendwa Muhammad (saw) alivyotwambia. Abu Daud Tayalisi alisimulia kutoka kwa Hudhaifa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:
«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ» “Kisha utakuwepo utawala wa uovu na vurugu, ambao utadumu kwa muda mrefu kama Mwenyezi Mungu apendavyo uwepo...”
Leo, wale walio upande wa haki sio walio na nguvu. Leo, wale walio madarakani, ndio walio na pesa na jeshi, ambao ni wenye nguvu. Madhalimu hawa wanatawala kwa nguvu, wakiwalazimisha watu kujisalimisha kwa dhulma na uovu wao, wakijitajirisha kwa gharama ya rasilimali za watu, na kuwafunga wale wanaolingania Uislamu na uongofu. Watu wamechoka na udikteta wa watawala wao, na hakuna mtu wa kusimama na watu, kuwatetea na kuwaokoa kutokana na mateso yao.
Lakini hili halitadumu milele. Utawala wa madhalimu utafikia mwisho hivi karibuni. Kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) aliendelea na hadith na akatwambia kuwa:
«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»
“...Kisha utakuwapo utawala wa kutenza nguvu ambao utadumu kwa muda apendao Mwenyezi Mungu kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume,” na kisha akanyamaza.”
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir



