Jumatatu, 17 Muharram 1444 | 2022/08/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 ‘Virusi vya Kigeni’

Habari:

CNN ililalamika kuhusu Trump mnamo 13 Machi kwa kichwa: “Kwa nini ni MUHIMU ZAIDI kwamba Trump hajapimwa virusi vya corona” licha ya kuwa na mahusiano na mtu aliyeambukizwa wiki iliyopita. Alipoulizwa lau atapimwa, jibu lake lilikuwa: “Tuseme hivi, mimi sina wasiwasi, SAWA?” na pia akasema: “Sio kama ni jambo kubwa, nitafanya tu, sihisi sababu yoyote – Najihisi vizuri sana.” Akaulizwa tena mnamo Ijumaa na jibu lake lilikuwa: “Hatuna dalili zozote.”

CNN ilielezea wasiwasi wake kwamba kiongozi wa Amerika anakuwa hajali na kuyahatarisha maisha ya Waamerika kutokana na mtazamo wake.

Maoni:

Kususuwaa kwa Trump kunatufundisha namna taifa lenye nguvu na linaloongoza linaweza kuendelea kujipiga kwa muda, ilhali polepole linaisha kindani. Viongozi wengi wa kisiasa walilikadiria kiuchache tishio la Covid 19, lakini hakuna hata mmoja amedumu katika hilo kama Trump kwani amefeli kutambua athari ya virusi hivyo kwa nchi yake. Hatimaye Trump ‘alipohutubia taifa’ hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba masoko ya hisa yalikuwa yameporomoka kutokana na mkanganyiko na sintofahamu katika hotuba yake. Hata ilionekana kama ambaye anadhania kuwa virusi hivi ni njama ya mtu kumfanya aonekane mbaya. Kwa wiki kadhaa, alilalamika kuhusu wanasiasa wapinzani walioko nchini kwa kutumia “virusi kama silaha” dhidi yake, na hotuba yake ilikuwa na marudio kama “virusi kutoka Uchina” na “virusi vya kigeni” kama ambaye kuthibitisha chuki na hofu yake kwa wageni na mapenzi yake kwa kuta. Sasa amepiga marufuku ndege kutoka Ulaya, licha ya hata Amerika kukumbwa na virusi na kutokuwa na vifaa vya kupimia vya kutosha ili kujua hali ni mbaya kwa kiasi gani haswa.

Licha ya Amerika kuwa ni taifa la kimfumo, watu wanaotawaliwa kwa sheria na katiba, zinazotekelezwa na taasisi zilizojengwa kwa msingi wa “ufuatilizi na uhakiki,” kila kukicha inaonekana kama jamhuri mpya ya fujo. Hata viongozi wa dola dhaifu na vibaraka wanaonekana kuwa wanaume wa dola zaidi kuliko kamanda mkuu wa Amerika. Lazima kwao ni uzito kutomcheka mjinga hadharani, ambaye anaweza kubofya funguo na kuwasambaratisha wote lau wasaidizi na washauri wake hawatomtizama kwa makini zaidi.

Je wendawazimu hawajaanza kusimamia hifadhi? La, bado. Watu wanaiendesha na wote hawawezi kuwa ni wendawazimu, au inawezekana? Walimpigia kura Trump, na kisha wengi wa wabunge ndani ya Seneti, ambao watu waliwapigia kura, waliamua kumuondoshea mashtaka yote Trump baada ya jaribio la kijinga la kutaka kumng’atua madarakani. Kwa hiyo, la, wendawazimu hawajaanza kusimamia; bali watu bado ndio wanaosimamia. Lakini vipi kuhusu upinzani – wanaweza kuwateka watu ili kupigia kura kwa kitu kizuri zaidi? Mshindani anayeongoza ndani ya chaguzi ndogo za kidemokrasia ndiye anayefanana zaidi na Trump, na labda mwanamume kama Jo Biden, anayeweza kuapa na kuwalaani watu anaweza kufaulu katika kazi ya kumng’atua Trump. Viongozi wabaya wanakuja na kuondoka, lakini chaguzi na taasisi ni dhaifu katika kuleta kheri kubwa.

Miaka tisini na tisa imepita tangu kufutwa kwa Khilafah kutoka ndani ya katiba ya Uturuki, lakini itikadi ambayo dola ilibuniwa bado iko hai ndani ya mioyo na akili za Waislamu. Lakini, dunia inataabika katika kiza kwa kukosekana kwake.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu