Jumatano, 04 Jumada al-awwal 1443 | 2021/12/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 14/08/2021

Taliban Yaichukua Afghanistan na Kuifanya Sasa Kushikilia Zaidi ya Nusu ya Miji Mikuu ya Mikoa

Kwa mujibu wa na ripoti ya shirika la habari la Associated Press mnamo Ijumaa, katika mapigano ya kasi isiyo dhibitika kwenye ngome yao ya kusini mujahidina wa Afghanistan waliichukua miji mikuu mingine minne ya mikoa ikiwapa udhibiti wa nusu ya miji mikuu ya mikoa ya Afghanistan na theluthi mbili za nchi hiyo, ikiwemo pia masaa 24 yaliyopita kukamatwa kwa Herat upande wa Magharibi na Kandahar upande wa Kusini ambayo ni mji wa pili na wa tatu kwa ukubwa nchini humo. Serikali ya vibaraka ya Kabul iliyopandikizwa na Amerika sasa inashikilia mikoa michache tu eneo la katikati na mashariki, na pia jiji la Mazar-i-Sharif upande wa kaskazini. Ripoti hiyo inasema kwamba ingawa mji wa Kabul bado hauko chini ya tishio la moja kwa moja, vikosi vya serikali ya Kabul vilikuwa vikipambana katika mkoa wa Logar umbali wa kilomita 80 tu kutoka mji mkuu na jeshi la Amerika linakadiria kuwa Kabul yenyewe inaweza kuwa chini ya shinikizo ndani ya mwezi mmoja, ikiwawezesha mujahidina hatimaye kuimarisha haraka udhibiti wao juu ya nchi nzima.

Licha ya jaribio la vyombo vya habari vya Magharibi kuwaonyesha mujahidina kama wasiopendwa, kasi ya maendeleo yao kote nchini haingewezekana bila ya uungwaji mkono mkubwa ulimwenguni. Thaqafa na nidhamu za Kimagharibi ziliweza tu kusonga mbele sana katika miji michache mikubwa; sehemu kubwa ya nchi hiyo iliendelea kushikamana na maagizo ya Kisheria muda mrefu baada ya kuanguka kwa utawala wa Kiislamu, ikiwa ni kawaida kwao kupata wanachuoni wa Kiislamu kuamua mizozo yao badala ya kujiwasilisha mbele ya majaji wa serikali wanaotekeleza sheria ya Kimagharibi. Fauka ya hayo, sio Afghanistan tu ambayo majeshi ya Magharibi yameshindwa kuishikilia. Hawakuweza pia kuishikilia Iraq, ambayo waliivamia mara tu baada ya Afghanistan; na kwa hivyo Amerika ililazimika kusoma upya mafunzo ya karne ya ishirini ya wajenzi wa himaya za Ulaya, ambao hatimaye ilibidi waondoe majeshi yao yote kutoka katika nchi za Waislamu.

Waislamu wanakabiliwa na udhaifu tu katika maono na kujiamini. Matabaka ya ya waliyoelimishwa Magharibi kati ya Waislamu yamepima nguvu ya Magharibi, huku yakidharau nguvu ya Umma wa Kiislamu na Sharia ya Kiislamu. Watawala wao wametongozwa kufikiria kwamba maendeleo katika ulimwengu huu yanahitaji kufuata Magharibi, kuwategemea wao na kutafuta msaada wao na mwongozo katika mambo yote, ingawa kukaribisha uingiliaji katika wa Magharibi katika maswala ya Waislamu sio chochote ila ni kujiua kisiasa. Mpaka sasa, uongozi wa Taliban uko chini ya shinikizo kubwa la kimataifa kukubali suluhu iliyowekwa na Amerika nchini Afghanistan ambayo itamaanisha aina fulani ya kugawanya mamlaka na serikali iliyopo ya Kabul na mambo mengi muhimu ndani yake na kuiunga mkono. Wizara ya Mambo ya Nje wa Amerika ilielezea madhumuni ya ziara ya mjumbe wa Amerika Zalmay Khalilzad nchini Qatar wiki hii kuwa ni "kuishinikiza Taliban kuacha mashambulizi yao ya kijeshi na kujadili suluhu ya kisiasa". Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitishia, "Huu ni wakati wa kusitisha mashambulizi. Huu ndio wakati wa kuanza mazungumzo mazito. Huu ni wakati wa kuepuka vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu, au kutengwa kwa Afghanistan”. Kwa kuulazimisha uongozi wa Taliban kuwakubali watu wa kutoka nje, Amerika inatarajia kuwa na uwezo wa kuendelea kudumisha ushawishi juu ya maswala ya Afghanistan, ili yote isipotezwe kwao. Lakini ikiwa Magharibi haikuweza kuishinda Taliban katika vita, basi kwa nini masharti yao yakubaliwe kwa amani?

Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Ummah wa Kiislamu hivi karibuni utapata ufahamu wa kweli na utasimama na kutengua ushawishi wa dola za kigeni za kikafiri, kusimamisha tena Dola ya Kiislamu ya Khilafah kwa njia ya Mtume (saw), ambayo itayakomboa maeneo yote yaliyokaliwa, kuziunganisha ardhi zote za Waislamu, kutabikisha Sharia ya Kiislamu, kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kubeba nuru ya Uislamu ulimwengu mzima.

Tunisia, Lebanon

Amerika inaendelea kutafuta njia ya kuimarisha ushiriki wake nchini Tunisia, baada ya ushindi wake mkubwa nchini Libya, ikitumia fursa ya mzozo unaozidi kutokota nchini Tunisia kati ya Uingereza na Ufaransa. Mwishoni mwa Julai, Rais wa Tunisia Kais Saied alimfuta kazi waziri wake mkuu na kusimamisha bunge, kwa kuungwa mkono na vikosi vya jeshi. Kama koloni ya zamani ya Ufaransa, jeshi la Tunisia linaendelea kuwa na uhusiano wa kina na Ufaransa, huku wanasiasa wengi wa Tunisia wakiunganishwa na Uingereza kwa sababu ya miaka mingi ya utawala wa kibaraka wa Uingereza Habib Bourguiba na kisha Zain el Abidine Ben Ali. Amerika inajaribu kujiingiza kwenye mzozo huu wa kijeshi wa Ufaransa na Uingereza kwa kuonyesha kumuunga mkono Kais Saied. Mnamo siku ya Ijumaa, naibu mshauri wa usalama wa kitaifa wa Amerika Jonathan Finer alikutana na Kais Saied na kutoa ujumbe kutoka kwa Rais wa Amerika Joe Biden "akithibitisha msaada wake wa kibinafsi, na ule wa Utawala wa Biden-Harris, kwa watu wa Tunisia na kuwataka kurudi haraka kwenye njia ya demokrasia ya bunge la Tunisia”. Ardhi za Waislamu zitaendelea kuwa uwanja wa unyonyaji na ushindani kati ya dola za kigeni hadi Ummah wa Kiislamu utakapodhibiti mambo yao kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah ambayo, tangu kusimamishwa kwake, itaingia katika safu za dola kuu kwa kigezo cha ukubwa wake, idadi ya watu wake wenye nguvu, na rasilimali kubwa nyingi pamoja na eneo lake muhimu la kisiasa ya kijografia na mfumo wake bora kabisa wa Kiislamu.

Katikati ya moja ya mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi kuikumba nchi yoyote mahali popote, Benki Kuu ya Lebanon imeongeza mateso juu ya mateso kwa kutangaza kukomesha ruzuku ya mafuta, katika mpango ambao unakubaliana kikamilifu na mawazo ya soko la Kirasilimali. Mabadiliko yoyote katika bei ya mafuta bila shaka yatakuwa na athari kubwa kwa uchumi mzima. Sharia ya Kiislamu inayaona mafuta kama mali ya umma ambayo inamilikiwa kwa pamoja na watu na chini ya usimamizi wa serikali kwa niaba yao. Dola ya Khilafah pia inaweza kuchagua kuweka bei ya mafuta katika kiwango cha soko lakini kwa hali hiyo faida itakuwa ya Umma wa Kiislamu na sio ya pote la wafanyabiashara wachache wa Kibepari. Watu wa Lebanon ni wenye tija zaidi na wajasiriamali kati ya Umma wote; kabla ya shida zake kuanza, Lebanon ilikuwa injini ya kibiashara iliyoendesha shughuli za kiuchumi kote Mashariki ya Kati. Msiba wa Lebanon uko katika mfumo wake wa unyonyaji wa kiuchumi na mfumo wake mbovu wa kisiasa uliowekwa juu yake na Magharibi. Uchumi wa kirasilimali haufanyi kazi; ikiwa Magharibi huonekana kufanikiwa, sio kwa sababu ya uchumi wao wa ndani bali kwa sababu wanaendelea kupora rasilimali na utajiri wa ulimwengu mzima. Hii ni tofauti na Uislamu ambao haukuwafaidi Waislamu tu bali pia watu wengine wa ulimwengu kupitia sera za Uislamu zilizo wazi na za ukarimu za kimataifa. Waislamu wana akili sana, wana uwezo na bidii, na wanasaidiwa na mfumo thabiti wa kijamii wa kifamilia ambao unawawezesha watu kufikia uwezo wao wa hali ya juu; wanachokosa ni mfumo sahihi wa serikali wa kuzipeleka nguvu zao katika kujinufaisha wenyewe badala ya kuwanufaisha kipote cha Wamagharibi. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Dola ya Khilafah itakayosimamishwa tena itajenga kwa haraka kilimo chake, biashara, viwanda na biashara kupitia utekelezaji wa mfumo wa kiuchumi wa Kiislamu na kwa mara nyingine tena kuzifanya ardhi za Waislamu kuwa kitovu cha ustawi wa kiulimwengu, kama hapo awali ukiwanufaisha sio tu Ummah wa Kiislamu bali wanadamu wote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ﴿

“Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.” [al-Qasas: 77].

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu