Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 22/03/2023

Uingereza Kuipa Ukraine Makombora ya Uranium Iliyopungua Licha ya Maonyo ya Urusi

Afisa mmoja wa Uingereza amethibitisha kuwa Uingereza itaipatia Ukraine makombora yenye uranium iliyopungua ambayo yatatumika pamoja na vifaru vya Challenger 2 vilivyotengenezwa Uingereza licha ya maonyo kutoka kwa Urusi kwamba itazingatia matumizi ya silaha hizo zenye sumu sawa na bomu chafu. "Pamoja na utoaji wetu wa kikosi cha vifaru vikuu vya vita aina ya Challenger 2 kwa Ukraine, tutakuwa tukitoa silaha zikiwa ni pamoja na risasi zenye kutoboa ambazo zina uranium iliyopungua. Risasi kama hizo zina ufanisi mkubwa katika kuvishinda vifaru vya kisasa na magari ya kivita," alisema Annabel Goldie, naibu waziri wa ulinzi wa Uingereza, katika jibu la maandishi kwa swali lililowekwa kwenye tovuti ya Bunge la Uingereza. Uranium iliyopungua kwa kawaida huundwa kama bidhaa ya kuzalisha uranium iliyorutubishwa na ni nzito sana. Kwa sababu silaha za uranium iliyopungua zina mionzi, inayohusishwa na saratani na kasoro za kuzaliwa, haswa nchini Iraq, ambapo vikosi vya Marekani vilitumia idadi kubwa ya mabomu yenye utata wakati wa Vita vya Ghuba na uvamizi wa 2003. Ulemavu wa kuzaliwa bado ni jambo la kawaida katika mji wa Fallujah nchini Iraq hadi leo, huenda ni kutokana na upungufu wa madini ya uranium. Akijibu habari hizo, Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergey Shoigu alionya kwamba kupeleka Ukraine silaha za uranium iliyopungua kunauleta ulimwengu karibu na "mgongano wa nyuklia" kati ya Urusi na Magharibi na akaonya Moscow itajibu. "Kwa kawaida, Urusi ina kitu cha kujibu kwacho hili," alisema.

Upunguzaji Mkubwa wa Uzalishaji Uchafu Unaohitajika Ili Kukomesha Janga la Tabianchi

Jopo la Serikali za Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IPCC) lilionya kuwa kuna dirisha linalofungika kwa kasi la kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, likisema ongezeko la joto duniani huenda likazidi nyuzi joto 1.5 katika miaka ya 2030. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa nchi tajiri kujaribu kufikia uzalishaji wa hewa sifuri ya carbon ifikapo karibu 2040. Wanasayansi wa IPCC walisema kuna "njia inayowezekana, lakini nyembamba" ili kuepusha athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabianchi, lakini kufanya hivyo kunahitaji kupunguza gesi chafuzi kwa 43% duniani kote ifikapo 2030 na 60% ifikapo 2035, pamoja na upunguzaji wa juu zaidi wa CO2. Ripoti hiyo inaonya kuwa kutekeleza sera za sasa zinazotangazwa na serikali kutasababisha ongezeko la joto duniani kufikia wastani wa nyuzi joto 3.2. Pamoja na mlipuko wa COVID na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wengi wa watoa wakubwa zaidi ulimwenguni wamerudi kwenye malengo yao ya kupunguza utoaji na wengi wameanzisha tena viwanda vyao vya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe. Watoaji wakubwa zaidi duniani walikuwa tayari wakiburuza miguu yao kwenye malengo ya kupunguza utoaji na kuna uwezekano wataendelea kufanya hivi.

Machafuko nchini Pakistan

Mahakama moja ya Pakistan ilifutilia mbali hati ya kutaka kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan baada ya wafuasi wake kukabiliana na polisi nje ya jengo la mahakama ambapo Khan alionekana kama sehemu ya kesi dhidi yake. Baadaye polisi walimshtaki Khan na viongozi kadhaa wa chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kwa ugaidi. Mapambano ya kisiasa kati ya Khan na serikali yanaweza kusababisha makabiliano makali zaidi kati ya wafuasi wa Khan na polisi katika wiki zijazo. Kwa sababu hali hii tete inakaribia uchaguzi mkuu wa Pakistan utakaofanyika baadaye mwaka wa 2023. Imran Khan anaendelea na kumshambulia jenerali mstaafu wa jeshi, Qamar Bajwa pamoja na dori kubwa inayochezwa na jeshi nchini humo. Utawala wa Pakistan pamoja na Imran Khan wanacheza ili kudumisha nafasi zao na kubaki madarakani. Kwa mujibu wa nchi hii, hili halizingatiwi sana.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu