Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Dua ya Kunut “Kwa ajili ya Gaza... Mikono Imeinuliwa Mbinguni?!”
- Imepeperushwa katika Uturuki
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili ya halaiki ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 17, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa Waislamu zaidi ya 170,000, wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Uturuki iliandaa amali “Dua ya Kunut” kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, 18 Machi 2025, na kuanza tena mauaji yake ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao wakiwa ni wanawake, watoto na wazee, chini ya kichwa: Dua ya Kunut “Kwa ajili ya Gaza... Mikono Imeinuliwa Mbinguni?!”