Alhamisi, 23 Safar 1448 | 2026/08/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Malaysia: Hati ya Pingamizi kuhusu “KL Headline Msimu wa 2026”

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir Malaysia (HTM) uliwasilisha hati ya pingamizi kwa Wizara ya Mawasiliano huko Putrajaya kuhusu kuandaliwa kwa tamasha la “KL Headline Msimu wa 2026”. Hatua hii ilichukuliwa ili kuihimiza serikali kufuta tamasha hilo mara moja, kutokana na madhara makubwa ambayo lingesababisha kwa jamii na ukiukaji wake wa wazi wa sheria ya Kiislamu. Hati hiyo ilipokelewa na Bi. Wan Saidatul Shafina binti Mohamed Amin, Katibu wa Idara ya Mawasiliano ya Kimkakati na Masuala ya Taasisi, kwa niaba ya Wizara. Pia alitenga muda wa kusikiliza maelezo kamili na ya kina ya sababu za pingamizi zilizowasilishwa na Hizb ut Tahrir Malaysia.

Soma zaidi...

“KL Headline Msimu wa 2026”: Serikali ya Madani Haijali tena Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu!

Kuala Lumpur iko tayari kuibuka kama mahali mwanana pa ziara za matamasha ya kimataifa barani Asia kupitia “KL Headline Msimu wa 2026,” ambao unakutanisha maonyesho 25 ya wasanii wa kimataifa katika mwaka mzima wa 2026. Mji mkuu wa Malaysia umepangwa kuwa mwenyeji wa maonyesho 25 ya wasanii wa kimataifa katika maeneo sita, yakiwalenga zaidi ya mashabiki 500,000 kutoka pwani za ndani na nje ya nchi - kulingana na mratibu, Live Nation Malaysia.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan: Amali kwa Mnasaba wa Idd al-Adha Iliyobarikiwa 1447 H

Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan iliandaa amali katika afisi yake ya Khartoum kusherehekea Idd al-Adha kwa mwaka 1447 H (2026 M). Wakati wa amali hiyo, Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil), msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alitoa hotuba na kujibu maswali kutoka kwa waliohudhuria.

Soma zaidi...

Pongezi kwa Idd ul-Adha Iliyobarikiwa 1447 H

Kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema: «إِنَّ أَعْظَمَ الْأَيَّامِ عِنْدَ اللهِ يَوْمُ النَّحْرِ» “Hakika siku tukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni siku ya Arafah”, basi kwa mnasaba huu uliobarikiwa na kwa kutukuza alama za Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla: ذَلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ﴿ “Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” [Al-Hajj: 32], na Licha ya majanga ambayo Umma wa Kiislamu unapitia chini ya watawala waliouangusha na kuusalimisha kwa adui yake, ambayo yamejaza nyoyo zetu maumivu na huzuni, bado tunapaswa kutoa pongezi na baraka zetu za dhati kwa Umma wetu wa Kiislamu, wenye subira, na wenye kutaraji mema katika Idd al-Adha iliyobarikiwa, tukimwomba Mwenyezi Mungu azifanye siku hizi za Idd kuwa za baraka, ushindi, na kuinuliwa.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu