Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 527
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Enyi Waislamu kwa jumla, na watu wa Ash-Sham hasa: Kiongozi wa Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, anakuonyeni juu ya mikono ya mashetani wa wanadamu wanaotaka damu yenu imwagike bure, ili msifikie wema msafi na dhahiri, kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, bali hukmu iliyotungwa na mwanadamu lakini yenye jina na maana tofauti. Badala ya kuwa Umma ambao makafiri wanauchukulia kwa uzito, mumerudi kuwa wafuasi wa makafiri wakoloni na vibaraka wao, na huu ni uhalifu, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, ambao hatima yake ni udhalilifu duniani na adhabu kali kesho Akhera.
Kabla ya kuanzishwa kwa sarafu, watu walitumia ubadilishanaji wa bidhaa kwa huduma. Kwa kuwa dhahabu na fedha zimezingatiwa kuwa madini ya thamani yenye kima cha asili kwa binadamu tangu nyakati za zamani, zilitabanniwa kama pesa, huku sarafu zikichongwa kwazo ili kurahisisha ubadilishanaji. Dhahabu, hasa, inajulikana kwa kuhimili kwake kuharibika kwa muda mrefu.
Wito kwa Waislamu Wote, Na kwa Watu wa Ash-Sham Hasa!
Hizb ut Tahrir imekuwa mada ya mjadala wa kijamii ndani ya duara zenye ushawishi za Pakistan. Mjadala huo unajumuisha kama tiba za Shariah kwa matatizo ambayo Hizb ut Tahrir inayawasilisha zinapaswa kutekelezwa ili kuepuka matatizo mengi ambayo Pakistan inakabiliana nayo. Kuna mjadala mkali kuhusu Hizb ut Tahrir yenyewe, ikiwemo kupigwa marufuku kwake nchini Pakistan na msimamo mkali dhidi yake katika suala la mateso, unyanyasaji na kifungo. Kwa maslahi ya mjadala wenye tija, mambo yafuatayo ni ya kuzingatiwa na wenye ushawishi kwa jumla na watunga sera, waandishi wa habari, mashirika ya haki za binadamu na ndugu wanasheria hasa.
Hizb ut Tahrir inapinga Ukoloni wa Kithaqafa kwa nchi za Waislamu!
Hizb ut Tahrir inapinga Ukoloni wa Kisiasa wa nchi za Waislamu!
Hizb ut Tahrir inapinga Ukoloni wa Kijeshi wa nchi za Waislamu!
Umma na Majeshi Yake wanao Uwezo wa Kumaliza Mfumo Dhalimu wa Kilimwengu wa Amerika!