Kifo cha Kishahidi cha Mowlavi Ansari ni Muendelezo wa Mauaji ya Ajabu ya Mitandao ya Kijasusi!
- Imepeperushwa katika Afghanistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mowlavi Mujib-ur-Rahman Ansari, mzungumzaji fasaha na khatibu wa Msikiti wa Gazargah, aliuawa shahidi katika mlipuko mmoja pamoja na watu 17, huku makumi ya wengine wakijeruhiwa ndani ya Msikiti wa Gazargah wa mkoa wa Herat. Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan inalaani vikali kabisa shambulizi hili la kikatili na kitendo cha kigaidi, ikilizingatia kuwa ni kinyume na ubinadamu na mafundisho ya Shariah.