Alhamisi, 02 Ramadan 1444 | 2023/03/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  19 Jumada I 1440 Na: 1440 / 012
M.  Ijumaa, 25 Januari 2019

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Wakati Haujawadia kwa Mateso ya Waislamu wa Uyghur Kumalizika?
Je, Wakati Haujawadia wa Kuipa China Funzo Lisilo Sahaulika?

(Imetafsiriwa)

Katika miezi ya hivi karibuni tulisikia ripoti za habari za kupamba moto kwa ukatili wa sera kali za China kwa Waislamu wa Uyghur wanaoishi Mashariki mwa Turkistan, nchi nzuri iliyo Mashariki mwa ardhi ya Waislamu. Haikutulia tangu kunyakuliwa na Mao Zedong utawala wa Kikomunisti wa China mnamo 1949 aliyeliunganisha na eneo la China baada ya kuwauwa zaidi ya Waislamu wa Uyghur milioni moja na kuvunja misikiti elfu 25. Habari za hivi punde lakini zisizo za mwisho za uchunguzi ulioripotiwa na Jarida la Atlantiki na vyombo vyenginevyo vya habari kama BBC na Al-Jazeera, kwamba China inazuilia karibu Waislamu milioni moja katika mkoa wa Turkistan Mashariki katika kambi zake za uzuizi! Uchunguzi huo uliwanukuu wajuzi kutoka Umoja wa Mataifa, kuwa lengo la kambi hizo ni uchafuzi wa kifikra kwa Waislamu wa Uyghur eneo hilo, ili waachane na Uislamu, na inajulikana vyema kuwa China ni mojawapo ya nchi zilizo dhidi ya Uislamu wazi wazi, jarida hilo la kijasusi limechapisha tangazo la China kuwa Uislamu ni maradhi yanayo ambukiza na ni lazima yatibiwe kwa kila njia, hata kupitia mateso na mauwaji.

Uhalifu ndani ya Turkistan Mashariki hauelezeki. Ndugu zetu huko wanafungwa na kunyongwa katika vigogo vya miti, simiti na zege zinamwaga midomoni mwao kuwaziba pumzi, dada zetu wanazuiwa kushika mimba na kuzaa, wanaume wanahasiwa. Serikali ya kikafiri ya China inaweka Mchina kafiri katika kila nyumba ya Muislamu ili kuwachunguza chini ya kisingizio cha kuwaelimisha utamaduni wa Kichina, wakipuuzilia mbali faragha yao na matukufu yao. Waislamu wanazuiwa kufunga mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Waislamu wanalazimishwa kuukana Uislamu chini ya tishio la mateso ya kisaikolojia na kimwili, kwa mujibu wa Shirika la Haki za Kibinadamu.  Mamlaka za China zinadai kuwa zinalazimishwa kukabiliana na kilele cha uhalifu: ugaidi na mfumo wenye misimamo mikali na kulingania kujitenga, kama ilivyo ripotiwa na shirika la habari la BBC. Chini ya miito hii ya kirongo mamlaka hizo zinatekeleza vitendo kadha wa kadha vya kinyama.

Haya yanawatokea Waislamu wa Uyghur eneo la Turkistan Mashariki, na hakuna anayenyosha kidole, hakuna hata shutuma na kukemea madhalimu na watawala wahalifu wa Waislamu wameweza kufanya, kana kwamba Waislamu wa Uyghur sio katika Umma wa Kiislamu, kana kwamba ushindi wao sio wajib juu yao na juu ya Ummah wa Kiislamu! Je, kwani hawajasikia maneno ya Allah, Mtakatifu na Aliye tukuka:

(وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ وَلِيًّا وَاجْعَلْ لَنَا مِنْ لَدُنْكَ نَصِيرًا)

“Na muna nini nyinyi (mpaka) hamupigani katika njia ya Allah na (kwa ajili ya) wanyonge wanaume, wanawake na watoto ambao wanasema, ‘Mola wetu tutoe katika kijiji hichi cha watu madhalimu na utujaaliye kutoka kwako mtetezi na utujaaliye kutoka kwako mwenye kutunusuru” [An-Nisa: 75]

Turkistan Mashariki ilikuwa ni sehemu muhimu ya dola ya Kiislamu. China haikusubutu kuiunganisha hadi baada ya Khilafah Uthmaniyya kuvunjwa na ardhi za Waislamu kugawanywa kuwa idadi ya vidola 50.

Enyi Waislamu:

Ni nini kinachoifanya China kusubutu kuikalia Turkistan?

Ni nini kinachoifanya China kusubutu kuwagandamiza na kuwanyanyasa Waislamu wa Uyghur?

Je, si kwa sababu ya kuwa wamepoteza mchunga anaye chunga mambo yao, wamempoteza Imam muadilifu ambaye hupigana nyuma yake na kuhifadhiwa naye, wamempoteza Khalifah Muongofu anayejibu vilio, kelele na manung’uniko yao?

Enyi Waislamu:

Simameni na muwasaidie ndugu na dada zenu, Waislamu wa Uyghur na Waislamu wote walio kandamizwa Mashariki na Magharibi mwa dunia; kupitia kufanya bidii pamoja na Hizb ut Tahrir ili kuasisi dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, itakayozikomboa ardhi zilizo nyakuliwa za Waislamu, na kuziacha huru shingo za Waislamu kutokana na uimla na ukoloni katika aina zake zote, na itawaadhibu wale walio wakandamiza na itampiga kwa mkono wa chuma yeyote atakayewaza tu kushambulia matukufu ya Uislamu na Waislamu.

Enyi Waislamu: 

Sisi katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir tunatangaza kuzindua kampeni kubwa kwa anwani “Vita vya China Dhidi ya Uislamu eneo la Turkistan Mashariki Vitamalizwa Pekee Kupitia Khilafah Rashidah” ili kuwasaidia ndugu zako na dada zako wa Kiislamu eneo la Turkistan Mashariki, hivyo basi shiriki na sambaza maalumati zake mbali iwezekanavyo. Huenda ulinganizi wetu ukafika masikioni mwa vijana miongoni mwa watu wenye nguvu na ulinzi, na huenda wakawajibu walinganizi wa Allah na kuisaidia Dini Yake ili kusimamisha dola ya kweli (Haq), Dola ya Mtume wa Allah (saw), dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. 

 ( وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاء وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ * وَعْدَ اللَّهِ لا يُخْلِفُ اللَّهُ وَعْدَهُ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لا يَعْلَمُو )

“Na siku hiyo waumini watafurahi* Kwa Nusra ya Allah. Humnusuru amtakaye na Yeye ndiye mwenye nguvu Mwenye kurehemu* (Hii ni) ahadi ya Allah, Allah havunji ahadi yake lakini wengi wa watu hawajui” [Ar-Rum: 4-5]

 

Linki ya kampeni:

https://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/hizbuttahrir/16793.html

 

Hashtag ya Kampeni:

#الخلافة_تحرر_تركستان_الشرقية

#Khilafah_Liberates_EastTurkestan

Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu