Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  23 Jumada I 1440 Na: 1440/014
M.  Jumanne, 29 Januari 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Viongozi wa Muongozo wa Utoaji Fatwa wa Kiulimwengu Harakisheni na Mutubie Kabla Hamujachelewa!
(Imetafsiriwa)

Katikati ya vita muhimu mno vinavyo piganwa na Ummah pamoja na vijana wake, wanaume kwa wanawake, wazee wa kiume na wazee wa kike, na watoto wake waliofariki, waliokufa mashahidi kutokana na sera za kihalifu za Firauni wa zama hizi, Amerika, na watawala Waislamu wanaotekeleza mipango yake. Wamewachinja, kuwakosesha makao na kuwanyima chakula Waislamu, na kuwalipua kwa silaha za kemikali na mabomu, ikiongezewa na makombora aina ya Tomahawk Cruise yanayovuka bahari kuanzia Bahari ya Caspian, Bahari ya Mediterranean, Bahari Nyekundu hadi Bahari ya Arabia, ikiongezewa na ndege ziso rubani (drones) zinazo zizunguka anga za Pakistan, Yemen, Somalia na Afghanistan zikieneza mauwaji na uharibifu.


Katikati mwa hili, ni kikundi kidogo cha wanaume wa Al-Azhar kimeamua kufuata kambi ya Firauni mhalifu Amerika. Kwa hivyo wameamua kuitumia Al-Azhar Al-Shariff, ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ni ngome ya Uislamu na ilitumiwa na Waislamu kupambana na njama za wakoloni na hadaa yao ya endelevu ili kueneza sumu fisidifu za kiitikadi na uhadaifu wa kifikra unaolenga kuichafua itikadi ya Kiislamu na kuigeuza kuwa itikadi lemavu isiyokuwa na tofauti na itikadi nyenginezo za kikafiri, bali wanashiriki katika kumsifu na kumtukuza Firauni wa zama hizi, ikipelekea udhalilishaji wa wale wote wanaolingania waziwazi itikadi ya Tawhid kwa msingi wa shahada ya “Hapana Mola Apasaye Kuabudiwa kwa Haki Isipokuwa Mwenyezi Mungu, Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu” kwa kuwaita magaidi, na kuwabandika majina ya “makundi potevu”, yanayo haribu mipango ya Waamerika wakoloni, na kuyachukulia yenye kuleta ufisadi katika ardhi! Ama kuhusu ufisadi, na uhalifu wa Amerika, kwa mujibu wa Muongozo wa Fatwa za Kiulimwengu (GFI) wa Jumba la Fatwa la Misri, ni mzuri na wenye kuunganisha!


وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ لاَ تُفْسِدُواْ فِي الأَرْضِ قَالُواْ إِنَّمَا نَحْنُ مُصْلِحُونَ * أَلا إِنَّهُمْ هُمُ الْمُفْسِدُونَ وَلَكِن لاَّ يَشْعُرُونَ﴿


“Na wanapo ambiwa, ‘musifanye ufisadi katika ardhi’, wao husema, ‘sisi ni watengezaji’* Bila shaka, wao ni wafisadi, lakini hawahisi” [Al-Baqara: 11-12].


Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na GFI, ni jibu kwa misimamo ya kiitikadi inayo eleza hukmu kwa yale yote yaliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu kwa msingi wa fahamu iliyooza ya uzalendo iliyo chukuliwa kutoka kwa hadhara ya Kimagharibi. Muongozo huo unapinga msimamo wa Hizb ut Tahrir, pamoja na harakati kadhaa za Kiislamu, zinazo pinga sanamu lililotwa la Utaifa. Hoja walioileta ni kuwa Hizb ut Tahrir inaamini kuwa “itikadi ya Kiislamu ndio msingi wa dola na nyumba (Dar) ya Uislamu ni nchi ambako hukmu za Uislamu zinatekelezwa.”


Hii ni kinyume na nguzo za dini ya kikoloni “Utaifa”, ambayo wakoloni Wamagharibi wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii kwa takriban miongo miwili ili kulazimisha na kupigia debe fahamu zao zenye sumu, kwa kuwatumia baadhi ya wale wanaovalia sare za wanazuoni na wale wanaoshirikiana nao. Hakika, wanazuoni hao walipaswa kuwa warithi wa mitume na kustahili kuwa safu ya mbele ya Ummah, kuwaongoza katika kupambana na kampeni za kikoloni, zinazo washambulia kwa mawimbi mithili ya mawimbi ya bahari, na zinazo lenga kuhujumu Dini hii tukufu na umoja wa Ummah wa Kiislamu, ili kuugawanya, kuuvunjavunja na kuutenganisha, na kuchukua kutoka katika ukabila na uzalendo kisingizio cha kukuza chuki na hasira miongoni mwa Waislamu, na hata kuwashajiisha kumwagana damu zao kwa mikono yao. Kama yale yaliyotokea kwa mvuvi kutoka Gaza, alipokuwa anatafuta riziki, lakini dau lake likavuka bahari, na akawa ametekeleza “uhalifu mkubwa mno” wa kuvuka mpaka wa sanamu la Misri; mwanajeshi wa Misri akampiga risasi na kumuua. Hili ndilo sanamu la utaifa ambalo Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu unalingania kulitetea.


Na unasimama dhidi ya misimamo ya Waislamu wanaotaka kushikamana na itikadi ya Kiislamu. Ulitamatisha katika taarifa yake kwa kusema: “Muongozo huu umesisitiza umuhimu wa dori ya taasisi za kizalendo na kidini katika kuhudumia nchi zao na kusaidia juhudi zao katika nyanja tofauti tofauti ili kufikia usalama, ustawi, maendeleo na ufanisi kwa nchi na watu wake.” Unadai kujali kirongo usalama na ustawi, lau kama GFI ingekuwa ni mkweli inge shutumu uhalifu wa katili wa Misri Sisi, aliye mwaga damu tukufu katika viwanja vya Misri na barabara zake, na angali anawakamata kinyume cha sheria maelfu ya watu wa Misri, huku akikimbilia kuwaridhisha Mayahudi na Waamerika.
Jambo kubwa sana linaouathiri Uislamu, watu wake na wafuasi wake, ni kuwa mstari unaogawanya baina ya Uislamu na Ukafiri, baina ya haki na batili, na baina ya njia ya waumini na njia ya wahalifu umeyeyuka … hivyo Dini hii imepotea na mafundo yake kufunguka moja baada ya moja, kama Umar (ra) alivyosema: “mafundo ya Uislamu yatafunguka, moja baada ya moja, ikiwa katika Uislamu kuna wale waliokulia pasi na kuzijua siku za ujahiliya”
Hii ndio sababu Mwenyezi Mungu (swt) anasema:


﴾وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ وَلِتَسْتَبِينَ سَبِيلُ الْمُجْرِمِينَ﴿


“Na kwa hivyo basi tunazifafanu Aya hizi, na ili njia ya wahalifu idhihirike” [Al-An’am: 55]


Udhahiri wa ukafiri, uovu, uhalifu na ufasiki ni muhimu kwa ajili ya udhahiri wa iman, kheri na wema … Kutambulishwa kwa njia za wahalifu ni mojawapo ya malengo ya ufafanuzi wa aya zilizo teremshwa kwa wahyi. Kutofahamika au shaka yoyote katika msimamo wa wahalifu na njia yao itamulikwa kama kutofahamika au shaka katika msimamo wa waumini na katika njia yao. Hivyo basi, ni wajib kuweka wazi mistari na misimamo hii. Tumeonywa na Al-Haq (swt) kutokana na kufuata njia za Manaswara na Mayahudi, na Yeye (swt) ametukataza kuwatii wanazuoni wanaofanya biashara na Dini, kwa kuhalalisha Haram na kuharamisha Halal:


﴾اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَاباً مِنْ دُونِ اللَّهِ وَالْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا إِلَهاً وَاحِداً لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ﴿


“Wamewachukua wanazuoni wao na makasisi wao kuwa ni miungu kando na Mwenyezi Mungu, na [pia] Masihi, mwana wa Maryam. Na hawakuamrishwa isipokuwa wamuabudu Mola mmoja; hakuna Mola mwengine wa haki isipokuwa Yeye. Utakatifu ni wake Yeye kutokana na yale wanayo mshirikisha nayo.” [At-Tawba: 31]


Licha ya hayo, tunatamatisha kwa kuwalingania viongozi wa Muongozo wa Fatwa wa Kiulimwengu wa Jumba la Fatwa la Misri kwa haraka kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kusimama upande wa Ummah. Ili kupata utukufu wa kuwa warithi wa Mitume pindi watakapo tangaza neno la haki, na hili ndilo linaloturidhisha, na ndilo ambalo Mwenyezi Mungu na Mtume Wake (saw) walilofaradhisha. Ikiwa wao ni katika genge la majasusi wa kigeni, tunawaonya juu ya hasira za Mwenyezi Mungu hapa duniani na kesho Akhera, na tunawapa habari njema kuwa ahadi ya Allah ni ya kweli.


﴾هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ﴿


“Yeye ndiye aliyemtumiliza Mtume wake kwa uongofu na Dini ya haki ili aidhihirishe juu ya dini zote, hata kama washirikina watachukia.” [As-Saff: 9]


﴾وَلَتَعْلَمُنَّ نَبَأَهُ بَعْد حِين﴿


“Na kwa yakini mutajua [ukweli] wa habari yake hivi punde.” [As-Sad: 88]


Dkt. Osman Bakhach
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu