Alhamisi, 02 Ramadan 1444 | 2023/03/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  24 Muharram 1440 Na: 1440 H/ 07
M.  Jumapili, 31 Machi 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Kenya Imefaulu Kukamilisha Kampeni Maalum kwa Mwito – Kuzidi Kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba

         

Jumapili, 31 Machi 2019, Hizb ut Tahrir / Kenya kwa ridhaa za Mwenyezi Mungu (swt) ili kamilisha kampeni yake kwa mwito "Kuzidi kwa Gharama za Maisha: Uislamu Ndio Tiba" ambayo ili zinduliwa rasmi Jumapili, 13 Januari 2019.

Lengo la kampeni lilikuwa ni kufichua dori ya ukoloni urasilimali katika kuendeleza matatizo ya kiuchumi kwa ujumla ambayo yanaendelea kulikumba taifa la Kenya na dunia kwa jumla. Kampeni ili lenga amali kadhaa zikijumuisha Darsa, Maandamano baridi, Kuwazuru watu wenye usemi na kujadiliana nao kuhusu masuala yanayo ukumba Ummah wa Waislamu. Muda wote wa kampeni tuliweza kuwasilisha suluhisho la Uislamu katika kutatua matatizo ya kiuchumi kwa ukamilifu na ambao pia una sheria za kupambana na matatizo yote yanayo wakabili wanadamu.       

Kampeni hii ilikuwa moja ya kazi za Hizb ut Tahri katika kujenga rai jumla kwa kuwasilisha sera ya uchumi safi inayo chipuza kutoka kwa Nidhamu ya Uchumi ya Kiislamu ambayo ili tekelezwa kivitendo kwa karne 13 chini ya Dola ya Kiislamu ya Khilafah. Ndani ya muda wote wa utekelezwaji wake, Ummah haukupata machungu ya minyororo kama inavyopitia leo chini ya nidhamu ya ulafi wa uchumi wa kirasilimali. Kwa kuwa bado Ummah unaishi chini ya udhibiti wa nidhamu fisadi ya uchumi wa kirasilimali, umedidimia katika matatizo ya kiuchumi! Tunatarajia Ummah umezinduka na utaongeza juhudi zao katika kufanya kazi kuleta mabadiliko msingi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kukubali amali zetu na zenu na kuubariki Ummah huu kupata mlinzi na ngao ya Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ambayo kwa mara nyingine itawakomboa wanadamu kutoka katika njama za kiuchumi na maovu mengineo kwa kutekeleza mfumo wa Kiislamu na nidhamu zake ikijumuisha nidhamu ya uchumi ya Kiislamu pamoja na sera yake adhimu iliyomo ndani yake.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi Kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu