Jumatatu, 30 Safar 1444 | 2022/09/26
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  26 Rajab 1440 Na: 1440H/08
M.  Jumanne, 02 Aprili 2019

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Dola ya Uchina na Utawala wake Unaogopa Mwito wa La ilaha illa Allah

Jumanne, 2 Aprili 2019, Hizb ut Tahrir Kenya ilituma ujumbe wake kwa Ubalozi wa Uchina nchini Kenya. Ujumbe huo uliongozwa na Mkuu wa Kamati ya Mawasiliano wa Hizb ut Tahrir /Kenya Arkanuddinn Yassin, akifuatana na Shabani Mwalimu -Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir /Kenya. Waliwasili katika ubalozi mjini Nairobi saa 8:56 a.m EAT.

Ubalozi ulikataa kupokea au kukubali nakala/ujumbe kuhusiana na Uyghur wanaopitia ukandamizaji kutoka kwa Dola ya Uchina, kwa kuuona mwito wa La ilaha illa Allah wa Muhammad (saw) katika kalima rasmi za Hizb ut Tahrir. Hizb ut Tahrir /Kenya haikushangazwa na hatua hiyo ya ubalozi, kwani ni jambo la kawaida linalotarajiwa kutoka kwa tawala kandamizaji ulimwenguni kote. Tunaiona ni ishara ya kiburi na kuchupa mipaka kwa Dola ya Uchina mbele ya haki ambayo ni Uislamu! Hizb ut Tahrir itaendelea kuwa safu ya mbele katika kupinga uhalifu wa kinyama unaofanywa na tawala zote fisadi dhidi ya Waislamu duniani kote.

Barua waliyofikishiwa ilikuwa ni taarifa kwa vyombo vya habari kwa kichwa:"Khilafah Itakomboa Turkestan Mashariki Na kuwanusuru Uyghur kutoka kwa Ukandamizaji wa Kihalifu wa Uchina." Iliyotolewa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir. Sehemu ya taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilisema kama ifuatavyo:" Huku utawala wa Uchina ukiendelea kuwahangaisha Waislamu wa Uyghur kwa kutumia kila mbinu ya kidhalimu ikiwa ni pamoja na kuwawekea vikwazo wasitekeleze ibada zao na wasihudhurie misikiti kwa kuifunga, kuwalazimisha wasifunge katika mwezi wa baraka wa Ramadhan, na kupiga marufuku ibada aina yoyote ya Kiislamu mpaka hivi majuzi wamezindua kambi kubwa na kuwafunga Waislamu zaidi ya milioni 1 ndani ya kuta zake eti ni kampeni inayodaiwa kulenga "kupambana na ugaidi" kwa kisingizio cha mwito wa: "mafunzo ya kitaaluma" na huku ikiwashika wasomi, wanasayansi, wanafikra na maprofesa wa vyuo. Yote haya ili kueneza wasiwasi na kutia hofu katika mioyo ya Waislamu ili kujisalimisha kwa udhaifu wa ushikamanaji wa Dini yao ya Kiislamu."

Kisha barua ikatamatisha kwamba ni Khilafah Rashidah (Khilafah iliyoongoka) kwa njia ya Utume ambayo itasimama hivi karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu italeta ushindi kwa ndugu zetu waliokandamizwa ndani ya Turkestan Mashariki na itawahesabu wote walio wakandamiza na kuwatenga, Mtume (saw) alisema:

«إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi ni ngao, nyuma yake mnapigana na kujilinda”

Na wakati huo si Uchina wala mwengine atakayejaribu kuwadhuru Waislamu kwa sababu watajua kuwa chochote watakacho kifanya kitaregeshwa kwao mara dufu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu na Muweza.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu