Ijumaa, 16 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  27 Rajab 1443 Na: 1443/08 H
M.  Jumatatu, 28 Februari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Kenya Yaandaa Kampeni ya Kumbukumbu Miaka 101 ya Kuvunjwa kwa Khilafah Yetu

Kama sehemu ya kumbukizi ya miaka 101 tokea kuvunjwa kwa Khilafah, Harakati ya Hizb ut-Tahrir Kenya ilifanya kampeni yenye kauli mbiu KHILAFAH HITAJIO LETU kwa kuandaa msururu wa amali huku kubwa zaidi ni hizi:-

1-Maandamano baridi baada ya Swala ya Ijumaa sehemu mbali mbali za nchi. (Haya yalifanywa tarehe 24 Rajab 1443 H sawa na tarehe 25 Februari 2022 M)

2-Ziara za mitaani na kuzungumza na watu (Ilifanyika Jumamosi tarehe 25 Rajab 2022 sambamba na Februari 26, 2022)

3- Kuandaliwa kwa semina tarehe 26 Rajab 1443, sawa na Februari 2022, Semina hii ilikuwa chini ya kauli mbiu KHILAFAH HITAJIO LETU. Katika semina hii mada mbili ziliwasilishwa kwa wahudhuriaji.

  • Miaka 101 pasina na Khilafah mzungumzaji; Ustadh Mohamad Khamsin mwanachama wa Hizb ut-Tahrir Kenya
  • Khilafah Hitajio Letu Mzungumzaji; Shabani Mwalimu – Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari Hizb ut Tahrir Kenya.

Katika kampeni hii Umma wa Kiislamu ulikumbushwa hali mbaya ya kutamausha iliowasibu tokea kuvunjwe Khialafah tarehe 28 Rajab 1342 H sawa na tarehe 3 Machi,1924 M. Tokea tukio hili la kuhuzunisha, Umma umegawanywa kupitia ule mradi wa kikoloni wa Sykes – Picot  biladi zao zikagawanya na kuwekwa kwenye ukoloni unaotishia usalama na amani. Biladi zao zikakosa amani huku damu za Waislamu zikimwagwa na kuchuruzika kama mito… damu za mama zetu na watoto wetu zikimwagwa huko Syria, Yemen, China na nchi zote za Kiislamu jumla.

Kwa idadi ya takriban bilioni mbili Waislamu leo wamekuwa kama povu la bahari hii ni kutokamana na kukosekanwa kwao kwa Khalifa ambaye ndiye mlinzi na ngao yao. Umma wa Kiislamu ukakosa heshima, hadhi na mlinzi. Tumeipoteza Al-Aqswa Ardhi Iliyobarikiwa ya Israa’ wal Miiraj ambayo pia ni kibla chetu cha kwanza. Ni kwa kupitia Khilafah Al-Raashidah – ndio itakayoirudisha bali kurudisha biladi zetu zote zinazokaliwa kimabavu.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu SWT atufanyie haraka kusimama kwa Khilafah Raashidah kwa Njia ya Utume na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hili. Mtume (SAAW) amesema:

"تكون النبوة فيكم ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها الله إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج النبوة فتكون ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها الله إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون ملكًا عاضًا فيكون ما شاء الله أن يكون، ثم يرفعها إذا شاء الله أن يرفعها، ثم تكون ملكًا جبرية فتكون ما شاء الله أن تكون، ثم يرفعها الله إذا شاء أن يرفعها، ثم تكون خلافة على منهاج النبوة، ثم سكت"

 "Utakuweko kwenu unabii kwa kadri ya muda atakaoutaka Mwenyezi Mungu kuweko kwake. Kisha Mwenyezi Mungu atauondoa pindi atakapotaka kuondoa kisha iwe Khilafah kwa mfumo wa unabii, uweko kadri ya atakavyo Mwenyezi Mungu kuweko kisha auondoe atakapotaka kuundoa. Kisha ufuate ufalme wa kuumana uwe kwa kadri ya muda autakao Mwenyezi Mungu kisha aundoe pale atakapotaka kuondoa. Kisha baadaye kuweko na utawala wa kidikteta uwe kwa muda autakao Mwenyezi Mungu kuweko kisha aundoe atakapotaka kuondoa kisha iwe Khilafah kwa mfumo wa unabii kisha akanyamaza." [Musnad ya Imam Ahmad].

Mwisho, tuna imani kubwa juu ya kurudi tena kwa Khilafah Raashida kwa mfumo wa unabii hapo Dini, maisha na matukufu yetu yatahifadhiwa na siku hiyo waumini watafurahi kwa nusra ya MwenyeziMungu.

(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ)

"Na siku hiyo waumini watafurahi." [Ar-Rum: 4]

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir

Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu