Ardhi Zetu Zitabaki Kukiukwa na Damu Yetu Itaendelea Kumwagika Hadi Tutakaposimamisha Khilafah Rashida Yetu
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo Jumapili, tarehe 14 Juni 2026, jeshi la Kiyahudi lilifanya shambulizi la anga likilenga vitongoji vya kusini mwa Beirut, saa chache tu baada ya kuwaonya wakaazi wa takriban miji 30 kusini mwa Lebanon na kuwaamuru waondoke. Tovuti ya habari ya Axios iliripoti kwamba “jeshi la ‘Israel’ liliiarifu CENTCOM muda mfupi kabla ya shambulizi jijini Beirut kutokea.” Trump aliandika kwenye jukwaa lake la ‘Truth Social’ mnamo Jumapili: “Shambulizi la asubuhi ya leo dhidi ya Beirut halikupaswa kutokea, haswa katika siku maalum ambapo tuko karibu sana na Mkataba wa Amani na Iran.”



