Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Kikao “Waliohamishwa Ni Ndugu Zetu”
- Imepeperushwa katika Lebanon
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon iliandaa kikao kikubwa katika mji wa Tripoli Ash-Sham, kuanzia Msikiti Mkuu wa Al-Mansouri. Hii ilikuwa ni kueleza mshikamano wao pamoja na waliohamishwa na wakimbizi kutoka Syria, ambao walikimbia ukandamizaji wa utawala wa mhalifu Assad na kutafuta hifadhi kwa ndugu zao nchini Lebanon kutafuta usalama na makaazi hadi wapate fursa ya kuregea kwa heshima na usalama katika nchi yao ambako walilelewa na kukulia.



