Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 444
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) iliandaa kisimamo cha halaiki katikati mwa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, ambapo kupitia kwacho ilitoa wito kwa majeshi ya Umma wa Kiislamu kujibu hujma ya Mayahudi dhidi ya Msikiti wa Al-Aqsa uliobarikiwa na kuchafuliwa kwake, na kupandisha bendera ya umbile lao liliopotoka katika viwanja vyake na matusi yao kwa Mtume (saw).
Ujumbe wa dharura wa Mhandisi Ismail Al-Wahwah (Abu Anas) Mwenyezi Mungu amrehemu
Hizb ut Tahrir / Amerika ilifanya Kongamano lake la kila mwaka la Khilafah kwa mafanikio. Hafla hii ni sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kukumbuka kuondolewa kwa Khilafah mwaka 1924.
Je, Malengo ya NEMC Ni Kupiga Marufuku Adhana Zinazotumia Vipaza Sauti?
Ni muhimu kufahamu maana na uhalisia wa neno “Jahiliyah” ili tuifahamu jamii ya sasa ambayo tunaishi. Ili, hitajio la kurejesha tena Khilafah liwe na umuhimu wa kipekee katika maisha ya Waislamu. Tunapoangalia uhalisia wa jamii ya Makkah yenyewe na Waarabu kwa jumla, tunaona kwamba kulikuwa na baadhi ya makabila yanayo hama hama na kulikuwa na uwepo wa makabila kama Thaqif, Quraish, Shaiban na mengineyo.
Kwa imani na kujisalimisha kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Jordan inaomboleza kwa Waislamu kwa jumla, na watu wa Jordan na Waislamu hasa wa Australia, mmoja wa wanachama wanyoofu, wenye subira na waheshimika wa hizb, mwenye misimamo imara yenye kumridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), na sisi hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu.
Mwanafikra wa kisiasa kutoka kizazi cha zamani cha wanachama wa Hizb ut Tahrir
MhandisiIsmail Al-Wahwah (Abu Anas)
Rais wa Indonesia Joko Widodo amethibitisha kwamba kuwalinda wafanyikazi wahamiaji na wahanga wa ulanguzi wa binadamu ni mojawapo ya makubaliano msingi yaliyotokana na Mkutano wa 42 wa Wakuu wa ASEAN uliomalizika hivi karibuni huko Labuan Bajo, Indonesia, Mei 2023.
Mnamo tarehe 18 Mei 2023, Mwenyekiti wa Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), Imran Khan, alilaani shambulizi kwenye mitambo ya jeshi. Alisema muungano tawala wa PDM ulitaka kuiondoa PTI kutoka kwa siasa za kuu kupitia kuligombanisha jeshi na chama cha upinzani.
Kamanda wa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), Jenerali Michael Kurilla aliwasilisha ripoti kwa Bunge la Congress kuhusu operesheni yao ya kijasusi kuanzia robo ya kwanza ya mwaka huku akisema kuwa Taliban wana dhamira kubwa ya kuiangamiza Dola ya Kiislamu-Khorasan (IS-K) nchini humo, lakini kulingana na yeye, Taliban hawana uwezo wa kuzuia mashambulizi ya kigaidi ya mustakbali ya kundi hilo lililotajwa. Hivyo basi, Marekani inaongeza juhudi za uchunguzi juu ya anga ya Afghanistan.