Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 304
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Vichwa Vikuu vya Toleo 304
Vichwa Vikuu vya Toleo 304
Machafuko ya 2020 ya Maisha ya Weusi ni ya Kuzingatiwa (Black Lives Matter) hivi sasa yamefikia kwenye mwezi wake wa nne, yakiweka kivuli kirefu juu ya uchaguzi wa urais wa Amerika. Machafuko ya umma yaliripuka kutokana na kifo cha George Floyd mnamo tarehe 25 Mei 2020 na yamechochewa kwa miongo ya miaka ya ubaguzi wa kitaasisi.
Mnamo tarehe 27 Agosti, shirika la habari la ‘Buzzfeed News’ lilichapisha taarifa zilizotokana na uchunguzi ulioegemea maelfu ya picha za satelaiti katika eneo la ‘Xinjiang’ inayofichua “miundo mbinu mikubwa na inayoendelea ya uwekaji kizuizini na kushikiliwa kwa muda mrefu” kwa jamii za Uyghur, Kazakh na Waislamu wengine inayotekelezwa na utawala wa kidhalimu wa China.
France 24 jana 14/9/2020 M ilichapisha: (Mashariki ya kati, Jumanne itaingia kwenye mkondo mpya, wakati ambapo dola ya Imarati na Ufalme wa Bahrain zitatia saini mkataba wa makubaliano pamoja na (Israel) huko Washington…
Somalia ni taifa ambalo linaruka janga kuingia janga jingine yote yakichochewa na wakoloni Wamagharibi wakiongozwa na Amerika na washirika wake upande mmoja na Ulaya, hususan Uingereza na washirika wake upande mwingine.
Mnamo tarehe 13 Agosti 2020, ‘Israel’ na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) zilikubaliana juu ya Mkataba wa Abraham (Abraham Accord).
Mnamo tarehe 4 Septemba 2020 gazeti la The Guardian limeripoti juu ya ushuhuda wa mwalimu Muislamu wa Kiuighur aliyelazimishwa kufanyiwa hatua nyingi za kudhibiti kizazi baada ya kupata vitisho vya mara kwa mara kwa maisha yake na ya familia yake.
Baada ya jarida la vichekesho la Kifaransa la Charlie Hebdo, kurudia tena kuchapisha michoro ya vikaragosi vya kumtusi Mtume Muhammad (saw) kabla ya kesi ya mshtakiwa kwa shambulizi la makao yake makuu mnamo 2015,
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa kisimamo cha kukataa kipengee cha kutenganisha dini na dola (sekula), katika makubaliano yaliyotamatishwa baina ya Waziri Mkuu Abdullah Hamdok na Abdel Aziz Al-Hilu,
Vichwa Vikuu vya Toleo 303