Bila jeshi hata moja la Waislamu kumzuia, Trump alitimiza ahadi yake ya kufanya maangamizi makubwa Gaza. Kamera zimenasa picha za sehemu za miili ya waumini zikipaa angani, juu ya majengo marefu, kutokana na kukithiri kwa mashambulizi ya makombora. Madaktari wa uokoaji wanafunikwa macho na kupigwa risasi. Watoto, wanawake, wazee na waliojeruhiwa wanauawa shahidi kwa kulipuliwa mahema yao. Sera ya njaa ya Amerika, iliyotekelezwa na wafuasi wake, umbile la Kiyahudi, imeongeza mateso hadi kiwango cha baa la njaa. Sasa imedhihirika kwa kila mtu kwamba Firauni wa Washington anafanya maangamizi makubwa kwa Gaza, kwa usaidizi kamili wa kijeshi na uongozi wa kisiasa wa Waislamu na Mayahudi.