Jumanne, 29 Sha'aban 1444 | 2023/03/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  11 Rajab 1443 Na: BN/S 1443 / 09
M.  Jumamosi, 12 Februari 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza cha Hizb ut Tahrir

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza katika wanaume wake, mbebaji Da'wah kutoka kizazi cha kwanza katika safu zake. Marhum bi idhnillah (swt):

Al-Hajj Ibrahim Ahmad Musa Hind (Abul-Munthir)

Ambaye alikwenda katika rehma za Mwenyezi Mungu (swt) katikati ya usiku wa Jumamosi 12/2/2022 akiwa na umri wa miaka 91. Al-Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, alijiunga na ulinganizi pamoja na Sheikh Taqiuddin an-Nabhani, Mwenyezi Mungu amrehemu, tangu mwanzo wa shughuli yake mwaka wa 1952 na kabla ya kutangazwa kuasisiwa kwa Hizb, kisha akayatumia maisha yake katika kubeba ulinganizi wa Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume popote alipo kwenda na kusafiri. Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa ni mshale miongoni mwa mishale ya kazi ya kuregesha mfumo wa kamili wa maisha ya Kiislamu, mtiifu, mwenye ikhlasi, aliye vumilia kwa ajili kifungo, dhiki, na safari, kama mwalimu na mhubiri kwa watu katika misikiti, hafla, mabaraza, na kupitia mtandaoni.

Licha ya uzee wake, aliendelea kuwa mchangamfu, mvumilivu, akihudhuria halaqa, akishiriki katika amali, kusoma matoleo, kuwapenda wanachama na alikuwa mwenza wao, akiwaombea na wao wakimuombea kwa kheri zote, mapenzi na ikhlasi. Aliishi akizingatia ahadi yake na Mwenyezi Mungu hadi dakika za mwisho za uhai wake na akafa juu ya hilo, akiwacha nyuma yake kizazi chema kilichobeba Dawah chenye kuupenda Uislamu na kufanya kazi ya kuuinua, mithili yake yeye katika amali, azma na utoaji, jambo ambalo litakuwa ni rasilimali kwake na katika mizani ya mema yake, Mwenyezi Mungu akipenda.

Mwenyezi Mungu amrehemu maiti wetu kwa rehema zake nyingi, na amjaalie maskani yake katika Bustani zake pana, Inna Lilah Wa Inna Ilaihi Raji’uon, “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye hakika tutaregea”. Mwenyezi Mungu awalipe ujira mwema jamaa zake na watu wake na awajaalie subira na faraja, na sisi hatusemi ila yanayomridhisha Mwenyezi Mungu (swt). Ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na ni cha Mwenyezi Mungu alichokichukua, na kila kitu kwake kimewekwa kwa muda maalumu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

- Kalima ya Mhandisi Baher Saleh, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir, katika mazishi ya marehemu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, Aba al-Mundhir –

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu