Jumamosi, 15 Dhu al-Qi'dah 1444 | 2023/06/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  20 Rabi' I 1444 Na: BN/S 1444 / 05
M.  Jumapili, 16 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Je, Huduma za Usalama na Huduma ya Kijasusi ya Kijeshi Zinatoa Kinga kwa Wahalifu Miongoni mwa Wanachama wao?!

(Imetafsiriwa)

Katika mfano hatari, na uhalifu kamili wa kulaaniwa, jana, Jumamosi 15/10/2022, kundi la shabiha (wanamgambo) mjini Ramallah wanaohusishwa na vyombo vya usalama; kati ya mfanyikazi, watoto wake na mshirika wake wa karibu, anayejulikana kwa jina na cheo, waliwashambulia idadi ya wafanyikazi wa Hizb ut Tahrir kwa visu na marungu mbele ya Msikiti wa Saad bin Muadh mjini Ramallah, pia katika jaribio la kumkanya kwa gari kijana mdogo, na kumjeruhi mwengine kwa majeraha kadhaa mwilini na kichwani kwa visu, pamoja na kuharibu gari jengine, na tishio lao la wazi la kuua na kupiga risasi, yote hayo yamechanganyika na uhalifu wa kulaani hotuba ya kiwahyi kwa maneno machafu yanayostahiki tu majambazi na uovu.

Ukweli kwamba Huduma ya Ujasusi ya Kijeshi ilitoa dhamana kwa mmoja wa wanachama wake, ambapo malalamishi yaliwasilishwa kwa Ujasusi wa Kijeshi siku mbili zilizopita kutokana na kutishia kwake kumuua mmoja wa wafanyikazi wa hizb, ni moja ya jinai kubwa, na lau haingekuwa ni kwa ushirikiano wa wanachama wa Ujasusi wa Kijeshi, mhalifu huyu na wanawe wasingesubutu kutekeleza tishio lao siku iliyofuata.

Mamlaka ya Palestina ndiyo inayobeba matokeo ya uhalifu huu. Majina ya wale waliofanya uvamizi yanajulikana kwake, na ushahidi wa uhalifu wao ni orodha ya mashahidi na video, na uhalifu huu unaakisi hali ya vipengee vya huduma za usalama vilivyofunzwa na Jenerali Dayton na kuwaita "Mpalestina mpya!”, Mpalestina ambaye ana chuki na watu wa Palestina na watetezi wa Uislamu na anajivunia uvamizi na utumishi wake.

Na kwamba Mamlaka ya Palestina na vyombo vyake vya usalama inahusika na jinai za wahusika wake, na kwamba uchokozi huu una madhara yake, na hili limesitishwa katika utendaji wa Mamlaka ya Palestina dhidi ya wahalifu hao. Ima inathibitisha kwamba inawajibika kwa uhalifu wao, au inakomesha mikono yao na kuwaadhibu wale waliofanya uhalifu huu.

﴿وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَاناً وَإِثْماً مُّبِيناً

“Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.” [Al-Ahzab:58]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu