Jumatatu, 19 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  29 Rabi' I 1444 Na: BN/S 1444 / 06
M.  Jumanne, 25 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mauaji ya Nablus, na Ushujaa wa watu wake, Yafichua Wazembe, na Kutuma Ujumbe kwa Majeshi ya Kiislamu!

 (Imetafsiriwa)

Mujahidina watano waliuawa shahidi, akiwemo mmoja wa viongozi mashuhuri wa kundi la Areen Al-Asoud (Shimo la Simba), Wadih al-Hawah, na wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa kwa risasi za jeshi la Mayahudi. Majeraha ya watano kati yao yalielezewa kuwa mabaya, wakati wa shambulizi kwenye Mji wa Kale wa Nablus.

Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Yair Lapid, alisema kuwa rais wa Palestina lazima adhibiti uwanja ikiwa anataka kuleta utulivu kwa mamlaka yake. Wakati huo huo, Msemaji wa Rais wa Palestina Nabil Abu Rudeineh alisema kuwa Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas alitoa maagizo yake kuwasiliana na upande wa Marekani mara moja ili kukomesha uchokozi wa Kiyahudi dhidi ya Nablus. Baraza la Mawaziri la Palestina pia lilitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa ya haki za binadamu kuingilia kati ili kukomesha uchochezi wa Mayahudi huko Nablus.

Kinachotokea Nablus kinathibitisha kwa mara nyingine tena kile ambacho matukio yamethibitisha mara kwa mara kwa kila uchokozi wa umbile la Kiyahudi. Inathibitisha uoga wa umbile hili na kutokuwa na uthabiti mbele ya watu walio na nusu-ulinzi, basi itakuwaje iwapo litakabiliana na jeshi kubwa linalotarajia kufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, jeshi linalopenda kifo kama ambavyo waoga hawa wanapenda uhai?! Vile vile inathibitisha kuwa tawala katika nchi za Kiislamu ndizo zinazotoa ulinzi kwa uhalifu wake, huku wakichunga usalama wake, na ilhali wanaona na kusikia uhalifu linaloufanya na hawanyooshi hata kidole, badala yake wanakazanisha mikono yake ili kufanya mengi zaidi kupitia uhalalishaji wao mahusiano na uwekaji mipaka na kupitia kuridhia kwao wizi wake wa utajiri wa Waislamu! Vile vile inathibitisha kuwa jukumu la Ummah ni jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, na kwamba hakuna suluhisho isipokuwa kwa kuikomboa tu, na hilo ni kupitia msaada wa majeshi ya Ummah pekee, si Umoja wa Mataifa wala si Marekani.

Mtazamo wa Mamlaka ya Palestina ni msimamo dhaifu, kwani ina uwezo wa kuhamasisha makumi ya maelfu ya vyombo vyake vya usalama vilivyo na silaha kulinda na kuhami watu, na hii ndio kazi ya vyombo vya usalama ulimwenguni, au inapatikana tu kulinda umbile la Kiyahudi na kuwaandama na kuwakamata mujahidina?!

Mtazamo wa rais wa Mamlaka ya Palestina, ambaye aliamuru kuanzisha mawasiliano na Amerika ili kukomesha uchokozi dhidi ya watu wa Palestina, ni njama, dharau na ujinga wa kisiasa. Marekani ni kichwa cha ukafiri kinachotoa hifadhi kwa umbile la Kiyahudi kufanya jinai zake, na ndiyo inayoipatia fedha, silaha na nyenzo za kuwadhulumu watu wa Palestina, na ndiyo iliyotoa idhini kwa Gantz na Lapid kuwaua watu wa Palestina ili damu yao safi iwe kadi ya uchaguzi kwao, hivi ni mtu gani mwenye akili timamu angetafuta kinga dhidi ya moto uwakao?! Au mamlaka ya Palestina iliyotokana na uamuzi wa kimataifa ina uwezo tu wa kusujudu kwenye mlangoni mwa Ikulu ya White House na Umoja wa Mataifa?!

Ni jinai kubwa na uhaini mkubwa kwamba maombi yanaelekezwa kwa adui wa Ummah, Marekani, jumuiya ya kimataifa na taasisi za kimataifa zenye uadui, na hayaelekezwi kwa Umma wa Kiislamu na majeshi yake, kwani ndio mmiliki wa jambo hilo na ndiye pekee mwenye uwezo wa kulimaliza?!

Kuhutubia Ummah na majeshi yake ili wasonge ndio njia pekee ya kuwasukuma kusonga mbele, na kuusukuma Umma na majeshi yake ndio njia pekee ya kuwaokoa watu wa Palestina, ndio maana maadui na zana zao wanapambana na mazungumzo haya na kuyazuia katika vyombo vya habari, na tawala haziyalinganii haya na makundi yanayatenga haya, licha ya kuwa ndio suluhisho pekee na la kivitendo kwa kadhia ya Palestina!

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa: Mkisubiri na mkashikamana na Dini yenu, Mwenyezi Mungu atakufanyieni wepesi baada ya dhiki, na atakuandalieni askari watakaoikomboa njia ya Mtume wenu (saw), na wataingia msikitini kama wafunguzi walivyoingia humo kwa mara ya kwanza, basi shikamaneni na dini yenu na Ummah wenu na mtafute nusra ya vizazi vya Khalid na Swalah al-Din, na muachane na miradi ya wakoloni, na mwisho utakuwa katika neema yenu. Mwenyezi Mungu ndiye mola wenu, na wao hawana mola.

﴿إِن يَنصُرْكُمُ اللَّهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ﴾

“Akikunusuruni Mwenyezi Mungu hapana wa kukushindeni, na akikutupeni ni nani, basi, baada yake Yeye ataye kunusuruni? Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu..” [Ali’ Imran 3:160]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu