Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 522
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni mwaka mmoja kamili baada ya watawala wa Waarabu na Waislamu kukusanyika kujadili kadhia ya Palestina kufuatia mkasa wa Oktoba 7, wanakutana tena mahali pale pale, pamoja na mtu yule yule, wakishughulikia tatizo lile lile, na hatimaye kutoa maazimio yale yale! Zaidi ya viongozi 50 wa dola za Waislamu walihudhuria Mkutano wa Waarabu na Waislamu mnamo tarehe 11/11/2024, akiwemo Waziri Mkuu wa Malaysia. Kwa kutabiriwa, mapendekezo yaliyochakaa yaliwasilishwa, na Mkutano huo ulihitimishwa kwa maazimio yaliyochakaa vilevile. Kikubwa kinachotolewa na watawala hao ni kulaani mauaji ya halaiki ya Gaza na ‘Israel’ na kuomba Umoja wa Mataifa (UN) - shirika lile lile lililohusika na kuzaliwa kwa umbile halifu la Kiyahudi.
Kwa mnasaba wa kupita mwaka mmoja wa mauaji ya kikatili yanayoendelea (mauaji ya halaiki) yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo yamepelekea kuuawa shahidi na kujeruhiwa Waislamu zaidi ya 160,000 wanaume na wanawake hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Indonesia iliandaa amali kubwa kwa anwani “Kukomesha mauaji ya halaiki nchini Palestina kunaweza tu kutekelezwa kwa kusimamisha Khilafah na kuhamasisha majeshi ya Kiislamu.”
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Hakika Makafiri wa Dunia Wamekusanyika dhidi yYetu!
Moto wa vita umeangaza anga, na jambo hilo liko wazi mithili ya usiku na mchana. Kuwanusuru Waislamu wa Gaza na Palestina hakutatokea, bila ya zana za kivita za majeshi ya Waislamu. Majeshi yetu ndiyo yalio na uwezo huu. Basi ni nini sababu, enyi Waislamu, kwamba tusikutane na maafisa wa kijeshi tunaowajua kibinafsi, na kujadiliana na kila afisa mmoja mmoja? Kwa nini tusiwatembelee ndugu wa maafisa hawa na kuwahimiza wachukue hatua za haraka? Ummah lazima uyatake majeshi yake yaondoe kila ukuta, na kushinda kila kizuizi, kinachosimama kati yao, na uharibifu wa uvamizi wa Mayahudi.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Ijapokuwa Ulimwengu wa Kiislamu Unatawaliwa na Mfumo wa Kikoloni!
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Maafisa Hawa wa Kijeshi Hawaishi ndani kabisa ya Misitu yenye Giza!
Kalima ya kutaka kupinduliwa kwa viongozi wa vikundi, kuregeshwa kwa maamuzi ya kijeshi, na kufunguliwa kwa mipaka.