Alhamisi, 01 Dhu al-Hijjah 1443 | 2022/06/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hukumu za Kifo za Al Sisi na Tukio la Ajabu la Erdogan na Misri

(Imetafsiriwa)

Katika muda wa miaka 10 kamili iliyopita, Erdogan, alipokuwa bado ni Waziri Mkuu wa Uturuki wakati huo, alitembelea Misri na kukutana na wawakilishi wa makundi tafauti na vyama vya kisiasa, pamoja na wagombea uraisi, katika kipindi cha mpito baada ya utawala wa Mubarak, ambao umeangushwa na Mapinduzi ya Kiarabu. Erdogan alipendekeza Usekula kwa Katiba mpya ya Misri wakati huo na kusema: “Sikubali kuwa usekula ni kutoishika dini, sikubali kuwa usekula ni kuipinga dini. Usekula sio kupinga dini. Katika tafsiri ya Chama cha AK ya usekula; Inasema kuwa mtu hatokuwa sekula, dola ndio yaweza kuwa sekula.” Waziri Mkuu wa Uturuki pia alitumia maneno “Msiogope usekula”.

Baada ya kauli hizi za Erdogan, Mahmoud Ghuzlan, msemaji wa Ikhwaan al-Muslimin, alimjibu Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, akiishutumu serikali ya Uturuki kwa kuingilia mambo ya ndani ya Misri na kusema: “Uzoefu katika nchi nyengine hauwezi kuigizwa Misri. Hali zilizopelekea kuanzishwa kwa dola ya kisekula Uturuki ni tafauti na zile za Misri.”

Baada ya matamko haya, uchaguzi ulifanyika Misri na Muhammad Mursi, mgombea wa kundi la Ikhwaan al-Muslimin, alishinda uchaguzi na kuwa Raisi wa Misri. Hata hivyo, baraza la kijeshi nchini Misri mara likafanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Mursi na kumwaga damu za maelfu ya Waislamu. Kikawaida, suala la kujaribu uzoefu wa Ikhwaan al-Muslimin nchini Misri haukutoa tishio kwa upande wa mataifa ya Magharibi na hasa kwa Amerika, kama ilivyo kwa AKP kuwa mamlakani, Uturuki haitoi tishio… Lakini Amerika haikuona muelekeo wa wazi juu ya njia inayoelekea mapinduzi ya Syria, ilichagua kufanya kazi na jenerali mpinduaji SISI nchini Misri badala ya Ikhwaan al-Muslimin. Hakika tunafahamu kuwa utawala wa Uturuki, kwa maana nyengine Erdogan, ulikuwa na uhakika kuwa Amerika ilikuwa nyuma ya mapinduzi ya Misri. Hata hivyo, serikali ya Uturuki ilielekea tu kwenye mazingatio ya kishujaa yasio ya kweli kuhusiana na mpangaji mapinduzi SISI. Mahesabu haya yalimfanya Erdogan kushinda siasa za ndani za Uturuki. Kimaumbile, kutokana na mazingatio haya ya kinafiki, kumekuwa na kuvurugika kwa mahusiano baina ya Uturuki na Misri na diplomasia kukatwa kabisa.

Baada ya miaka 8, hatua za kurejesha tena mahusiano zilianza kuchukuliwa baina ya Uturuki na Misri. Kwa kejeli, Raisi Erdogan amejaribu kuzioanisha hatua hizi kuwa ni mahusiano baina ya watu wa Uturuki na Misri, badala ya kuwa ni mahusiano ya kisiasa na kidiplomasia baina ya dola hizo mbili, Erdogan aliashiria mnamo March 2021 kuwa watu wa Misri na watu wa Uturuki hawatozozana baina yao, na kuwa hakuna tatizo baina ya watu wa mataifa haya mawili na akasema yafuatayo: “Muelekeo wetu kwa watu wa Misri ni chanya mno. Tunajitahidi kuuleta tena mshikamano wetu na Misri uliotokana na historia, sio kama ndugu maadui bali kama marafiki.”

Mbinu hii alioitumia Erdogan ni mfano wa ujanja wa kisiasa. Kwa sababu tatizo la kidiplomasia la miaka 8 baina ya Misri na Uturuki sio tatizo baina ya watu wa Misri na Uturuki. Baadhi ya watawala wa serikali ya chama cha AK, hasa Erdogan, alitumia kauli kama hii katika mchakato wa usawazishaji mahusiano ya Urusi na “Israel”. Wamechukua hatua za usawazishaji mahusiano kwa kusema kitu kama “Hakuna tatizo baina ya watu wa Urusi na watu wa Uturuki”, “Watu wa Israel na watu wa Uturuki ni marafiki”.  Kwa sababu hiyo, tatizo baina ya serikali ya Misri na ya Uturuki sio tatizo linalotokana na uadui wa watu, hivyo kulitatua kwa urafiki wa watu liko nje ya maudhui. Tatizo hili ni lenye kutokana na mahusiano baina ya watawala wa nchi, zaidi ya hivyo, tatizo linalotokana na mahusiano baina ya watawala wa Misri na Uturuki na Amerika. Kwa hivyo, ujanja wa kisiasa hufanywa ili watu wasije kusema kwa Erdogan kuwa “tokea ulipofanya amani, tokea ulipopeana mikono na Sisi, kwa nini ulibakia kuwa ni adui kwa miaka 8”. Kila mtu anatambua Misri na Uturuki ni nchi mbili ambazo zinaitegemea sana Amerika, kwamba zinatumikia maslahi ya Amerika katika siasa za kigeni, na Erdogan anaweza kujidanganya mwenyewe kwa ujanja wake wa kisiasa. Hivi karibuni, hukumu za kifo za makumi ya Waislamu zimefanyika na kutekelezwa. Je Erdogan, aliyejitokeza kwenye viwanja na alama ya “Rabia” (ya kuwaunga mkono Ikhwaan al-Muslimin wa Misri), ataweza kusema chochote kuhusu mauwaji haya? Hapana!

Kwa nini? Kwa sababu nchini Uturuki, siasa haziko kwa ajili ya utawala wala kwa ajili ya vyama vya upinzani vinavyoegemea misingi na maadili. Sio serikali wala upinzani kuwa unafanya siasa juu ya misingi na maadili. Kuna mambo mawili makubwa yanayoamua sera za vyama vya kisiasa nchini Uturuki: kwanza, maslahi na mapato yasiopatikana ndani yake, na pili, kuyafikia matarajio ya mataifa ya Magharibi kutokea Uturuki…

Vivyo hivyo, suala la kuwa Erdogan na viongozi wa vyama vyengine vya kisiasa kuonyesha hisia kwa mapinduzi ya Misri, ni kupata maslahi ya kisiasa katika siasa za ndani; na suala la serikali ya chama cha AK kubakia kimya kwa hukumu za vifo hivi leo ili kupata maslahi ya Amerika katika eneo, ni kufikia matarajio ya utawala wa Biden. Kwa mara ya kwanza katika miaka 30, ziara ya raisi wa Misri nchini Iraq inaonyesha kiasi cha umuhimu wa maslahi ya Amerika katika eneo. Kwa hivyo, Amerika inataka usawazishaji mahusiano, Uturuki inayakamilisha. Kwa sababu Misri na Uturuki ni nchi mbili muhimu katika eneo ambazo zinashindana kwa ajili ya maslahi ya Amerika.

Mpangaji mapinduzi, utawala wa SISI, polepole unaendelea kutekeleza adhabu za vifo. Serikali iliokuwa na hisia kali kwa Sisi wakati mapinduzi yalipotokea na kusema kuwa yupo dhidi ya mapinduzi katika viwanja na kuifanya alama ya “Rabia” kuwa ni nembo, alitumia ukandamizaji wa SISI katika siasa za ndani siku hiyo, na kuitumia kwa ajili ya siasa zake. Hivi leo, inapuuza adhabu za vifo kwa sababu lazima itekeleze maslahi ya Amerika katika eneo dhidi ya nchi za Muungano wa Ulaya. Serikali ya Uturuki inajitangaza kwa umma kuwa inatekeleza usawazishaji huu sio kwa sababu Amerika inataka hilo, bali ni kwa maslahi ya Uturuki katika Mashariki ya Mediterenia.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mahmut KAR

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Katika Wilaya ya Uturuki

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu