Jumatano, 30 Dhu al-Qi'dah 1443 | 2022/06/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uhalali wa Kimataifa Utatupeleka Wapi?

(Imetafsiriwa)

Taliban wametangaza kuwa wanajaribu kuunda serikali mpya nchini Afghanistan – serikali ambayo inataka mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliojengwa juu ya ‘kuheshimiana’ na Amerika na sehemu nyengine za dunia. “Imarati ya Kiislamu inataka kuwa na diplomasia nzuri, mahusiano ya kiuchumi na biashara pamoja na Amerika yanayoegemea katika kuheshimiana na usawa,” Bilal Karimi, afisa wa ngazi ya juu wa Taliban na mwanachama wa kamati ya utamaduni, ameiambia VOA. (Kumb: Sauti ya Amerika)

Kutokana na maendeleo ya hivi karibuni ya historia ya siasa ya mwanaadamu [hadi hivi leo], na kabla ya ujio wa sheria za kimataifa na kuachwa kwa tamaduni za kimataifa, uhalali wa Dola yoyote ulipatikana kimaumbile kwa njia ya nguvu zake na fikra pamoja na uwezo wake wa kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni. Hata hivyo, baada ya familia ya Dola za Kikiristo zilipoungana dhidi ya ufunguzi wa Khilafah wakati wa kumalizika kwa kipindi cha Khilafah Uthmaniya, walibadilisha hatua kwa hatua desturi za kimataifa kuwa sheria za kimataifa; matokeo yake hatimaye, kukaibuka mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Amerika baada ya panda shuka kadhaa.

Katika mfumo huo wa kimataifa unaoongozwa na sheria za kimataifa, sheria hizi hutungwa na dola kuu kupitia taasisi mbali mbali za kimataifa; makubaliano, maazimio, matamko na sera ambazo zinalazimishwa juu ya nchi dhaifu zilizopata uanachama kwenye mashirika hayo kupitia mchakato wa hadaa. Huku kukiwa hakuna dola yoyote tekelezi inayoweza kutabikisha sheria hizo juu ya wale waliozitunga sheria hizo.

Kwa hali hii, uhalali wa kimataifa kwa Dola zinazoibuka bila shaka zitahitajika kwao kuukubali kwa ukamilifu mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Amerika pamoja na wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hivyo, swali huzuka hapa kwamba je, serikali inayodai kuwa ni Dola ya Kiislamu, inayojinadi kwa muundo wa Dola ya Mtume (saw) na Makhalifah wake, inaweza kukubaliana na sheria za kimataifa zilizojengwa juu ya ‘Usekula’ na ufahamu wa Kimagharibi na kuweka mahusiano na nchi zote za dunia juu ya msingi wa ‘kuheshimiana’?! Ikiwa jibu ni ndio, basi maswali haya lazima yajibiwe. Je, haikuwa Dola ya Kiislamu ni yenye sera yake ya kigeni, na kulazimishwa kueneza ulinganizi wa Uislamu duniani kote kupitia Da’wah na Jihad?! Je, haikuwa sera ya kigeni ya Dola ya Kiislamu iliyoasisiwa wakati wa Mtume, Khilafah na wengineo ni kueneza Uislamu kupitia Da’wah na Jihad?! Je, ardhi hii kubwa ya sasa ya Ummah wa Kiislamu haikugeuzwa kuwa Dar-ul-Islam kupitia damu za Mujahidina na wafunguzi wa Ummah huu na je hili halikuwa ni kutokana na sera ya kigeni ya Dola anuwai za Kiislamu katika pindi chote cha historia ambapo sisi tumekuwa Waislam hivi sasa kama walivyokuwa mababu zetu?! 

Kwa hivyo, viongozi wa Dola iliochipuka ya Imarati ya Kiislamu lazima watambue kwa usahihi kuwa Dola ya Kiislamu ni yenye kutabikisha ‘Uislamu’ pekee katika nyanja zote za maisha na kuubeba kupitia sera yake ya kigeni [kwa njia ya Da’wah na Jihad] ikiwa ni moja ya majukumu ya Ummah kuelekea dunia kote. Ikiwa sehemu ndogo ya Uislamu inatekelezwa ndani ya nchi na huku uenezaji wa Uislamu kwa walimwengu ukifungwa kwa mfumo ulioundwa na binaadamu na/au sheria za kimataifa, basi hili litaharibu vibaya mno uhalali wa Dola ya Kiislamu na kushusha hadhi ya serikali kutoka kuwa ni Dola ya Kiislamu hadi kuwa ni Dola isiyokuwa ya Kiislamu. Lazima tuwe na hadhari sana kwa kutotenda hilo kwani Mwenyezi Mungu (swt) ametuonya wazi kabisa katika Quran. Kama Yeye (swt) alivyosema:

(وَأَنِ احْكُم بَيْنَهُم بِمَا أَنزَلَ اللَّهُ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ وَاحْذَرْهُمْ أَن يَفْتِنُوكَ عَن بَعْضِ مَا أَنزَلَ اللَّهُ إِلَيْكَ فَإِن تَوَلَّوْا فَاعْلَمْ أَنَّمَا يُرِيدُ اللَّهُ أَن يُصِيبَهُم بِبَعْضِ ذُنُوبِهِمْ وَإِنَّ كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ لَفَاسِقُونَ)

“Na wahukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao. Nawe tahadhari nao wasije kukufitini ukaacha baadhi ya aliyokuteremshia Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka, basi jua kwamba hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwasibu kwa baadhi ya dhambi zao. Na hakika wengi ya watu ni wapotofu.” [Al-Maidah: 49].

Katika mapambano kwa ajili ya uhalali; dunia, nchi za Kimagharibi, hasa Amerika zina wasiwasi mkubwa kwa Imarati ya Kiislamu kusimamisha Uislamu katika nyanja zote za maisha ya Waislamu; kukiuka sheria na mfumo wa kimataifa kwa njia ya sera ya kigeni ya Dola ya Kiislamu inayoibuka; na kuulingania Ummah wa Kiislamu kote katika ardhi za Waislamu kuingia katika susu la Dar-ul-Islam.

Vivyo hivyo, Magharibi na Amerika sio tu zinakhofu juu ya Imarati ya Kiislamu kuingia kwenye mtego wa uhalali uliowekwa na China na Urusi bali pia inatatizwa na kuwa ulimwengu wa Kimagharibi huenda ukakumbana na wimbi kubwa la wahamiaji pindi Taliban watapotekeleza ukandamizaji na udikteta. Hata hivyo, Taliban inakhofu juu ya vikwazo, matatizo ya kiuchumi na kutengwa kama waliotangulia; na hiyo ndio sababu hawataki kwenda njia sawa nao ili kutafuta utambulisho na uhalali wa kimataifa, na kuonyesha kubadilika badilika kwa hadhari ya polepole.

Kwa upande mwengine, pindi Amerika na Magharibi zikitokea kuitambua Imarati ya Kiislamu ya Taliban, basi uhalali wa vita vyao vya miaka 20 utazusha maswali; na kwa upande mwengine, kama Taliban watakuja kuonyesha ulegevu zaidi katika muelekeo huu, watakumbana na mzozo mkubwa wa ndani. Kwa hivyo, pande zote mbili zinakabiliana na changamoto kubwa na ngumu. Na zinachukua hatua za hadhari za kutatua tatizo polepole, lakini ulimwengu wa Kimagharibi unajitahidi ili hatimaye Taliban ijiyayushe ndani ya mfumo wa kiulimwengu na mfumo wa Dola ya Kitaifa, mwishowe kuifanya Afghanistan kwa mara nyengine tena, badala ya uvamizi wa kijeshi, ipitie uvamizi wa kikoloni [ujasusi na uchumi] wa nchi za kibepari. Kwa hivyo, katika hatua mwanzo, wale mukhlisina miongoni mwa Wataliban wasiruhusu Imarati ya Kiislamu kuelekea kwenye kufifia na kuweza kubadilika badilika pamoja na Magharibi; na katika hatua ya pili, Waislamu mukhlisina miongoni mwa Ummah wasiwaache Wataliban kuregelea kufeli kule kule yalikopitia makundi ya Kiislamu nchini Afghanistan. Kwa sababu sisi, Waislamu, tunalazimika kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt) na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu (swt) anatutosha dhidi ya Fitnah za watu na dhamira ovu za Wamashariki na Wamagharibi. Kama tumechagua kuwaridhisha watu na kwa jamii ya kimataifa badala ya kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt), basi Mwenyezi Mungu (swt) atatuacha mikononi mwa wavamizi na jumuiya ya kimataifa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

  مَنِ الْتَمَسَ رِضَاءَ اللَّهِ بِسَخَطِ النَّاسِ كَفَاهُ اللَّهُ مُؤْنَةَ النَّاسِ، وَمَنِ الْتَمَسَ رِضَاءَ النَّاسِ بِسَخَطِ اللَّهِ وَكَلَهُ اللَّهُ إِلَى النَّاسِ

“Anayetafuta kumridhisha Mwenyezi Mungu kwa ghadhabu za watu, Mwenyezi Mungu humtosheleza kutokana na watu. Na anayetaka kuwaridhisha watu kwa ghadhabu za Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamwakilisha kwa watu.”

#أفغانستان        Afganistan      #Afghanistan#       

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Saifullah Mustanir
Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Afghanistan

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu