Jumatano, 13 Rabi' al-awwal 1443 | 2021/10/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 China na Amerika: Vita, Mapambano au Udhibiti

(Imetafsiriwa)

Mnamo Septemba 24, 2021 viongozi wa ushirikiano usio rasmi wa Quad ulitangaza, “Kwa pamoja, tumejifunga tena kukuza mpango huru, ulioegemea kanuni za uwazi, zilizochimbuka katika sheria za kimataifa na zisizo na hofu ya shinikizo, kuimarisha usalama na ustawi katika Indo-Pacific na nje yake.” [1] Viongozi hawakuitaja China kuwa ni lengo kuu la kauli yao, lakini ilikuwa ni wazi kuwa Beijing ndio mlengwa hasa. Zaidi ya hayo, kutumika maneno Indo-Pacific badala ya Asian Pacific ni dalili wazi kuwa India, Amerika, Japan na Australia hazitovumilia utanuzi wa China katika eneo.

Mkutano wa Quad kwa haraka ulifuatiwa na tamko la AUKUS, ambapo Amerika, Uingereza na Australia zilitangaza mkataba mpya wa kijeshi wa nyambizi za nyuklia zitazokuwa Australia miongoni mwa mambo mengine. Mnamo 2016, Amerika na Uingereza ziliingia kwenye muungano wa kijeshi pamoja na Japan—ingawa suala la nyambizi za nyuklia kwa ajili ya Japan likiwa nje ya ajenda. China kwa ukali ilipinga hatua zote hizo mbili. China imeielezea Quad kuwa ni njia itayoendeleza daima vita baridi kiakili. [2] Kuhusiana na AUKUS, msemaji wa wizari ya mambo ya nje ya China, Zhao Lijian, amesema kuwa hatua hiyo “inazorotesha kwa kiasi kikubwa amani na usalama wa kieneo.” [3]

Wakati jitihada hizo zinaangaliwa katika muktadha wa mhimili wa Obama katika mkakati wa Asia na vita vya kibiashara na China wakati wa Trump, kuna hisia ya kuongezeka wasiwasi ambao huenda hatimaye Amerika imeshaelekea kwenye mvutano. Akiandika kwenye Financial Times, Edward Luce anaamini kuwa Amerika karibuni itapambana na China. [4] Wachunguzi wengine wanashikilia kauli kuwa Amerika imeshikilia mkao wa kuidhibiti China. Brands na Beckley wana maoni ya kuwa kwa kipindi cha miaka mitano iliopita Amerika imejiingiza katika udhibiti mpya kwa China. [5] Kwa mujibu wa Larson, Amerika imefufua tena mapambano kutokea zama za Vita Baridi (Cold War 2.0) kukomesha aina za ubaya muovu wa Urusi na China. [6] Wakati huohuo, John Ikenberry anawakilisha kundi dogo la wanafikra wanaoamini kwa dhati juu ya mapambano na China. Hii inajumuisha kuiunganisha China na sheria za Kimagharibi kwa msingi wa mfumo wa kimataifa. [7]

Maneno kama mgongano na mvutano mara nyingi yanahusishwa na vita, lakini hii ni kupotosha na haikisi kwa usahihi mahusiano ya Amerika na China. Tunazungumza kwa kauli pana kuwa maingiliano ya Amerika na mataifa yanaweza kugawanywa katika hatua tatu: vita, udhibiti na mapambano. Mapito ya hatua moja kwenda nyengine mara nyingi hayaonekani wazi, na wachunguzi kwa kawaida hutumia kauli kama mgongano au mvutano kuelezea mahusiano ya Amerika na taifa maalum.

Katika aina tatu hizo, vita hufahamika kwa wengi kwa matamko yake rahisi kuwa ni vurugu za kihatia za dola moja dhidi ya nyengine. Mapambano ni kuyapatia mataifa kile chenye kuhitajika - hata kama ni mataifa ya wabadilishaji itikadi ya kisiasa -  kwa kuwaingiza kwenye  kanuni za Kimagharibi zenye kuegemea mfumo wa kimataifa. Kwa njia hii, mataifa kama Urusi na China zitataka kushikilia kanuni za mfumo wa Kimagharibi hata kama mchango wa Magharibi kwa mfumo wa kimataifa upo katika kipindi cha mporomoko. [8]

Udhibiti ni fahamu ngumu kuipata kwa sababu ni yenye tafsiri tata. Kwa mujibu wa George Kennan – msanifu mkuu wa fahamu hii – udhibiti mara zote umekuwa ni kuhusu kuzuia ushawishi wa mfumo wa kikomunisti kote duniani, na sio kabisa kuhusiana na matumizi ya kijeshi ya sera ya nje ya Amerika. Akiandika katika kumbukumbu zake, Kennan alielezea kwa ufasaha fikra zake juu ya udhibiti kuwa “udhibiti wa kisiasa wa kisho la kisiasa”. [9] Inaelekea kuwa tawala zilizofuatia za Amerika kwa makusudi zimeipamba fikra ya udhibiti ya Kennan kwa kujumuisha kuzuia nguvu yoyote ya nchi kijeshi, kiuchumi, uwezo, upanuzi wa kieneo, na shauku za kimfumo zinazoelekea kuwa tishio kwa maslahi ya Amerika.

Mara tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, Amerika iliingia vitani na China kuzuia kuenea kwa Ukomunisti kwenye rasi ya Korea. Baada ya 1953, Amerika ilijiingiza kuidhibiti China kuzuia ushawishi wa mfumo wa kikomunisti katika eneo la Asia ya Pasifiki. Baadhi ya muda, Amerika iliendesha vita vya uwakala na Usovieti barani Afrika na China nchini Vietnam kusitisha ushawishi wa ukomunisti duniani. Hata hivyo, mtengano wa China na Usovieti uliofuatiwa na vita vya mpakani vya miezi 7 baina ya mataifa ya kikomunisti yaliyokuwa rafiki hapo awali mnamo 1969 yaliiwezesha Amerika kupunguza kuishughulikia China.

Baina ya miaka ya 70 hadi muongo wa kwanza wa karne ya 21, Amerika ilijaribu kuijumuisha China katika mfumo wa kimataifa. Kilele cha jitihada hizi kilikuwa ni msaada wa Amerika kwa China kuingia kwenye WTO. Mnamo katikati ya miaka ya 2000 China ilikuwa ikizingatiwa zaidi kuwa ni mshindani wa kimkakati wa Amerika. Kama vita nchini Afghanistan na Iraq havingewashughulisha Bush na Obama, Amerika ingeelekea kwenye udhibiti mpya kwa China mapema zaidi.

Hivi leo, Amerika imeachana na mapambano kwa ajili ya udhibiti au Vita Baridi 2.0. Amerika inafanyakazi pamoja na washirika wake kukabiliana kivitendo na jeshi la majini la China katika Bahari ya Kusini ya Asia. Kuifanya iwe vigumu kwa China kutatua Korea Kusini, Taiwan, na mizozo ya kieneo pamoja na majirani zake. Na kuidhoofisha OBOR katika Eurasia. Ni wazi kuwa tokea miaka ya1950, amri za kimfumo za Amerika zimekuwa katika kitovu cha mahusiano yake na China na hii imechukuwa sura ya vita, udhibiti na mapambano kupunguzwa nguvu na udhibiti mpya.

Hatua za vita, udhibiti na mapambano sio maalum kwa taifa maalum. Bali zipo kiujumla lakini zinasukumwa na mazingatio ya kimfumo. Dola ya mwanzo ya Kiislamu Madina kwa haraka ilifuata njia ya vita dhidi ya Maquraysh. Kabla ya Vita vya Badri na Uhud, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitekeleza uvamizi kadhaa dhidi ya Maquraysh akiwa na nia pekee ya kuchochea vita. Hali hii ya vita na Maquraysh ilibadilika kuwa hali ya udhibiti kupitia Mkataba wa Hudaybiyyah.

Mkataba ulimuwezesha Mtume (saw) kupunguza kwa kiasi kikubwa ushawishi wa Maquraysh katika Bara Arabu kwa kiasi cha kutekeleza vita na mapambano na makabila mengine na dola kwa wakati mmoja. Baada ya wiki mbili tu tokea kufunga mkataba, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliondoa nguvu ya Banu Khaybar waliokuwa washirika na Maquraysh. Mkataba pia ulimshajiisha Mtume (saw) kuyalingania waziwazi katika Uislamu makabila na mataifa yalio jirani na Arabia. Kwa hivyo, mapambano na makabila mengine na mataifa yalipunguza kwa kasi nguvu za Maquraysh na kutia moyo utanuzi wa Uislamu. Makhalifah baada ya Mtume (saw) waliendelea na vita (jihad), mapambano (ulinganizi wa Uislamu au kuishi chini ya Uislamu) na udhibiti (mikataba ya kusitisha vita), na hii ilipelekea kukuwa kwa kasi kwa Uislamu.

Hivyo Waislamu tusibaki tu kuwa watazamaji tukiangalia mjadala wa udhibiti au vita katika mahusiano ya Amerika na China. Bali, Waislamu ni lazima kufuatilia kwa uangalifu mahusiano baina ya China na Amerika ili kuitarajia nyakati za mvutano wa kiwango cha juu na kuipatiliza fursa ya kuirejesha tena Khilafah Rashida ya pili. Baada ya yote, Mtume (saw) alifuatilia kwa ubingwa mkubwa mkondo wa vita baina ya Warumi na Waajemi wakati aliposimamisha dola ya Kiislamu mjini Madina.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Abdul Majeed Bhatti

 

Marejeo

[1] Reuters, (2021).  Quad leaders press for free Indo-Pacific, with wary eye on China. Reuters. Available at: https://www.reuters.com/world/china/quad-leaders-meet-white-house-amid-shared-china-concerns-2021-09-24/

[2] Economic Times News, (2021). China says it firmly opposes Quad alliance as it adheres to Cold War mentality. Economic Times News. Available at: https://economictimes.indiatimes.com/news/international/world-news/china-says-it-firmly-opposes-quad-alliance-as-it-adheres-to-cold-war-mentality/articleshow/81692933.cms

[3] BBC, (2021). Aukus: UK, US and Australia launch pact to counter China. BBC, Available at: https://www.bbc.com/news/world-58564837

[4] Luce, E. (2021). A US-China clash is not unthinkable. Financial Times, Available at: https://www.ft.com/content/b3d41138-7dab-4a7f-9ed5-7b5ec7baf985

[5] Brands, H. and Beckley, M. (2021). The End of China's Rise: Beijing Is Running Out of Time to Remake the World. Foreign Affairs. 100(6).Available at: https://www.foreignaffairs.com/articles/china/2021-10-01/end-chinas-rise.

[6] Larson, D. (2021) The Return of Containment: What the Cold War policy means for our current moment. Foreign Policy, Available at: https://foreignpolicy.com/2021/01/15/containment-russia-china-kennan-today/

[7, 8] Ikenberry, J. (2014). The Rise of China and the Future of Liberal World. Chathamhouse. Available at:https://www.chathamhouse.org/sites/default/files/field/field_document/20140507RiseofChina.pdf

[9] Kennan, G. (2020) Memoirs 1925-1950. Plunkett Lake Press.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu