Jumatatu, 10 Rabi' al-awwal 1445 | 2023/09/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kamanda wa Jeshi Tunayemhitaji

(Imetafsiriwa)

Pamoja na mabadiliko katika amri ya jeshi la sita kwa ukubwa duniani, mjadala ulizushwa ndani, nchini Pakistan, na kiulimwengu, juu ya dori ya taasisi yenye nguvu ya kijeshi na mkuu wake wa jeshi. Mengi yamejadiliwa kuhusu urithi wa wakuu wa jeshi, waliomtangulia Jenerali Syed Asim Munir, Mkuu wa Jeshi wa Kumi na Saba wa jeshi la nyuklia, la tisa kwa nguvu zaidi duniani. Hata hivyo, zaidi ya urithi wa watangulizi, ambayo ni chanzo cha majuto na hasira, wajibu wa kamanda wa kijeshi wenyewe, lazima uwe mada ya tahadhari.

Kwa hivyo, ni aina gani ya kamanda wa kijeshi anayehitajika? Mkuu wa Majeshi nchini Pakistan ni dori ambayo inabeba mojawapo ya majukumu makubwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu (swt), Muumba wa wanadamu, katika ulimwengu wa leo. Dori ya kamanda wa kijeshi imewekwa kutoka kwa Amri ya Mwenyezi Mungu (swt), kwani Yeye (swt) Pekee ndiye Mwenye enzi juu ya maafisa wote wa kijeshi. Kwa hivyo, kamanda wa kijeshi hatakiwi kutilia maanani mafundisho ya kitaasisi ya Kimagharibi, au matakwa na matamanio ya watu wowote, yale yanayopendwa na yasiyopendwa ya jumuiya ya kimataifa ya wakoloni au chochote ambacho USCENTCOM taasisi ya jeshi la Marekani, Pentagon ya Marekani na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani inaweza kutaka “kukifanya zaidi”.

Urithi wa aliyetangulia, au aliye madarakani, Amiri Jeshi Mkuu unatathminiwa kwa mujibu wa Dini, ambayo Mwenyezi Mungu (swt) alituchagulia. Kauli mbiu ya vikosi vya Jeshi la Pakistan ni kielelezo cha Amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt), kuhusu dori ya mkuu wake. Mkuu mpya wa Jeshi anatoka katika Kikosi cha 23 cha Jeshi la Mpakani, ambacho kauli mbiu yake “Labbaik,” ni kielelezo cha kujisalimisha kikamilifu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kamanda wa jeshi wa kweli wa Kiislamu hasalimu amri, maagizo, miongozo, maazimio au amri za Taghut (mamlaka yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt).

Hakuna nafasi ya kumuasi Mwenyezi Mungu (swt), kwa kamanda wa kijeshi wa Kiislamu. Hakuna nafasi; kurudi kwenye kambi wakati wa ukandamizaji huku wakidai “kurudisha uadilifu wa kitaasisi,” wakiwa vipofu kwa ukatili dhidi ya Waislamu katika Kashmir Iliyokaliwa kwa mabavu na India kutokana na “uchumi wa kieneo,” kulegeza msimamo kwa dola za kimataifa za kikoloni kutokana na mafundisho ya lazima, kukengeuka na kuachana na kupigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kisingizio cha uchumi dhaifu na kuwa “kutojihusisha na siasa” kupitia kuunga mkono demokrasia, ambayo huharibu tu uwezo wetu na kuongeza masaibu yetu.

Historia ya ajabu ya Kiislamu imetufundisha kwamba makamanda wa kijeshi wanaoheshimiwa ni wale waliopigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), kulinda ardhi, maisha, mali na heshima ya Waislamu. Hivyo, Salahuddin, Sultan Muhammad Fateh, Mehmud wa Ghazni, Fahreddin Pasha na Tipu Sultan wanaishi ndani ya nyoyo na Dua za mabilioni ya Waislamu. Hata hivyo, Mir Sadiq na Mir Jaffer, ambao waliuza majeshi na watu wao kwa makafiri, wanachukiwa hadi leo.

Jenerali anayeheshimiwa tunayemhitaji sasa atabatilisha mpango wa Marekani wa kuimarisha India dhidi ya China, kwa kuhakikisha “kizuizi” cha Jeshi la Pakistan kutokana na “makosa” yoyote. Atakataa uungwaji mkono wa malengo ya kijeshi na kimkakati ya Marekani nchini Afghanistan, kupitia kutoa GLOC na ALOC ya ukanda wa anga wa “Boulevard”, ambayo inaruhusu droni za Marekani kupeleleza mali zetu nyeti za kijeshi. Atakomesha machapisho ya kijasusi ya Amerika ambayo yamejificha chini ya pazia la balozi, ambazo zinaweza kusikiliza mawasiliano yetu ya kijeshi. Atakataa kuitelekeza Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, ambayo inawaacha wanawake na watoto wetu kwenye huruma ya Jeshi la kikatili la India. Atakataa uingiliaji kati wa IMF na FATF nchini Pakistan, ambao unaharibu uchumi wetu na kudhoofisha jeshi letu.

Hivyo, jenerali mtukufu tunayemhitaji sasa, hajali chochote isipokuwa Amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Kamwe hatairuhusu Marekani kuwa na mamlaka yoyote juu ya mambo yetu. Kamwe hatashirikiana na kumsaidia adui mkubwa wa Waislamu, kufikia malengo yake ya kimkakati ya kieneo na kiulimwengu.

Kamanda wa kijeshi anayeheshimiwa tunayemhitaji sasa, kamwe hatalifungia jeshi lake kwenye kambi, wakati ambapo Nusrah yake inahitajika kusimamisha tena hukmu kwa Uislamu. Hakika Uislamu unaamrisha kuchukua hatua wakati wa dhulma na sio kutotenda. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلَا ‌تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Surah Hud 11:113].

Kamanda wa kijeshi tunayemhitaji ni mtoto muheshimiwa wa Answar, ambao kiongozi wao, Sa’ad bin Mu’adh (ra) alipata kifo chenye heshima zaidi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«اهْتَزَّ عَرْشُ الرَّحْمَنِ لِمَوْتِ سَعْدِ بْنِ مُعَاذٍ»

Kiti cha Enzi cha Mwingi wa Rehema (Mwenyezi Mungu) kilitikisika kwa sababu ya kifo cha Sa’ad bin Mu’adh.” [Bukhari]. Kuhusu kutikisika kwa Arshi kulikotajwa hapa, katika kitabu chake Fatah Al-Baaree, Ibn Hajar ameifasiri kwa kusema, والمراد باهتزاز العرش استبشاره وسروره بقدوم روحه “Maana ya kutikisika Arshi ni kupata kwake bishara njema na furaha yake kwa kupokewa roho yake.” Kifo hicho kitukufu kilikuwa baada ya kutoa Nusrah kwa ajili ya kusimamisha Dini, na Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kuieneza.

Baada ya kutoa Nusrah yake kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, kamanda huyo wa kijeshi atahamasishwa na Khalifa, kama tunavyohitaji. Khalifa kamwe hatawaacha wanawake na watoto wa Kiislamu kwenye huruma za madhalimu na wagandamizaji, iwe ni Kashmir au Palestina. Ataitikia wito wa waliodhulumiwa, kutuma Swalahudin mwenye utashi, akizingatia tu wajibu aliowekewa na Mwenyezi Mungu (swt). Khalifa hatawaacha Waislamu katika mtafaruku, wakigawanywa katika zaidi ya dola hamsini za taifa. Chini ya amri ya Khilafah yenye kuunganisha, Salahudin atatumwa kuwang'oa wasaliti na washirika wa makafiri. Na madhalimu wa dunia watapinduliwa, mmoja baada ya mwingine, kupitia jeshi ambalo hatimaye litawakomboa wanadamu kutokana na ukandamizaji wa sheria zilizotungwa na mwanadamu.

Dori ya kamanda wa kijeshi tunayemhitaji iko wazi. Nani ataibuka kutimiza matakwa yake, ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt)? Hiyo, inasubiriwa kuonekana.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Arsalan Farooq – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu