Ijumaa, 16 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Upigaji Marufuku na Ususiaji Inamfanya tu Mbebaji Dawah Kuwa Imara Zaidi!

(Imetafsiriwa)

Serikali ya Uingereza imepitisha marufuku iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu dhidi ya shughuli za wabebaji wa dawah. Kitendo hiki kimetokana na kufilisika kifikra na akili ya dola iliyofeli, kwani ulimwengu unajua Khilafah iko karibu.

Kuna idadi kadhaa ya mafunzo muhimu ambayo Waislamu na wabebaji dawah wanapaswa kuchukua kutoka katika hali hii mpya ya mambo. Jambo la kwanza ni kuelewa ni nini hasa kinachotarajiwa kutoka kwa hatua hii na jinsi hatupaswi kuingia katika mitego ambayo imewekwa kwa ajili yetu.

Kwanza, maadui wa Uislamu wanataka kutia hofu katika nyoyo za waumini, na wazo lenyewe ni kuwalazimisha Waislamu kutanguliza mambo ya dunia mbele ya hadhi yao katika Akhera. Hili limetajwa katika Quran katika Sura 8:2.

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللّهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ وَإِذَا تُلِيَتْ عَلَيْهِمْ آيَاتُهُ زَادَتْهُمْ إِيمَانًا وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُونَ]

“Hakika Waumini ni wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hujaa khofu, na wanapo somewa Aya zake huwazidisha Imani, na wakamtegemea Mola wao Mlezi.”

Mbinu za kutumia nguvu na vitisho dhidi ya Waislamu ili kuongeza hofu si jambo geni. Katika historia ya Uislamu, miaka 6 katika majaribio ya kuipotoa dawah na ulinganizi wa Uislamu, Wapagani hawakufanikiwa kabisa. Wakati maadui wa zamani walipojaribu kutumia kila silaha dhidi ya Waislamu kuanzia kwa matamanio na manufaa ya kidunia hadi kuwatishia kuwaondolea mafungamano ya kifamilia. Kanuni msingi katika Uislamu ni kwamba tusifanye ushirikina na kuweka washirika wowote pamoja na Mwenyezi Mungu (swt).

Katika zama za Mtume (saw) matusi na maoni hasi ya umma kuwakejeli Waislamu ilikuwa ni desturi maarufu.

[وَمِنْهُمُ الَّذِينَ يُؤْذُونَ النَّبِيَّ وَيِقُولُونَ هُوَ أُذُنٌ قُلْ أُذُنُ خَيْرٍ لَّكُمْ يُؤْمِنُ بِاللّهِ وَيُؤْمِنُ لِلْمُؤْمِنِينَ وَرَحْمَةٌ لِّلَّذِينَ آمَنُواْ مِنكُمْ وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ رَسُولَ اللّهِ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ]

“Na miongoni mwao wapo wanao muudhi Nabii na kusema: Yeye huyu ni sikio tu. Sema: Basi ni sikio la kheri kwenu. Anamuamini Mwenyezi Mungu, na ana imani na Waumini, naye ni rehema kwa wanao amini miongoni mwenu. Na wanao muudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watapata adhabu chungu.” [9:61].

Mateso na unyanyasaji wa umma yalinakiliwa vyema, kama tunavyojua kutoka kwa hadithi za Seerah. Leo sio tofauti; faradhi na wajibu wetu wa kufuata njia ya Mtume (saw) lazima vije mbele ya kipengele chochote cha viumbe na madai yao. Sisi tuko imara kama walivyokuwa Maswahaba walipokuwa wakikabiliwa na vitisho na adhabu za Maquraish na wafuasi wao dhidi ya Uislamu huku tunakumbushwa thawabu kubwa walizoahidiwa wale wenye subira.

[وَبَشِّرِ الَّذِين آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ كُلَّمَا رُزِقُواْ مِنْهَا مِن ثَمَرَةٍ رِّزْقاً قَالُواْ هَـذَا الَّذِي رُزِقْنَا مِن قَبْلُ وَأُتُواْ بِهِ مُتَشَابِهاً وَلَهُمْ فِيهَا أَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَهُمْ فِيهَا خَالِدُونَ]

“Na wabashirie walio amini na wakatenda mema kwamba watapata mabustani yapitayo mito kati yake; kila watapo pewa matunda humo, watasema: Haya ndiyo kama tuliyo pewa mbele. Na wataletewa matunda yaliyo fanana; na humo watakuwa na wake walio takasika; na wao humo watadumu.” [2:25]

Hii inapelekea kwenye lengo la pili la kupiga marufuku thaqafa, kutengwa, ambayo imeundwa kuleta udhaifu. Nguvu ya imani ya Waislamu leo na katika historia ni jambo ambalo makafiri wamekuwa wakipambana nalo. Leo wanatumia utaifa, na watawala wote wa Kiislamu ni watumwa wa kufanya kazi dhidi ya Waislamu na kuwatenganisha. Huko nyuma, walijua kwamba Abu Twalib alikuwa kizuizi cha utawala kwa vile alivyokuwa anamuunga mkono Mtume (saw). Walitarajia ama wangemshawishi Abu Twalib kuacha kumuunga mkono na kumlinda mpwa wake na Uislamu. Walitaka kumtenga Muhammad kutoka kwa ukoo wake ili kuondoa uwezo wake wa kupata rai jumla na kufanya maendeleo kwa wito wa nguvu ya Kiislamu. Ilikuwa ni jambo lisiloepukika kwamba jaribio lolote la kuwatenga Banu Hashim lingesababisha mgawanyiko wa makundi mjini Makka. Kila mtu mjini Makka angelazimika kujitangaza kwa ajili ya au dhidi ya Banu Hashim. Ni aina hii ya mgawanyiko ambao makafiri wanataka kuuweka katika jamii za Kiislamu. Ama uko pamoja na serikali za Magharibi au wewe ni adui wa kimsingi wa serikali ambaye lazima aangamizwe na kutupwa kihalisi nje ya muundo wa kijamii kabisa. Ndiyo maana sasa tunaona jinsi sheria zote za kisasa za muamala wa kibinadamu hazitekelezwi kwa Waislamu. Gaza ni mfano unaong'aa wa mtindo unaowekwa kwa ulimwengu wote wa Kiislamu. Utakuwa peke yako katika kifo chako na maangamivu na chombo cha kidunia kukusaidia.

Tunakumbuka hadithi za Waislamu walipokuwa wamefukuzwa jangwani na kuachwa bila mahitaji ya kimsingi kiasi kwamba binti kipenzi (ra) wa Mtume (saw) alikuwa na njaa na kudhurika kabisa kutokana na aliyoyapitia.

Tatu, kunaweza kuwa na jaribio la kupunguza dhihirisho wa kitambulisho cha mtu cha Kiislamu kwa kuona aibu kwamba unahusishwa na kitu ambacho hakiungwa mkono waziwawi na mfumo. Shinikizo la kujisalimisha kwa rai jumla na “kuunganishwa” zaidi ndani ya thaqafa isiyo ya Kiislamu ni njia hatari ambayo imeundwa kimkakati ili kuwa na athari ya kizazi. Hadith na dalili waziwazi zinakataza hili:

Imepokewa kutoka kwa Ibn Umar akisema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَنْ تَشَبَّهَ بِقَوْمٍ فَهُوَ مِنْهُمْ» “Mwenye kujifananisha na watu fulani basi naye ni miongoni mwao.” (Imesimuliwa na Abu Dawood).

Serikali zisizokuwa za Kiislamu zinajua kwamba Waislamu wana kitambulisho cha wazi ambacho wanataka kuwapa watoto wao kwa kuitikia dalili za Kiislamu:

(na inafahamika kuwa Waislamu hawapendezwi na hatua za kupanga uzazi ili kupunguza uzazi). Tuseme wanaweza kukishika kizazi cha wazazi katika wakati wa udhaifu wa kimfumo. Katika hali hiyo, tabia za kudidimiza kitambulisho chao cha Kiislamu ili kuendana nazo zitapitishwa kwa vizazi vyao. Uingizaji fikra hii unaoweza kusababisha maafa hauwezi kamwe kuvunjwa bila uingiliaji mkali katika nasaba na mafunzo. Bila shaka, wanawake ndio waelimishaji muhimu wa watoto, na ikiwa wanawake wanaweza kupatikana ili kuhatarisha kitambulisho chao, huu utakuwa ushindi dhidi ya makumi ya watu, sio mmoja tu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا]

“Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto” [At-Tahrîm: 6].

Kwa kumalizia, wabebaji dawah lazima wachukue funzo kutoka kwa mifano iliyopita ya Mtume (saw) na dalili katika Quran na Sunnah, na waelewe kwamba hatuna tofauti katika kuitikia kwetu ususiwaji na marufuku. Wabebaji dawah wa Kiislamu wanaofanya kazi katika Majal (eneo), ambako Khilafah itasimamishwa daima wamekuwa wakifanya kazi pamoja na kupigwa marufuku na kususiwa kwa mateso, kukamatwa na kutengwa kama desturi ya kila siku katika kazi yao. Hata hivyo, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu (swt), kamwe hawaogopi na hubakia thabiti na kiapo chao kwa Mwenyezi Mungu (swt). Muislamu anajua kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kweli, na walio bora zaidi katika waumini wanatazamia kukutana na Mola wao na kubadilisha amali zao kwa mafanikio makubwa zaidi, ambayo ni kuingia kwenye safu za Pepo pamoja na Mtume (saw) na Maswahaba (ra).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu