Jumatano, 11 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hakuna Suluhisho kwa Suala la Sudan Isipokuwa Kutawalisha Uislamu
(Imetafsiriwa)

Tangu uhuru wake mnamo tarehe 1/1/1956, Sudan imeshuhudia mfululizo wa mapinduzi ya kijeshi. Ya kwanza ilikuwa jaribio lililofeli lililoongozwa na Ismail Kabida, ambaye alijaribu kupindua serikali ya kwanza ya kitaifa iliyoongozwa na Ismail al-Azhari. Hii ilifuatiwa na mapinduzi ya kwanza yaliyofaulu yaliyoongozwa na Luteni Jenerali Ibrahim Abboud mnamo Novemba 1958 dhidi ya serikali iliyochaguliwa ya al-Azhari.

Mnamo Mei 1969, mapinduzi maarufu zaidi katika historia ya Sudan yalifanyika, yakiongozwa na Brigedia Jenerali Jaafar Nimeiri na kikundi cha maafisa wa kikomunisti na kitaifa. Utawala wake ulidumu kwa miaka 16. Alikabiliwa na majaribio kadhaa ya mapinduzi, ya kwanza yalifanyika mwaka 1971. Mnamo 1975, Nimeiri alifanikiwa kuzuia jaribio la mapinduzi dhidi yake, ambapo wapangaji wa mapinduzi waliuawa. Majaribio ya mapinduzi dhidi ya Nimeiri yaliendelea, na jaribio la mapinduzi la vurugu mnamo Julai 1976, na kufuatiwa na mapigano ya barabarani katika mji mkuu, Khartoum, kati ya vikosi vya serikali na wale waliopanga mapinduzi. Jaribio hili lilifeli na kiongozi wake aliuawa. Lakini baada ya changamoto hizi zote, mnamo Aprili 1985, utawala wa Nimeiri haukuweza kuhimili uasi wa wananchi. Aliondolewa madarakani. Field Marshal Abdel Rahman Swar al-Dahab, Waziri wa Ulinzi wa wakati huo, alishika urais wa baraza la mpito la kijeshi. Ni yeye pekee katika historia ya nchi na eneo hili aliyetimiza ahadi yake, akikabidhi madaraka mwaka mmoja baadaye kwa serikali iliyochaguliwa iliyoongozwa na Sadiq al-Mahdi. Hata hivyo, mwaka wa 1989, serikali hii pia ilikabiliwa na mapinduzi ya kijeshi yaliyoongozwa na Omar al-Bashir, ambaye alichukua nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Amri ya Mapinduzi ya Wokovu, wakati huo huo akihudumu kama Waziri Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Sudan.

Msururu wa mapinduzi ya kijeshi yamewakumba watu wa Sudan, na kuwaweka katika uharibifu wa vita na ukosefu wa utulivu. Hali hizi ziliendelea chini ya Omar al-Bashir, ambaye alitawala Sudan kwa mkono wa chuma kwa muda wa miaka thelathini, ambapo aliwaweka watu kwenye uchungu wa dhulma na ukandamizaji, pamoja na kuitumbukiza nchi katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Mnamo 1999, aliamuru kuvunjwa kwa Bunge la Kitaifa na kutangaza hali ya hatari kufuatia mzozo wa madaraka kati yake na Spika wa Bunge Hassan al-Turabi. Uasi dhidi ya al-Bashir na serikali yake uliendelea, na ulikabiliwa na ukandamizaji na mateso. Mwaka 2004, kwa mfano, vikosi vya jeshi vilihamia Darfur magharibi mwa Sudan ili kuangamiza vuguvugu la waasi ambalo lilituhumu serikali kuu ya Khartoum kwa kulitelekeza eneo hilo. Mamia ya maelfu ya watu wa Darfur walihamishwa hadi nchi jirani ya Chad, hali inayozidi kuzorota ya kisiasa iliyosifiwa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakati huo Colin Powell kuwa ‘mauaji ya halaiki’.

Mwaka 2005, serikali ilitia saini mkataba wa amani na waasi wa kusini, lakini ulikiukwa na uhalifu wa kivita ukatekelezwa. Katiba mpya ilitolewa ambayo ilitoa kiwango kikubwa cha uhuru wa kusini. Baadaye, kusini ilipata uhuru mnamo 2011 baada ya kura maarufu ya maoni.

Baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini, serikali ilipoteza mafuta iliyokuwa imezalisha kutoka mashambani mwake. Kusini ilichangia robo tatu ya pato la taifa. Sudan haikuweza kukidhi mahitaji yake ya mafuta na hivyo kupoteza chanzo kikubwa cha fedha za kigeni. Takwimu nyingi za kiuchumi zilithibitisha kuwa 90% ya Wasudan waliishi chini ya mstari wa umaskini na kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira kilizidi 60%. Mfumko wa bei ulifikia takriban 37% mwezi Juni 2012, na kupanda kwa kasi kwa bei za bidhaa na huduma zote, kulingana na kushuka kwa kiasi kikubwa kwa mapato ya mtu binafsi.

Wakati huo huo, serikali ilidai kuwa itaanza kutekeleza Shariah ya Kiislamu (Hudud) kwa ukali zaidi baada ya kujitenga kwa Sudan Kusini. Katika hotuba yake wakati wa kikao cha nne cha Chuo cha Fiqh cha Kiislamu, Makamu wa Kwanza wa Rais alisisitiza kwamba Omar al-Bashir ana shauku kubwa kwa Chuo hicho kuendelea kwenye njia ya kisayansi, mtazamo wa kimawazo, na “kuweka kipaumbele na kuvua hukmu za Shariah bila upendeleo.” Je, alikuwa anazungumzia vipaumbele gani? Serikali, ambayo ilifanya haraka kuwawekea watu Hudood (kanuni ya adhabu za Kiislamu) kwa watu, imenyima hata viwango msingi vya maisha, na kuwaacha waishi katika umaskini na mahitaji, haioni wasiwasi wowote kuhusu kuruhusu matumizi ya mikopo yenye riba (kutokana na ukosefu wa fedha wa serikali na haja yake ya ufadhili kutoka nje), kama inavyodai.

Serikali imefuata sera ya kifedha iliyofeli, kuwanyima wananchi ukwasi na kushindwa kuwapa unga wa mkate, jambo ambalo limewafanya watu wa Sudan washindwe kupata mahitaji yao ya kimsingi na kuwapatia mahitaji muhimu zaidi ya maisha. Mbali na hali ya afya, ambayo inachukuliwa kuwa mbaya; kulingana na takwimu iliyochapishwa na tovuti ya “Sudan Now” mwaka wa 2018, mtoto mmoja kati ya 20 nchini Sudan anaugua utapiamlo, na magonjwa kama vile malaria na kichocho yanaenea, na kufikia kesi milioni mbili!

Wananyanyua kauli mbiu ya kutabikisha Shariah na kuchagua kutoka katika hukmu zake, baada ya kuzifinyanga, zile zinazotumikia maslahi yao na maslahi ya Magharibi, na kuzitupilia mbali hukmu zengine. Hakuna utawala wa Uislamu katika siasa au bwana wa nchi. Wao ni wafuasi wa kafiri Magharibi, kwani wanaitegemea, wanakopa pesa kutoka kwake, wanatoa fatwa juu ya hilo na wanahalalisha, na wanaruhusu kuingilia mambo ya nchi yao na kuamua hatima ya watu wao. Hakuna huduma kwa watu wala uchungaji, wakati watu wa Sudan wana njaa na wanaishi katika umaskini wa kutisha. Je, ni aina gani ya Shariah wanayoitabikisha? Uislamu ni jumla usiogawanyika wenye sheria na mipaka yake, inayotabikishwa kama mfumo kamili wa maisha ambao Mwenyezi Mungu ameuchagua kwa waja wake, na hakuna mja mwenye haki ya kuchagua baadhi yake na kuacha mengine. Yeyote anayechagua kutekeleza Shariah lazima azitii sheria zake zote bila ya kupunguza chochote kutoka kwazo.

Kuondolewa kwa ruzuku juu ya mkate na mafuta, kupanda kwa bei za bidhaa kimsingi, uhaba wa bidhaa nyingi, kuendelea kwa sera za kifedha zilizoamriwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na wengineo, na kuzorota kwa hali ya afya kulikuwa na athari kubwa katika kutoridhika kwa watu wote wa Sudan na mfumo wao wa maisha, hali ya kutoridhika ambayo ilienea kote nchini na kuwa mbaya zaidi kila uchao. Ufisadi wa utawala wa Omar al-Bashir na kushiriki kwake katika kuchezea fedha za serikali ulidhihirika wazi. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kimataifa la Uadilifu wa Kifedha imefichua kuwa utawala huu ulificha takriban dolari bilioni 31 katika mauzo ya nje ya Sudan kati ya 2012 na 2018. Serikali ilitangaza kuwa mauzo ya nje ya nchi hiyo yalifikia dolari bilioni 65 katika kipindi hicho kilichotajwa, huku nchi 70 za washirika wa kibiashara wa Sudan, zikikadiria uagizaji wao kuwa takriban dolari bilioni 96. Kulaani na maandamano yalizuka, na moto wa mapinduzi ulizuka dhidi ya serikali hii katika miji yote ya Sudan. Ilipinduliwa mwaka 2019 baada ya Wizara ya Ulinzi kutangaza kuwa Al-Bashir amejiuzulu wadhifa wake na kwamba jeshi litasimamia masuala ya nchi.

Licha ya kupinduliwa kwa utawala wa Bashir, mateso ya watu wa Sudan yanaendelea chini ya kivuli cha mizozo inayoendeshwa na nchi za Magharibi na kusimamiwa na mashirika yao. Mateso haya hayatakoma na hayatakwisha isipokuwa Shariah itabikishwe kikamilifu na nchi itawaliwe na wale wanaomcha Mwenyezi Mungu peke yake, wasionyenyekea kwa adui, bali wanafanya kuinua bendera ya Uislamu kuwa lengo lao na kutekeleza kanuni zake ndio lengo lao.

أزمة_السودان #     #SudanCrisis

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeena As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu