Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Kampeni “Katika Kumbukumbu ya Miaka 14 ya Kutekwa Nyara Kwake… Mwachilieni Huru Naveed Butt!”
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan ilizindua kampeni ya mitandao ya kijamii, haswa kwenye mtandao wa X (zamani ikijulikana kama Twitter), yenye kichwa “Katika Kumbukumbu ya Miaka 14 ya Kutekwa Nyara Kwake... Mwachilieni Huru Naveed Butt!” Kampeni hii inalenga kuishinikiza serikali dhalimu ya Pakistan, ambayo huduma zao za siri zilimteka nyara Mhandisi Naveed Butt, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir nchini Pakistan, miaka 14 iliyopita mbele ya familia yake na majirani zake.



