Jumapili, 15 Rajab 1444 | 2023/02/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Kisimamo cha Al-Aqsa "Khiyana ya Watawala wa Waislamu na Uovu Wao Umewapa Ujasiri Waabudu Ng'ombe Juu ya Cheo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu."

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) iliandaa kisimamo katika nyua za Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kwa ajili ya kumnusuru Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kuyahamasisha majeshi ya Waislamu kuwang’oa watawala wasaliti na kusimamisha dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na kuchukua hatua mara moja ya kuwaadhibu wale wote waliosubutu kuasi dhidi ya mbora wa viumbe, bwana wetu Muhammad, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.

Ijumaa, 11 Dhul-Qa’adah 1443 H – 10 Juni 2022 M

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Walimwengu wote, Mwenye nguvu

Anayeweza kuwasagaga madhalimu; Yule mwenye kusema katika Kitabu Chake Kitukufu: مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاء عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاء بَيْنَهُمْ   "Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao." [Al-Fat’hi: 29] Na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, aliyesema: «أَنَا سَيِّدُ وَلَدِ آدَمَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا فَخْرَ وَبِيَدِي لِوَاءُ الْحَمْدِ وَلَا فَخْرَ» “Mimi ni bwana wa wanadamu Siku ya Kiyama wala sijifakhiri kwa kiburi na bendera ya (Liwaa) shukrani itakuwa mkononi mwangu wala sijifakhiri kwa kiburi.”

Naomba shifaa yako ewe bwana wangu, ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Makafiri wanahujumu cheo chako, watawala wetu ni wasaliti na viongozi wa majeshi yetu ni wazembe. Enyi Waislamu, hapa mnaona jinsi makafiri wanavyomtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimshukie, na kuendelea kwao kuvuka mipaka juu ya cheo chake kitukufu. Matusi ya Ufaransa yalikuwa karibu kutoweka kutoka kwetu, wakati matusi ya Mabaniani waabudu ng’ombe kwa ndimi za baadhi ya wasemaji wa chama tawala nchini India yalipotujia.

Enyi Waislamu, matusi haya si chochote ila ni vita dhidi ya Uislamu na Waislamu; juu ya imani zetu, ardhi, mali, heshima, Hijab ya wanawake wetu na mshikamano wa familia zetu. Kwa sababu ya hayo yote wanajaribu kumhujumu Mtume wetu, Mwenyezi Mungu ambariki na ampe amani. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema kweli pale aliposema (swt):قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ  “Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aali- Imran: 118]

Vita hivi dhidi ya Waislamu vinaduru baina ya makafiri, Marekani na uvamizi wake dhidi ya Iraq na Afghanistan, Uswidi na utekaji nyara wake wa watoto wa Kiislamu. Ufaransa inavuka mipaka wakati mmoja, Warusi, wengi; China, na nini kitakuwezesha kujua uhalifu wa China? Sasa wanakuja Mabaniani waabudu ng'ombe, waliobomoa misikiti, wakaua Waislamu na kuchoma vijiji vyao; hapa wanasubutu kutusi cheo cha Bwana wa Wanaadamu, Muhammad, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na hilo ni jambo ambalo linaweza kujibiwa kwa jambo moja tu. Yaani tamko la Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu na kufunguliwa kwa safu za vita, ili silaha iseme neno lake katika kuwatia adabu makafiri na washirikina, na kung'oa mizizi yao. Ewe Mwenyezi Mungu, tuletee kwa haraka kiongozi mithili ya Khalid bin Al-Walid.

Uhaini wa watawala wa Waislamu na uovu wao, unawashajiisha waabudu ng'ombe kutukana cheo cha Mtume wa Mwenyezi Mungu, Bwana wa Wanaadamu; na sisi, kutoka katika Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa, tunatoa hotuba yetu kwa majeshi ya Waislamu nchini Misri, Hijaz, Uturuki, Jordan na ardhi zote za Waislamu, na tunawaambia: Mko wapi? Je! haujafika wakati kwenu kuinusuru Dini yenu na Mtume wenu, na kukomboa ardhi zenu na Masra zenu? Tunawaambia viongozi wa majeshi haya kwamba utegemezi wenu kwa Marekani, na watawala makhaini umekufanyeni mupoteze utu wenu, na kuyafanya majeshi yenu yapoteze thamani na maadili, na kuyasahaulisha wajibu wao kwa Ummah wao na Dini yao, hivyo maadui wa Uislamu wakasubutu kukiuka mipaka dhidi ya matukufu yote, na wakafanya madhambi makubwa dhidi ya Waislamu, yote haya ni kwa sababu ya uzembe wenu, na kunyamaza kwenu kimya dhidi ya watawala hawa.

Basi ni nani, Enyi Makamanda na Maafisa wa majeshi, atakuwa kiongozi shupavu Mpiganaji jihad, anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na akajitwika jukumu la kuyakomboa majeshi haya kutokana na utiifu wao kwa maadui wa Ummah na watawala waovu, na awaongoze katika viwanja vya vita vya Jihad kuinusuru Dini ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie.

Nanyi, enyi watu wa Pakistan:

Uhamasikaji wenu wa kupigana na Mabaniani ni wajibu zaidi kuliko kuwahamasisha wengine, kwani wao wako kwenye mipaka yenu, wanazikalia ardhi zenu na wanaua watu wenu, na hakika nyinyi mna jeshi kubwa lenye uwezo wa kuwatia adabu, na kuwasahaulisha minong'ono ya Shetani. Basi kwa nini mnakaa kimya juu ya utegemezi wa jeshi lenu kubwa, pamoja na silaha, askari, maafisa na taasisi zake kwa matakwa ya Amerika, ambalo hupigana Amerika inapopigana na kufanya amani inapofanya amani, kutokana na hayo hawakuja kuwasaidia ndugu zao wa India kutokana na ukandamizaji wa Mabaniani, ingawa Mwenyezi Mungu (swt) asema: وَإِنِ اسْتَنصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ “Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Anfaal: 72]

Na hawakutangaza Jihad katika kuuhami Uislamu, Mtume wa Uislamu na Aqsa, Masra ya Mtume wa Uislamu, na Mtume Wetu asema: «مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً عِنْدَ مَوْطِنٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ» “Hakuna mtu yeyote (Muislamu) atakayemtelekeza Muislamu katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa na heshima yake kuvunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamtelekeza katika sehemu ambayo angependa nusra Yake.”

Ama kwa nyinyi, enyi Waislamu katika nchi zote za Waislamu:

Maafisa na makamanda wa majeshi ni watoto wenu na ndugu zenu, na ni juu yenu kuwataka watimize wajibu wao ambao Mwenyezi Mungu amewawajibisha juu yao na nyinyi; wajibu wa kuinusuru na kuisaidia Dini ya Mwenyezi Mungu, na vile vile wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Dini hii kupitia Khilafah Rashida, na Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hakika kheri katika Ummah huu ni halisi, na Ummah wa Muhammad (saw) kamwe hautakosa maafisa, mabrigedia na majenerali watakaoregesha upya izza ya Mujahidina, Maswahaba na Wafunguzi.

Basi simameni kwa watoto wenu, maafisa wa majeshi, na muwasukume kwenye izza ya Dunia na Akhera. Wakeni juu yao neno la uongofu na muwafanye walitendee kazi; na pandeni ndani ya nyoyo zao hamu ya kusimamisha Khilafah ya Uislamu, ukombozi wa Al-Aqsa, na kusimama na Mtume, rehma na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie.

Ewe Mwenyezi Mungu mshuhie rehma na amani zako, mja na Mtume wako Muhammad. Rehma ambazo kwazo Ummah wake utashinda kupitia Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo kwayo Utaufanya Uislamu na Waislamu kuwa washindi, na kudhalilisha ukafiri na makafiri. Ewe Mwenyezi Mungu ijaalie kheri hii iwafikie Waislamu na uwaongoze kwayo.

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa Walimwengu wote.

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina):

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Media

https://s3.htcmo.com/htmedia/nidaat/2022/06/Nidaa_alaqsa_Siam10062022.mp4

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu