Jumanne, 29 Sha'aban 1444 | 2023/03/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kampeni ya Kitengo cha Wanawake katika Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Khilafah

 “Mabadiliko ya Kweli ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah Pekee”

"Je, Khilafah ni Ndoto Isiyowezekana?"

Ili kufuatilia Matangazo ya Moja kwa Moja

Bonyeza Hapa

Video ya Uzinduzi wa Kampeni

Dunia iko katika machafuko. Nchi zinatumbukia katika mgogoro baada ya mgogoro chini ya tawala zilizoundwa na binadamu - ambazo zote zimethibitisha kutokuwa na uwezo wa kutatua matatizo ya binadamu. Umaskini, njaa, mauaji ya halaiki, uonevu, ufisadi, vita visivyo na maana, ukaliaji kimabavu, kusambaratika kwa familia, kuenea kwa uhalifu, unyanyasaji dhidi ya wanawake, migogoro ya afya na elimu, maisha yenye uharibifu, na matatizo mengine yanayokumba nchi kutoka mashariki hadi magharibi. Je, tutayamaliza vipi haya yote? Je, tunatokaje kwenye kinamasi hiki?

Mabadiliko ya kweli hayawezi kupatikana kwa kurudisha mzunguko wa mifumo iliyofeli - demokrasia au mengineyo. Mabadiliko haya hayawezi kufikiwa kwa kutoa tu marekebisho ya sehemu au suluhu za viraka kwa mifumo hii ya sasa yenye kasoro. Badala yake, inahitaji mabadiliko makubwa, ya msingi na ya kina.

Inahitaji kuzaliwa kwa mfumo badali unaobeba masuluhisho ya kihakika kwa matatizo ya binadamu, Inatutaka sisi kama Waislamu kuregea katika yale ambayo Mwenyezi Mungu ametuitia kwayo: Hukmu na mfumo Wake... na kuutabanni ujumbe wa Uislamu... ili kuasisi uongozi wa kweli kwa ajili ya wanadamu...

Khilafah kwa njia ya Utume

Katika mwezi wa Rajab, Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kinazindua kampeni ya kimataifa yenye kichwa:

"Mabadiliko ya Kweli ni kwa kupitia Ulinganizi wa Khilafah Pekee"

Kampeni hii itaonyesha jinsi Khilafah kwa njia ya Utume itakavyozihuisha nchi za Kiislamu na kuzitoa katika hali ya machafuko na hasara zinamoishi, na kuonyeesha dhima iliyo juu yao ya kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi zao na dunia kwa jumla. Kampeni hii pia itadhihirisha iwapo mabadiliko msingi na kusimamishwa kwa Khilafah ni ndoto tu au ni uhalisia unaoweza kufikiwa.

Tunatoa wito kila mtu anayetaka kuona mustakabali mwema kwa nchi za Kiislamu na ulimwengu huu, kuunga mkono kampeni hii muhimu, ambayo inaweza kufuatiliwa katika anwani zifuatazo:
FB – QANITATHT2
Twitter – @WSHARIAHA
Instagram – @WOMEN_SHARIA

Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M

- Kufuatilia Kampeni Hii kwa Lugha Nyenginezo -

Kiarabu Kiingereza
Kituruki Kijerumani
Kiurdu  Fuatilia na Usambaze

 

Ushiriki wa Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina

Katika Amali za Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Khilafah

Jumapili, 28 Rajab 1444 H - 19 Februari 2023 M

Kalima ya Dkt. Nazreen Nawaz

Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka 102 ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah

Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M

- Alama Ishara za Kampeni -

#ReturnTheKhilafah

#KhilafaBringsRealChange

#YenidenHilafet

#HakikiDeği