Jumanne, 14 Shawwal 1445 | 2024/04/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Angazo la Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa Dola ya Khilafah 1444 H – 2023 M

Katika mwezi wa Rajab Tukufu wa mwaka huu 1444 H - 2023 M, na kwa mnasaba wa kumbukumbu chungu ya wahalifu wa Kiarabu na wa Kituruki, kuivunja dola ya Uislamu iliyoasisiwa na bwana wa Mitume wote, Muhammad (saw), na maswahaba zake watukufu, Mwenyezi Mungu awawie radhi, na kuundoa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu mwaka 1342 H sawia na 03/03/1924 M, Hizb ut Tahrir inapanga amali kubwa za halaiki katika nchi zote inamofanyia kazi, na sisi katika afisi kuu ya habari ya Hizb ut Tahrir, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kupitia ukurasa huu, tutaangazia amali hizo kwa ukamilifu, tukimuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakisha kusimamisha kwa dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

((وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ)).

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Jumatatu, 01 Rajab Tukufu 1444 H – 23 Januari 2023 M