Alhamisi, 10 Muharram 1448 | 2026/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Baada ya Mwaka Mmoja wa Mauaji ya Halaiki (na Miaka 76 ya Ukaliaji Kimabavu), Watawala wa Ruwaibidha Wakusanyika Tena Kuendeleza Kejeli na Usaliti wao

Ni mwaka mmoja kamili baada ya watawala wa Waarabu na Waislamu kukusanyika kujadili kadhia ya Palestina kufuatia mkasa wa Oktoba 7, wanakutana tena mahali pale pale, pamoja na mtu yule yule, wakishughulikia tatizo lile lile, na hatimaye kutoa maazimio yale yale! Zaidi ya viongozi 50 wa dola za Waislamu walihudhuria Mkutano wa Waarabu na Waislamu mnamo tarehe 11/11/2024, akiwemo Waziri Mkuu wa Malaysia. Kwa kutabiriwa, mapendekezo yaliyochakaa yaliwasilishwa, na Mkutano huo ulihitimishwa kwa maazimio yaliyochakaa vilevile. Kikubwa kinachotolewa na watawala hao ni kulaani mauaji ya halaiki ya Gaza na ‘Israel’ na kuomba Umoja wa Mataifa (UN) - shirika lile lile lililohusika na kuzaliwa kwa umbile halifu la Kiyahudi.

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi “Gaza Inamwachia Mwenyezi Mungu Kiwango cha Usaliti jijini Riyadh na inataka Msaada kwa Umma na Majeshi yake!”

Matembezi ya hamsini na nane ya kunusuru Palestina na mateka Al-Aqsa, ambayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, chini ya kichwa “Gaza Inamwachia Mwenyezi Mungu Kiwango cha Usaliti jijini Riyadh na inataka Msaada kwa Umma na Majeshi yake!”

Watawala wa Iran ni Uhalisia tu wa Sauti na Maonyesho ya Fataki Hawana Uhusiano Wowote na Ushindi au Ukombozi

Kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Iran, Meja Jenerali Hossein Salami, alithibitisha katika ufunguzi wa mazoezi ya mapambano ya usalama ya “Nasrallah” kwamba “umbile la Kizayuni linakosea ikiwa linadhani kuwa Hizbullah itatoka nje ya uwanja kwa kuwauwa viongozi wake,” na kubainisha kuwa “chama hicho ni vuguvugu kubwa ambalo haliwezi kuzimwa wala kumalizwa.” Akalitisha umbile la Kiyahudi kwa kusema: “Leo tuna nyinyi machoni mwetu, na tutapigana mpaka mwisho, na hatutakuruhusuni kudhibiti hatma ya Waislamu, na tutalipiza kisasi, nanyi mtapata pigo chungu, na lazima musubiri.”

Sura Mpya ya Walaji Njama katika Astana 22 Imetanguliwa na Mkutano huko Tarnaba na Majadiliano kuhusu Kufungua Barabara na Vivuko vya Kimataifa

Enyi Wana Mapinduzi: Tusikilizeni, sisi ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir Al-Nadheer Al-Aryan (mwonyaji wa wazi), ndugu zenu ambao mumeyaona maneno yao kuwa ya kweli na ambao kuona kwao ni kukubwa. Sisi hatuhitaji fadhila katika jambo hili juu yenu, kwani huu ni wajibu wetu na tutakutana nao kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Tunakuombeni nyinyi, watu wetu, mufanyeni haraka kuregesha uamuzi wenu kutoka kwa waliouiba, kwani nchi na zana zao ni mikono yenye nia mbaya inayotaka kukuangamizeni.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu