Alhamisi, 10 Muharram 1448 | 2026/06/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Kuchochea Migogoro ya Kimadhehebu ni Mtazamo Uliofichuliwa wa Mayahudi katika Kushinikiza Mauaji na Suala la Kuhama Makao!

Mauaji nchini Lebanon yanaendelea tangu Mayahudi walipoanza uvamizi wao wa kikatili na wa kinyama dhidi yake na watu wake kwa jumla, na dhidi ya watu wa kusini haswa, hadi idadi ya wahasiriwa nchini Lebanon ikazidi 3200, na idadi ya waliojeruhiwa ikafikia 14,000, na karibu watu milioni 1.2 wamelazimika kuyahama makaazi yao, katika sera inayotekelezwa na adui huyu mnyakuzi nchini Lebanon, na alifanya hivyo hapo awali na anaendelea kufanya vitendo hivi katika Ukanda wa Gaza unaoheshimika kwa zaidi ya mwaka mmoja!

Waislamu nchini Denmark Kamwe Hawatajioanisha na Maadili ya Serikali ya Mauaji ya Halaiki

Katika mahojiano ya kina na ya jukwaani na Jyllands-Posten mnamo Novemba 18, 2024, Waziri Mkuu Mette Frederiksen anafanya juhudi kubwa kutoa taswira kali ya idadi ya Waislamu wa nchi hiyo. Anatuhumu Quran kuwashajiisha Waislamu kufanya uhalifu, kuwapiga watoto wao, na kujihusisha na tabia ambayo inaleta ukosefu wa usalama katika maeneo ya umma. Hatari inayodaiwa kuletwa na Waislamu wanaoishi Denmark inalinganishwa na tishio la “Urusi na Putin.”

Bila Mfumo wa Elimu ya Kiislamu, Haramu inakuwa ni Sharti la Kusoma

Mnamo tarehe 16 Novemba, gazeti la Times la India liliripoti kwamba Chuo Kikuu cha Uttarakhand Sanskrit huko Haridwar kimeanzisha hatua za kutekeleza uamuzi wa Mahakama ya Upeo juu ya mavazi ya wanafunzi ndani ya chuo kikuu na madarasani, Makamu wa Chansela wa Chuo Kikuu Dinesh Chandra Shastri aliiambia TOI mnamo Alhamisi. Hatua hiyo imekuja baada ya malalamiko kuwa “wanafunzi kadhaa wa Kiislamu wa kike wanaendelea kuvaa burka au hijabu wakiwa chuo hicho kikuu.”

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu