Kukamatwa Kupya kwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir nchini Yemen na Mahouthi Je, kauli mbiu “Kifo kwa Amerika” inawezaje kuishi sambamba na Kutetea Mpango wa Trump kuhusu Gaza?!
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Mnamo Alhamisi, 27/11/2025, vikosi vya usalama vya Mahouthi vilimkamata Saddam Ali Qa’id al-Mukirdi, mwenye umri wa miaka 28, kutoka wilaya ya Ṣabr al-Mawadim katika Mkoa wa Taiz ulio chini ya udhibiti wa Mahouthi katikati mwa Yemen. Kukamatwa huku ni kwa pili, kufuatia kukamatwa kwa ndugu Osama na Mohammad Mas’ad Al-Wurafi katika Mkoa wa Ibb mnamo 21/11/2025, baada ya kugawanya toleo lenye kichwa: “Trump Awaongoza Wafuasi Wake Miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mpango wa Fedheha na Aibu, Wanaosujudu Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza ya Hashim Chini ya Udhamini na Ukoloni.”



