Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 583
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 583
Vichwa Vikuu vya Toleo 583
Ni sababu gani za udhaifu wa Waislamu leo? Kwa nini heshima yao inavunjwa, ardhi yao inanyakuliwa, na wanamefukarishwa na kutiwa njaa, lakini hawajitetei dhidi ya dhulma, udhalilifu, na kudunishwa? Kwa nini wanatazamana wakifa kwa njaa, mauaji, na mateso mikononi mwa makafiri wahalifu bila kuinua kidole? Kwa nini wanahisi hawana msaada, dhaifu, na watiifu kwa Magharibi mbele ya majanga na vitisho vyote vinavyowapata?
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Khilafah, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon ilifanya kongamano lake la kila mwaka la kisiasa kwa kichwa: “Kuhalalisha Mahusiano na Kujisalimisha, au Ahadi ya Mwenyezi Mungu na Dola ya Uislamu?!”, ambapo wazungumzaji kutoka Lebanon, Syria, Uturuki, na Gaza walishiriki.
Mnamo Jumamosi, tarehe 28 Rajab 1447 H, sambamba na tarehe 17 Januari 2026 M, Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan ilifanya kongamano la kumbukumbu ya miaka 105 tangu kuvunjwa kwa dola ya Kiislamu ya Khilafah. Kongamano hilo lilihudhuriwa na watu mashuhuri, wakiwemo wanasiasa, watu mashuhuri wa vyombo vya habari, wasomi, na viongozi wa jamii. Kwa kuzingatia kwamba kumbukumbu hii chungu inakuja huku sisi nchini Sudan tukiteseka kutokana na vita vilivyowashwa na ubeberu wa Marekani, ikiwatumia vibaraka wake wa ndani kusambaratisha kile kilichobaki cha umoja wa nchi yetu chini ya sera yake inayoitwa “Mipaka ya Damu”. Hivyo, kichwa cha kongamano letu kilikuwa: “Sudan Kati ya Sera za Mipaka ya Damu na Kuunganisha Watu Kuwa Umma Mmoja.”